Kwanini Katiba Mpya ni muhimu sasa kuliko wakati wote!

sammosses

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2011
Posts
1,745
Reaction score
1,171
Mada yangu ya awali nilisema Katiba ya wananchi ndiyo moyo wa nchi unaosukuma mienendo/mwongozo wa sheria mbalimbali kwenye nchi yeyote Ile Duniani.

Umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi unashinikizwa na wakati uliopo na mwenendo wa serikali yetu katika utawala wake. Viashiri vya ukomavu wa utawala wa Kiimla umeshika Kasi na kutengeneza Demokrasia maarufu Tanzania inayoitwa Tanzania tuna Demokrasia yetu.

Demokrasia ya Tanzania imetengeneza mfumo mpya wa ubaguzi kinyume na matakwa ya Demokrasia halisi ya kidunia. Ndiyo maana watawala wameweka vigezo vya Demokrasia kwa misingi ya vyama vingi vya siasa,uchaguzi n.k.

Lakini Kuna swali muhimu la kujiuliza vigezo hivi vya Demokrasia ya Tanzania vinakidhi matakwa ya Demokrasia tuliyoisaini kuitekeleza kwa mujibu mikataba ya kidunia hususani utaoaji haki!

Je mfumo wa vyama vingi una tija kwa Taifa letu kwa kupata haki sawa,na chaguzi za viongozi wa nchi wanapatikana kwa haki na uwazi!

Maswali haya magumu kwa watawala ndiyo yenye kuleta ukinzani na anguko kwa serikali kung'ang'ania Katiba ya mwaka 1977 inayowapa fursa ya kunyang'anya haki za wananchi juu ya serikali waitakayo..

Hapo ndipo takwa la Katiba mpya ya wananchi linapouhishwa kwa nguvu kubwa kwa kuwa Katiba mpya inayokinzana na ya mwaka 1977 itazingatia yafuatayo;
  • Kufafanua haki na wajibu wa wananchi
  • Kuweka mipaka ya mamlaka ya viongozi
  • Kuongeza uwazi na uwajibikaji
  • Kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa maslahi ya wote
Muasisi wa Taifa la Tanzania Mwl Nyerere alionya kuhusu Katiba iliyoko,kwa kuona viashiria vya kumtengeneza Dikitekta ambaye atakuwa adui mkubwa wa wananchi,atakayehodhi mamlaka ya wananchi,kwa msingi wa maoni ya Mwl sasa yametimia.

Kwa mantiki hiyo juhudi kubwa inayofanyika ni kuwagawa wananchi kwenye makundi ya wanaotaka Katiba mpya na wanaotaka Katiba hii kwa mbinu za itikadi za vyama vyao.

Haya yanafanyika kwa nguvu kubwa sambamba na kukithiri kwa Ufisadi, ubadhirifu, au ukosefu wa uwajibikaji?

Matokeo ya mbinu hizo chafu ni Rais kuwa Mungu mtu na mwenye miliki na nchi yote bila kujali ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya muungano. Amehodhi mamlaka yote na zaidi amekuwa Katiba kwa kufanya hata yale yaliyokosa msingi wa kikatiba,mfano;
  • Usiri mkubwa wa mikataba serikali inayoingia na wahisani bila bunge kujua
  • kuzuia haki za vyama vya siasa kufanya siasa kwa utashi binafsi kama Kinga ya kujitanua kiutawala
  • Bunge kukosa uhalali wa kuwa Bunge la wananchi na kuwa chombo Cha uwakilishi wa serikali
  • Mgawanyo wa madaraka na mipaka ya kiutendaji inayosababisha wanasiasa na serikali yao kuingilia uhuru wa mahakama ambao ni Muhimili unaojitegemea.
Kimsingi yapo mambo mengi yanyaofanyika bila kuzingatia misingi ya utawala Bora.

Ukisoma Ibara ya 8 inataka nchi isimamiwe kwa maslahi ya wananchi wote. Kiongozi kuwa "Mungu mtu" na mwenye miliki ya nchi ni:
  • Kinyume na misingi ya utawala wa sheria
  • Hatari kwa demokrasia na haki za binadamu
Lakini haki hiyo inatekelezeka!

