Kwanini Kanisa limejengwa katikati ya madarasa?

Nimesoma pale a level, kanisa halipo katikati ya madarasa, lipo pembeni kabisa
 
Sio shule zote zilikuwa za Catholic ndugu mkupuo .
Mazengo Complex ilikuwa ni ya Anglican.
Msalato Girls ilikuwa ni Anglican.
sasa umekosoa nn , hoja ni kuwa ukikuta shule ina kanisa basi ujue iliwai kuwa mali ya kanisa ikataifishwa
 
Siyo shule zote ni za wakatoliki jifunzage kuandika taarifa sahihi. Kwa hiyo hata Ilboru(Arusha) ilikuwa ya wakatoliki? Acha ushabiki wa kidini andika tarifa sahihi kwa faida ya wasioujua hasa vijana wa siku hizi
unamshambulia kwavile kawakosoeni au mnamshambulia kwavile hamuna hoja mpya ?
 
sasa umekosoa nn , hoja ni kuwa ukikuta shule ina kanisa basi ujue iliwai kuwa mali ya kanisa ikataifishwa
Una uelewa mfinyu sana wa mambo au wewe ni "slow learner".
Nimeandika kuwa si shule zote zilikuwa za Kanisa Katoliki kama alivyoandika niliyemnukuu, kwani huo ni upotoshaji.
 
🤔🤔🤔🤔
 
Uongo

Minaki ilikuwa shule ya wa Anglikan.Sio wakatoliki
 
Ila tukubali asilimia nyingi shule zilikua za wakatoliki zilizotaifishwa
 
Pengine wewe ni mtoto wa juzi na hujui historia ya shule ya Pugu.
Shule hii ilijengwa na wamissionari miaka mingi kabla ya uhuru.
Ilikuwa inaitwa St Francis Sec School, na ilikuwa ni kwa ajili ya haswa dhehebu la Kikatoliki.
Hata Mwalimu Nyerere alipofundisha hapo 1952, St Francis(Pugu) aliajiriwa na kanisa Katoliki.

Shule ilitaifishwa kuwa ya serikali baada ya uhuru ili kila mtoto wa kitanzania apate elimu bila kutazama dini yake.
Na kanisa lipo hapo toka miaka hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…