Kwanini katika chumba cha upasuaji kote Duniani wanazaa au kutumia nguo za kijani

Rangi ya kijani ni opposite ya red....yani ni rangi yenye wavelength ndogo kwahio ni haivuti attention sana..
Hii inawawezesha ma dr wawe focused na mgonjwa na sio rangi ya nguo..

Mfano wangevaa nguo zenye rangi yenye wavelength kibwa kama red au yellow wangekuwa wanapoteza focus na kuanza kushangaa rangi za nguo..


Hii pia ndio sababu magari ya wanafunzi (schoolbus) zina rangi ya njano ili zionekane kwa uraisi....pia taa za brake ni nyekundu
 
@Mods nisaidieni kuedit hapo juu, sio kuzaa ni kuvaa
 
Ni sare tu wameamua kama majeshi walivyoamua kuwa na sare zao,
 
Nguo ya kijani kiimani inamaanisha uhai...ndio maana wanavaa kupunguza mkosi wa kifo!....kuna vitu duniani ni deep kuliko neno deep lenyewe....google "credo vusamazulu mutwa" aliwahi gusia hili katika kitabu chake cha "indaba my children"
Sio sababu
 
Ma Dr. na wajuzi wa mambo, hili swali limekua likiniumiza sana kichwa, majibu niliyopata Google hajakunifanya niishie hapo...

Kwanini rangi ya kijani?

Mkuu Going Concern, salama kwako.

Kwa taarifa yako rangi ya kijani kwenye vyumba vya upasuaji (operating theatres) siyo kwa ajili ya mavazi tuu yaani nguo za madakari,mashuka,vitambaa na hata mavazi ya watu wengine wote wanaohusika katika vyumba hivyo, bali pia ni kwa ajili ya mazingira ya vyumba hivyo kwani ni matakwa ya fani ya utabibu kuwa na rangi ya kijani kwenye vyumba hivyo.

Nikisema mazingira nina maanisha kuwa hata vifaa vya ujenzi vinavyotumika katika ujenzi wa vyumba huchaguliwa kwa makusudi kuwa vya rangi ya kijani. Mfano wall na floor tiles huwa ni za rangi ya kijani pamoja na samani yaani furniture. Kwenye taaluma ya utabibu rangi ya kijani huashiria uhai (kwa kuihusisha na viumbe hai hasa mimea), rangi ya kijani hupunguza stress kwa madakari na isitoshe damu inapodondokea kwenye shuka la kijani hutokea doa jeusi Na hivyo kumuepusha mgonjwa au daktari kuwa na uoga (nadhani unaweza kupata picha ya mazingira ya maduka ya kuuzia nyama au machinjoni ya nyama ambapo watumishi huvaa nguo nyeupe,iwe makoti na mabuti).Vilevile kwa ajili ya colour coding, muuguzi yeyote au mwana taaluma wa afya akiona kifaa au kitu cha rangi ya kijani mara moja hugundua kuwa kinahusika na chumba cha upasuaji.

Kuna Rangi nyingine pia, inatumika kwenye vyumba vya upasuaji,nayo ni rangi ya blue,rangi hii ni "sky blue" to be precisely. Rangi hiyo ni kama hii ya jukwaa hili letu la Jamii Forum. Kwa taarifa tuu,hii ndiyo rangi inayongoza kwa muonekano na binadamu kwenye hii dunia yetu, kwani hata anga ni la rangi hii. Katika fani ya utabibu hasa wa magonjwa ya akili rangi hii hutumika sana. Hii inaitwa neutral colour.............................Ukifuatilia maswala ya rangi,utagundua kuwa kila rangi huwa ina maana yake hasa kwenye itikadi, siasa, uchumi, michezo, utawala,majeshi nk.


kwa ruhusa yako naomba niishie hapa.

Wasalamu,
Mwenzetu
 
Wanazaa nini tena? [emoji41][emoji41][emoji41] Uwa hatuzai wew
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…