Moja ya msingi wa ibara hii ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni mamlaka ya wananchi kuziweka serikali madarakani na kupata Ustawi wake kama msingi mkuu wa serikali,lakini pia kuwajibika kwa serikali kwa wananchi,haya hayafanyiki.

Anayepaswa kuwekwa madarakani ndiye anayeunda timu yake iliyopewa mamlaka ya tume ili kujitanua ipasavyo madarakani. Hapa ndiyo unapoitishwa uchaguzi kwa kigezo Cha Demokrasia ya Kidunia kwa kupata maelekezo ya kusimamia uchaguzi kwa kubainisha nani anatakiwa na nani hatakiwi kuwa sehemu ya uchaguzi.

Bila kuathiri mbinu chafu za mtawala mahakama zinaingizwa mkenge kuzuia haki ya wasiotakiwa kugombea nafasi fulani kubwa kabisa na kupingwa mahakamani,lakini wakiweka kigezo Cha matokeo ya Urais kutohojiwa mahakamani,mfano mzuri kuzuiliwa kwa chama kikuu Cha siasa Tanzania kufanya siasa na kushiriki uchaguzi lakini mgombea anayedhaniwa kuwa na nguvu kuzuiliwa kushiriki kugombea nafasi hiyo.

Hivyo basi utaona kuwa dawa ya uchafu wa mfumo uliosimikwa kuzuilia haki za msingi za kikatiba zinatokana na Katiba isiyo na meno ni kufanya mabadiliko ya Katiba,toka Katiba ya viongozi kuelekea Katiba ya wananchi.

Mabadiliko ya Katiba yanaweza:
  • Kufafanua mamlaka na wajibu wa rais
  • Kuweka vikwazo vya kisheria
  • Kuhakikisha uwajibikaji na uwazi
Hali ya nchi si salama kama tunavyofikiri,ikiwa mchakato wa Katiba ya wananchi ulifikia hatua ya kupatikana kwa Rasimu ya tume ya Jaji Warioba na kuitishwa kwa bunge la Katiba kwa kufikia hatua ya kura za maoni,lakini ghafla mchakato ukazimwa kwa utashi wa mtawala,unafikiri nchi itakuwa salama!

Kama jambo kama hili lililotumia mabilioni ya fedha za wananchi hazionewi uchungu unafikiri mchakato wa Katiba mpya utaletwa tu bila shinikizo la wananchi!

Ni mambo mawili yanalazimika kufanyika
1. Kuendelea tulipoishia kwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba
2. Kuanzisha mchakato mpya kwa kuwa Kuna mambo mengi yameongezeka kwa vipindi viwili vya tawala zilizopita.

Tume ya Jaji Warioba imefanya kazi kubwa katika kuweka mbele mapendekezo ya kurekebisha mfumo wa uongozi nchini. Hata hivyo, kuna haja ya kuongeza mambo mengine ili kushughulikia changamoto za sasa, kama vile mmonyoko wa maadili na ombwe la uongozi.

Jaji Warioba mwenyewe aliapendekeza mabadiliko kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu, ambapo Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na serikali zao za ndani, huku serikali ya muungano ikishughulikia masuala ya ulinzi, usalama, na mambo ya nje.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo, muundo wa serikali tatu unapendekezwa ili kuleta uwiano na usawa kati ya pande zote za muungano. Lakini kinachofanyika ni mwendelezo na fikra za unyonyaji dhidi ya Watanganyika waliodhulumiwa nchi yao.

Muungano wetu umegeuzwa fumbo la Imani,ni sawa na kuchonga kinyago Kisha kikakutisha,wakati Jakaya Kikwete anamteua Jaji Warioba,kwenye hadidu za rejea alimuonya asijaribu kuuzungumzia Muungano,lakini namshukuru Jaji Warioba na Tume aliyoiongoza hawakuzingatia Hilo.

Unawezaje kufunika moto kwa mavi ya ng'ombe,kama si kuuchochea!

