MFAHAMU KENNETH KAUNDA, BABA WA TAIFA LA ZAMBIA PIA NDIYE MUASISI WA 'KAUNDA SUTI' VAZI AMBALO 80% YA WALINZI NA VIONGOZI WA Tz WANALIVAA WAKIWA KWENYE MAJUKUMU YAO.
Jana Juni 18, 2021 serikali ya Zambia iliripoti kuwa Rais wa Kwanza wa Taifa hilo, Mzee Kenneth Kaunda ambaye kwao wanamuita Baba wa Taifa ameaga Dunia.
Mzee Kaunda ndiye mzee pekee yake kati ya Wazee wa Mwanzo wapigania Uhuru barani Afrika aliyekuwa bado yupo hai.
Mzee Kaunda ana historia ndefu na ya kuvutia, leo nitajaribu kukupa historia yake fupi huyu mwamba wa Zambia na Afrika aliyefariki akiwa na miaka 97.
Wapo wanaosema Mzee Kaunda asili yake ni Malawi na alitoka huko ila alienda kusaidia Zambia kupata Uhuru na akabaki huko.
Hoja ya utata wa mahusiano ya Mzee Kaunda na Malawi na kwa nini Kaunda alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Rais wa Kwanza wa Malawi Mzee Banda?.
Jibu ni kwamba Baba yake Kenneth Kaunda alikuwa ni mzaliwa wa Malawi, Baba yake Kenneth KAUNDA, Mzee David Kaunda na Mama yake Kenneth KAUNDA walikuwa ni Walimu.
Walichukuliwa kwenda kufundisha Nothern Rhodesia yaani kwasasa ndio Zambia kutoka Nyasaland yaani Malawi kwasasa.
Wakiwa huko ndipo walibahatika kumzaa Kenneth KAUNDA Kama sehemu ya watoto wao nane. Hivyo Kaunda ni Mzambia kwa kuzaliwa lakini akiwa na asili ya Malawi.
Najua hapo tumeelewana, Mama yake Mzee Kaunda alikuwa ni mwanamke wa Kwanza Afrika kufundisha katika shule za kikoloni.
Turudi kwenye mada, Ukisoma maandiko mbalimbali ya Zambia Hayati Kaunda hajaandikwa sana. Hivyo ninaweza kusema ni mtu ambaye pamoja na umaarufu wake mkubwa lakini hajawekwa sana kwenye kumbukumbu za kwenye maandishi.
Kenneth Kaunda alizaliwa 24/4/1924 katika Kijiji Cha Lubwa ambacho kipo karibu na mji wa Chinsali Kaskazini mwa Zambia.
Kaunda alisoma shule ya msingi katika shule waliyokuwa wakifundisha wazazi wake. Alihitimu masomo ya sekondari mwaka 1940.
Kama ilivyo kwa Waafrika wengine ambao walau walikuwa wamepata elimu ya kati, Kaunda naye alienda kuwa Mwalimu. Aliwahi kufundisha Zambia na Tanganyika/Tanzania katika ya miaka ya 1940.
Mwaka 1949 Kaunda alirejea Zambia na akawa Mkalimani na mshauri wa Sir Stewart Gere-Browne a leberal white Settler ambaye pia alikuwa Mbunge. Huko Kaunda alijifunza vitu vingi ikiwepo siasa.
Mwaka 1950 Kaunda alijiunga na chama Cha ANC's na baadaye akawa katibu mkuu Mtendaji. Nafasi hii ilimuongezea exposure na akawa maarufu sana.
Hata 1959 ANC ilipoanza malengo ya kudai Uhuru Kaunda ndiye alipewa majukumu makubwa ya kutengeneza programu.
Baadaye alikuja kuwa kiongozi mkuu wa taasisi hiyo na kuanza kufoji baadhi ya nyalaka za kizungu katika makoloni ya Uingereza hasa Zambia, Malawi na Zimbabwe.
Alijitahidi kuwashawishi wananchi kupigania Uhuru lakini wengi wakawa waoga. Akaanzisha kitu kilichoitwa "Positive nonviolently action" ambacho kilihusika na raia kutokutii maagizo na sera za ukoloni.
Mzee Kaunda alikamatwa na wenzake na kwenda jela. Hii iliwapa ushujaa na kipindi hicho afrika nzima ilikuwa kwenye mapambano ya kudai Uhuru.
January 1960 aliruhusiwa kutoka magereza na akachaguliwa kuwa Rais wa UNIP( UNITED NATIONAL INDEPENDENCE PARTY) ambacho kilianzishwa mwaka 1959 na Mainza Chona.
Mwaka 1960 mwishoni Uingereza ilimualika Kaunda London kueleza kwa nini anataka Uhuru?
Uchaguzi ulipofanyika 1962 chama chake kilishinda. Na mwaka 1964 ikapata Uhuru kamili Kaunda akawa Rais.
Baada ya Zambia kupata Uhuru vilizuka Vita vya ukabila, hasa ukizingatia Kaunda alikuwa na asili ya Malawi.
Na uchaguzi ulipofanyika mwaka 1968 Kaunda alishinda. Alipoona mbele haoni kuendelea kuwa Rais hasa ukizingatia Vita ya ukabila na Utaifa, mwaka 1972 alifutilia mbali mfumo wa vyama vingi na mwaka 1973 akatengeneza katiba.
Mwaka 1990 Kaunda aliruhusu Mfumo wa vyama vingi na mwaka 1991 Kaunda na Chama chake Cha UNIP walishindwa vibaya kwenye uchaguzi na Chama Cha MMD kilishinda kwa ushindi wa kishindo.
NB: Huyu Mzee alikuwa mtu wa Suti tu, Ndio hapo likatokea vazi la KAUNDA SUTI.