Muungano huu ni fumbo la Imani la watawala,hakuna uwazi zaidi ya mambo ya Muungano,lakini umeuwa utaifa wetu,kwa msingi huo Kuna haja ya Article of Union kuwekwa wazi ili tuweze kujua sababu ya Muungano ni zipi,zinatekelezeka!

Kimsingi Hali ilivyo inachochea sana kuutazama Muungano huu kwa jicho la mwewe,kama wote ni Watanzania kwanini uchochezi ufanyike kwenye vyama vya siasa kuhusu mambo yao ya ndani.

Mambo yanayoendelea kwenye kesi ya zuio la CHADEMA kimsingi yanachokonoa Siri iliyojificha ndani ya Muungano. Imagine Watanganyika wafungue kesi ya kuzuia serikali ya Muungano kutekeleza majukumu yake mpaka Tanganyika irudishiwe mamlaka yake kamili,kwa kuwa Muungano bila Tanganyika hakuna sababu za Muungano,maslahi ya Watanganyika yatasimamiwa na upande Gani!

Kwa hiyo utaona Kuna haja ya uwazi sana kwenye suala hili na kuliondoa kuwa fumbo la Imani.

Yapo mambo mengi yanazua maswali mfano Kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar, ni kweli kwamba Zanzibar ilifanya mabadiliko ya Katiba yake na kujitambua kama nchi yenye mamlaka kamili. Kama hivi ndivyo Iko wapi Katiba ya Tanganyika inayotoa mamlaka kamili kama wenzetu wa upande wa pili.

Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza, na Zanzibar ilikuwa nchi huru chini ya Sultani. Baada ya uhuru, waliamua kuungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964.

Hakuna mamlaka iliyoamuru kuiua Tanganyika. Ilikuwa mabadiliko ya kisiasa na kiutawala, ambapo Tanganyika ilichanganya utambulisho wake na Zanzibar kuunda nchi mpya.

Kwa msingi huo mabadiliko hayo ya kisiasa yamepataje uhalali wa kuiua nchi Moja na Moja na kuibakiza nchi nyingine kama si kiini macho Cha wanasiasa wenye Siri nzito nyuma ya pazia.

Wengi wanafikiri muungano umeleta maendeleo na umoja, wengine wanahisi Tanganyika ilitolewa sadaka kwa maslahi ya Zanzibar. Ukweli utabaki wazi Article of Union ndiyo jibu.

Muungano huu umeleta changamoto za kiutawala na kiuchumi. Watanganyika hawana sauti kamili katika uamuzi wa nchi.

Kwa hiyo utaona umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi ndiyo itakayotoa majibu sawia na kutoa usawa wa Tanganyika yenye madaraka kamili.

Itaondoa maslahi ya Tanganyika yanayo nyonywa na Muungano kwa kuifanya Tanganyika kuwa Tanzania bara kinyume kabisa na Katiba ya mwaka 1977.

Katiba ya wananchi Itakuwa fursa kubwa ya:
  • Kujadili mustakabali wa nchi
  • Kuelewa mahitaji ya pande zote mbili
  • Kuunda muundo mpya wa Muungano kwa matakwa ya wananchi si watawala.
Kwa Hali ilivyo hatuaminiani katika ya wananchi na watawala,kutokana na mamlaka ya wananchi kuhodhiwa na watawala,hivyo suala la Muungano pia haliwezi kutoa majibu ya kina ikiwa yatasimamiwa na tume ya Rais ambaye mapendekezo ya wananchi yanaweza kupunguza nguvu yake ya kimamlaka.

Hivyo kwenye suala hili inapaswa makubaliano yetu yaratibiwe na Umoja wa Mataifa ili kulinda hadhi ya Taifa Moja dhidi ya Taifa lingine.

Uwazi na ukweli vitakuwa muhimu ili kuepuka migogano na kuleta amani.

Uwazi unaotakiwa ni kujua malengo halisi ya Muungano,kufahamu masharti na mikataba na kupima mafanikio na changamoto kwa uhalisia.

Hii itapunguza dhana ya Watawala kuamini kuwa kuvunjika kwa Muungano ni dhambi kubwa,hofu hii inatokana na migogano ya kikundi,kukosekana utulivu na kupoteza maslahi binafsi

Kwa msingi huo utaona mabadiliko ya Muungano utakaoinusuru Tanzania na Tanganyika iliyopotezwa kwa utashi wa watu wachache utakuwa umepatiwa dawa na kuzika migogoro isiyo na tija.

Ni jukumu la Kila mwananchi kusimamia nafasi yake kama wajibu wake kwa nchi na kukataa kugawanywa kwa misingi ya kudanganywa kuwa Katiba haileti ugali mezani,wakati Katiba hii ndiyo imewapa kushiba na kuvimbiwa.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Tanganyika.
Katiba ni sasa na muda ndiyo huu.
 
Ni jukumu la Kila mwananchi kusimamia nafasi yake kama wajibu wake kwa nchi na kukataa kugawanywa kwa misingi ya kudanganywa kuwa Katiba haileti ugali mezani,wakati Katiba hii ndiyo imewapa kushiba na kuvimbiwa
 
Mimi hua nasikitika sana nikiona mtu anaitwa msomi anacomment et katiba haileti ugali,kimsingi mtu kama huyo anamchango mdogo sana kwa taifa.
 
Mimi hapa nilipo nina kadi ya ccm! Ila kutoka moyoni mwangu ninatamani kuona hiki chama kinakufa hata kesho ili nchi nayo ipate maono mapya! Haya mambo ya kukubali kutawaliwa miaka nenda na ccm, ni hatari kwa mustakabari wa nchi.

Leo hii ccm siyo chama tena cha siasa! Badala yake imegeuka kuwa genge la wahuni wachache wanaojilimbikizia mali na, ushawishi kupitia kodi na raslimali zetu.
 
Tuna wajibu mkubwa kwenye jambo hili,Robert Kennedy Jr aliwahi kuwauliza Wamarekani wamewahi kuifanyia Nini America,badala ya kufikiri America imewafanyia Nini!

Sisi jukumu letu kubwa ni kudai Katiba mpya itakayofunua mifumo kandamizi ya kifamilia kwenye serikali ya umma. Hilo iwe ndiyo kazi ya kwanza,ukilala Katiba mpya,ukiamka Katiba mpya
 
Hoja maridhawa, ni kuelekea hatua ya utekelezaji tu sasa.
 
Tuna wajibu mkubwa kwenye jambo hili,Robert Kennedy Jr aliwahi kuwauliza Wamarekani wamewahi kuifanyia Nini America,badala ya kufikiri America imewafanyia Nini!

Sisi jukumu letu kubwa ni kudai Katiba mpya itakayofunua mifumo kandamizi ya kifamilia kwenye serikali ya umma. Hilo iwe ndiyo kazi ya kwanza,ukilala Katiba mpya,ukiamka Katiba mpya
Mimi ninahisi huu muungano una maagano machafu nyuma yake, ndio maana watu wakipata uongozi wanapewa hiyo Siri, na kuaanza kuulinda muungano bila sababu zenye mashiko. Maana jambo kama halipo kishirikina sababu za msingi hutolew kuhusu uwepo wake. Lakini kwa jinsi ilivyo, ni ngumu kutetea muungano huu kwa hoja.
 
Waweke Article of Union ituonyeshe uhalisia. Lissu alisema kwenye bunge la Katiba kuwa hati ya Muungano imefojiwa,lakini mpk kesho hakuna uthibitisho kama kweli haijafojiwa.

Wanaotaka Muungano ni watawala,waliwahi kutaka kujua Sisi wenye nchi na mwenye mamlaka za kuziweka serikali madarakani tunataka huo Muungano! Na tunataka ni Muungano upi,huu wa kuuwa Taifa Moja na kuimarisha Taifa lingine!
 
Mimi hua nasikitika sana nikiona mtu anaitwa msomi anacomment et katiba haileti ugali,kimsingi mtu kama huyo anamchango mdogo sana kwa taifa.
Ukiona mtu anakwambia Katiba haileti ugali tambua kwamba HATAKI uijadili Katiba ITAKAYOMPUNGUZIA huo ugali. Watu wa aina hiyo ni wanufaika wa Katiba mbovu inayowapa ugali wachache huku wengi wakigeuzwa kuwa "watumwa" wa wachache.
 
Nchi hii imeshikiliwa na walafi wachache,imagine mchakato wa Katiba kupitia Tume ya Warioba ilitumia zaidi ya Bilioni 300,lakini mahafidhina wakaua ndiyo za Watanzania za kupata Katiba mpya kwa ubinafsi wa kupoteza madaraka.

Ilani ya CCM imesema ndani ya siku 100 mchakato utaanza,Leo tuna siku ngapi,vurugu za MO29 chanzo chake ni madai ya katiba,serikali inataka wafe wangapi ili Katiba itokanayo na damu ipatikane!
 
Mimi huwa ninahoji kwanini mtu kutoka zanzibar anaweza kuja tanganyika na kushika wadhifa wa juu hadi kuwa rais/makamu wa raisi, wakati huo huo kwa mazingira hayo hayo ya kimuungano mtu kutoka tanganyika hawezi kupewa hadhi hiyo zanzibar? Kwanini upande mmoja wa muungano ndo uvune matunda ya muungano kwa kunyonya upande mwingine? Watanganyika tuamke tumelala vya kutosha...
Katiba mpya ni sasa
 
Mimi hapa nilipo nina kadi ya ccm! Ila kutoka moyoni mwangu ninatamani kuona hiki chama kinakufa hata kesho ili nchi nayo ipate maono mapya! Haya mambo ya kukubali kutawaliwa miaka nenda na ccm, ni hatari kwa mustakabari wa nchi.

Leo hii ccm siyo chama tena cha siasa! Badala yake imegeuka kuwa genge la wahuni wachache wanaojilimbikizia mali na, ushawishi kupitia kodi na raslimali zetu.
Wewe tunafanana limekua ngenge la watu flani kupigania maslahi yao sio chama
 
Mada yangu ya awali nilisema Katiba ya wananchi ndiyo moyo wa nchi unaosukuma mienendo/mwongozo wa sheria mbalimbali kwenye nchi yeyote Ile Duniani.

Umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi unashinikizwa na wakati uliopo na mwenendo wa serikali yetu katika utawala wake. Viashiri vya ukomavu wa utawala wa Kiimla umeshika Kasi na kutengeneza Demokrasia maarufu Tanzania inayoitwa Tanzania tuna Demokrasia yetu.

Demokrasia ya Tanzania imetengeneza mfumo mpya wa ubaguzi kinyume na matakwa ya Demokrasia halisi ya kidunia. Ndiyo maana watawala wameweka vigezo vya Demokrasia kwa misingi ya vyama vingi vya siasa,uchaguzi n.k.

Lakini Kuna swali muhimu la kujiuliza vigezo hivi vya Demokrasia ya Tanzania vinakidhi matakwa ya Demokrasia tuliyoisaini kuitekeleza kwa mujibu mikataba ya kidunia hususani utaoaji haki!

Je mfumo wa vyama vingi una tija kwa Taifa letu kwa kupata haki sawa,na chaguzi za viongozi wa nchi wanapatikana kwa haki na uwazi!

Maswali haya magumu kwa watawala ndiyo yenye kuleta ukinzani na anguko kwa serikali kung'ang'ania Katiba ya mwaka 1977 inayowapa fursa ya kunyang'anya haki za wananchi juu ya serikali waitakayo..

Hapo ndipo takwa la Katiba mpya ya wananchi linapouhishwa kwa nguvu kubwa kwa kuwa Katiba mpya inayokinzana na ya mwaka 1977 itazingatia yafuatayo;
  • Kufafanua haki na wajibu wa wananchi
  • Kuweka mipaka ya mamlaka ya viongozi
  • Kuongeza uwazi na uwajibikaji
  • Kuhakikisha rasilimali zinatumika kwa maslahi ya wote
Muasisi wa Taifa la Tanzania Mwl Nyerere alionya kuhusu Katiba iliyoko,kwa kuona viashiria vya kumtengeneza Dikitekta ambaye atakuwa adui mkubwa wa wananchi,atakayehodhi mamlaka ya wananchi,kwa msingi wa maoni ya Mwl sasa yametimia.

Kwa mantiki hiyo juhudi kubwa inayofanyika ni kuwagawa wananchi kwenye makundi ya wanaotaka Katiba mpya na wanaotaka Katiba hii kwa mbinu za itikadi za vyama vyao.

Haya yanafanyika kwa nguvu kubwa sambamba na kukithiri kwa Ufisadi, ubadhirifu, au ukosefu wa uwajibikaji?

Matokeo ya mbinu hizo chafu ni Rais kuwa Mungu mtu na mwenye miliki na nchi yote bila kujali ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya muungano. Amehodhi mamlaka yote na zaidi amekuwa Katiba kwa kufanya hata yale yaliyokosa msingi wa kikatiba,mfano;
  • Usiri mkubwa wa mikataba serikali inayoingia na wahisani bila bunge kujua
  • kuzuia haki za vyama vya siasa kufanya siasa kwa utashi binafsi kama Kinga ya kujitanua kiutawala
  • Bunge kukosa uhalali wa kuwa Bunge la wananchi na kuwa chombo Cha uwakilishi wa serikali
  • Mgawanyo wa madaraka na mipaka ya kiutendaji inayosababisha wanasiasa na serikali yao kuingilia uhuru wa mahakama ambao ni Muhimili unaojitegemea.
Kimsingi yapo mambo mengi yanyaofanyika bila kuzingatia misingi ya utawala Bora.

Ukisoma Ibara ya 8 inataka nchi isimamiwe kwa maslahi ya wananchi wote. Kiongozi kuwa "Mungu mtu" na mwenye miliki ya nchi ni:
  • Kinyume na misingi ya utawala wa sheria
  • Hatari kwa demokrasia na haki za binadamu
Lakini haki hiyo inatekelezeka!

Moja ya msingi wa ibara hii ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ni mamlaka ya wananchi kuziweka serikali madarakani na kupata Ustawi wake kama msingi mkuu wa serikali,lakini pia kuwajibika kwa serikali kwa wananchi,haya hayafanyiki.

Anayepaswa kuwekwa madarakani ndiye anayeunda timu yake iliyopewa mamlaka ya tume ili kujitanua ipasavyo madarakani. Hapa ndiyo unapoitishwa uchaguzi kwa kigezo Cha Demokrasia ya Kidunia kwa kupata maelekezo ya kusimamia uchaguzi kwa kubainisha nani anatakiwa na nani hatakiwi kuwa sehemu ya uchaguzi.

Bila kuathiri mbinu chafu za mtawala mahakama zinaingizwa mkenge kuzuia haki ya wasiotakiwa kugombea nafasi fulani kubwa kabisa na kupingwa mahakamani,lakini wakiweka kigezo Cha matokeo ya Urais kutohojiwa mahakamani,mfano mzuri kuzuiliwa kwa chama kikuu Cha siasa Tanzania kufanya siasa na kushiriki uchaguzi lakini mgombea anayedhaniwa kuwa na nguvu kuzuiliwa kushiriki kugombea nafasi hiyo.

Hivyo basi utaona kuwa dawa ya uchafu wa mfumo uliosimikwa kuzuilia haki za msingi za kikatiba zinatokana na Katiba isiyo na meno ni kufanya mabadiliko ya Katiba,toka Katiba ya viongozi kuelekea Katiba ya wananchi.

Mabadiliko ya Katiba yanaweza:
  • Kufafanua mamlaka na wajibu wa rais
  • Kuweka vikwazo vya kisheria
  • Kuhakikisha uwajibikaji na uwazi
Hali ya nchi si salama kama tunavyofikiri,ikiwa mchakato wa Katiba ya wananchi ulifikia hatua ya kupatikana kwa Rasimu ya tume ya Jaji Warioba na kuitishwa kwa bunge la Katiba kwa kufikia hatua ya kura za maoni,lakini ghafla mchakato ukazimwa kwa utashi wa mtawala,unafikiri nchi itakuwa salama!

Kama jambo kama hili lililotumia mabilioni ya fedha za wananchi hazionewi uchungu unafikiri mchakato wa Katiba mpya utaletwa tu bila shinikizo la wananchi!

Ni mambo mawili yanalazimika kufanyika
1. Kuendelea tulipoishia kwa Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba
2. Kuanzisha mchakato mpya kwa kuwa Kuna mambo mengi yameongezeka kwa vipindi viwili vya tawala zilizopita.

Tume ya Jaji Warioba imefanya kazi kubwa katika kuweka mbele mapendekezo ya kurekebisha mfumo wa uongozi nchini. Hata hivyo, kuna haja ya kuongeza mambo mengine ili kushughulikia changamoto za sasa, kama vile mmonyoko wa maadili na ombwe la uongozi.

Jaji Warioba mwenyewe aliapendekeza mabadiliko kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa serikali tatu, ambapo Tanganyika na Zanzibar zitakuwa na serikali zao za ndani, huku serikali ya muungano ikishughulikia masuala ya ulinzi, usalama, na mambo ya nje.

Kwa mujibu wa rasimu hiyo, muundo wa serikali tatu unapendekezwa ili kuleta uwiano na usawa kati ya pande zote za muungano. Lakini kinachofanyika ni mwendelezo na fikra za unyonyaji dhidi ya Watanganyika waliodhulumiwa nchi yao.

Muungano wetu umegeuzwa fumbo la Imani,ni sawa na kuchonga kinyago Kisha kikakutisha,wakati Jakaya Kikwete anamteua Jaji Warioba,kwenye hadidu za rejea alimuonya asijaribu kuuzungumzia Muungano,lakini namshukuru Jaji Warioba na Tume aliyoiongoza hawakuzingatia Hilo.

Unawezaje kufunika moto kwa mavi ya ng'ombe,kama si kuuchochea!

Muungano huu ni fumbo la Imani la watawala,hakuna uwazi zaidi ya mambo ya Muungano,lakini umeuwa utaifa wetu,kwa msingi huo Kuna haja ya Article of Union kuwekwa wazi ili tuweze kujua sababu ya Muungano ni zipi,zinatekelezeka!

Kimsingi Hali ilivyo inachochea sana kuutazama Muungano huu kwa jicho la mwewe,kama wote ni Watanzania kwanini uchochezi ufanyike kwenye vyama vya siasa kuhusu mambo yao ya ndani.

Mambo yanayoendelea kwenye kesi ya zuio la CHADEMA kimsingi yanachokonoa Siri iliyojificha ndani ya Muungano. Imagine Watanganyika wafungue kesi ya kuzuia serikali ya Muungano kutekeleza majukumu yake mpaka Tanganyika irudishiwe mamlaka yake kamili,kwa kuwa Muungano bila Tanganyika hakuna sababu za Muungano,maslahi ya Watanganyika yatasimamiwa na upande Gani!

Kwa hiyo utaona Kuna haja ya uwazi sana kwenye suala hili na kuliondoa kuwa fumbo la Imani.

Yapo mambo mengi yanazua maswali mfano Kuhusu mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar, ni kweli kwamba Zanzibar ilifanya mabadiliko ya Katiba yake na kujitambua kama nchi yenye mamlaka kamili. Kama hivi ndivyo Iko wapi Katiba ya Tanganyika inayotoa mamlaka kamili kama wenzetu wa upande wa pili.

Tanganyika ilikuwa chini ya utawala wa Waingereza, na Zanzibar ilikuwa nchi huru chini ya Sultani. Baada ya uhuru, waliamua kuungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964.

Hakuna mamlaka iliyoamuru kuiua Tanganyika. Ilikuwa mabadiliko ya kisiasa na kiutawala, ambapo Tanganyika ilichanganya utambulisho wake na Zanzibar kuunda nchi mpya.

Kwa msingi huo mabadiliko hayo ya kisiasa yamepataje uhalali wa kuiua nchi Moja na Moja na kuibakiza nchi nyingine kama si kiini macho Cha wanasiasa wenye Siri nzito nyuma ya pazia.

Wengi wanafikiri muungano umeleta maendeleo na umoja, wengine wanahisi Tanganyika ilitolewa sadaka kwa maslahi ya Zanzibar. Ukweli utabaki wazi Article of Union ndiyo jibu.

Muungano huu umeleta changamoto za kiutawala na kiuchumi. Watanganyika hawana sauti kamili katika uamuzi wa nchi.

Kwa hiyo utaona umuhimu wa Katiba mpya ya wananchi ndiyo itakayotoa majibu sawia na kutoa usawa wa Tanganyika yenye madaraka kamili.

Itaondoa maslahi ya Tanganyika yanayo nyonywa na Muungano kwa kuifanya Tanganyika kuwa Tanzania bara kinyume kabisa na Katiba ya mwaka 1977.

Katiba ya wananchi Itakuwa fursa kubwa ya:
  • Kujadili mustakabali wa nchi
  • Kuelewa mahitaji ya pande zote mbili
  • Kuunda muundo mpya wa Muungano kwa matakwa ya wananchi si watawala.
Kwa Hali ilivyo hatuaminiani katika ya wananchi na watawala,kutokana na mamlaka ya wananchi kuhodhiwa na watawala,hivyo suala la Muungano pia haliwezi kutoa majibu ya kina ikiwa yatasimamiwa na tume ya Rais ambaye mapendekezo ya wananchi yanaweza kupunguza nguvu yake ya kimamlaka.

Hivyo kwenye suala hili inapaswa makubaliano yetu yaratibiwe na Umoja wa Mataifa ili kulinda hadhi ya Taifa Moja dhidi ya Taifa lingine.

Uwazi na ukweli vitakuwa muhimu ili kuepuka migogano na kuleta amani.

Uwazi unaotakiwa ni kujua malengo halisi ya Muungano,kufahamu masharti na mikataba na kupima mafanikio na changamoto kwa uhalisia.

Hii itapunguza dhana ya Watawala kuamini kuwa kuvunjika kwa Muungano ni dhambi kubwa,hofu hii inatokana na migogano ya kikundi,kukosekana utulivu na kupoteza maslahi binafsi

Kwa msingi huo utaona mabadiliko ya Muungano utakaoinusuru Tanzania na Tanganyika iliyopotezwa kwa utashi wa watu wachache utakuwa umepatiwa dawa na kuzika migogoro isiyo na tija.

Ni jukumu la Kila mwananchi kusimamia nafasi yake kama wajibu wake kwa nchi na kukataa kugawanywa kwa misingi ya kudanganywa kuwa Katiba haileti ugali mezani,wakati Katiba hii ndiyo imewapa kushiba na kuvimbiwa.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu ibariki Tanganyika.
Katiba ni sasa na muda ndiyo huu.
Gentleman acha porojo,
katiba mpya si muhimu Tanzania hata kidogo,
kwasababu iliyopo bado ni nzuri sana, inajitosheleza na kukidhi zaidi ya 95% ya mahitaji ya waTanzania wote.

hata hivyo,
katika ilani ya chama cha mapinduzi CCM ya 2025-2030 jambo hilo dogo ni miongoni mwa mengi yaliyoahidiwa kutekelezwa katika awamu hii ya uongozi wa kipenzi cha waTanzania Dr.Samia Suluhu Hassan.

Niliishauri CCM, na nitaendelea kuishauri serikali yangi sikivu ya CCM, kuahirisha jambo hilo na kulifanyia kazi angalau kuanzia 2040, kwakua yapo mambo mengi muhimu zaidi yanafaa kufanyika kwa kipindi hiki kwaajili ya waTanzania kuliko jambo hilo dogo tu tena la kisiasa.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom