Kwanini Kenya wamefuta Mitihani ya Taifa kwenye Mtaala mpya?

Kama unataka kujua mengi zaidi kuhusu mtaala wenyewe fanya risechi yako mwenyewe. Sio jukumu langu kukuelimisha, acha uvivu.
Hahahaha, Sasa kwanini mnaweka Mambo hapa JF Kama hamna uwezo ya kuyafafanua?, Lengo la JF ni mijadala yenye kuelimishana na kubadilishana uzoefu wa Mambo mbalimbali.
 
Wapi hiyo ilishawahi kutumika duniani ili tujaribu kupima ufanisi wake.
 
Hahahaha, Sasa kwanini mnaweka Mambo hapa JF Kama hamna uwezo ya kuyafafanua?, Lengo la JF ni mijadala yenye kuelimishana na kubadilishana uzoefu wa Mambo mbalimbali.
Nadhani uzi huu ulikuwa kwenye jukwaa lingine na aliyeibuka nao ni mtanzania mwenzenu. Anyway, tashwishi halipo kwenye uwezo wangu wa kufafanua. Bali ni kwamba sina huo muda wa kudadavua kila jambo, kwa yeyote yule anayetaka kutafuniwa. Sitalipwa kwa huduma hiyo, ambayo itapoteza muda wangu bure. Kwa Kikikuyu huwa wanasema, ní gútee! Kumaanisha ni hasara tupu! Au ukipenda, ní úrimú! 😄
 
Wapi hiyo ilishawahi kutumika duniani ili tujaribu kupima ufanisi wake.
Mfumo wa 8-4-4, ambao umekuwa ukitumiwa kwa miaka mingi nchini Kenya ulibuniwa na wakenya wenyewe. Wala hautumiki sehemu yeyote ile nyingine duniani. Licha ya mfumo huo wa zamani kuwa na mapungufu yake bado umekuwa wa faida kubwa sana kielimu nchini Kenya na una afueni zaidi ya mifumo yote inayotumiwa kwenye nchi zote zingine ukanda huu wa A.M na ya Kati.

Kwa ufupi ni kwamba tuna uwezo wa kubuni na kujipangia wenyewe. Sio lazima tuige kwenye kila jambo, elimu ni suala nyeti mno.
 
Akimtaja unitag mkuu!!Mi sijaona hata Mimi ni graduate LAKINI nazalisha ajira za house girl tu na kuuza duka out of the professional yangu!!!
Hawezi kumtaja wala kujua chochote na hajui kwenye ajira hawatizami matokeo yako but education, skills, knowledge and sometimes experiences.

Mambo ya nilikuwa naongoza skuli au kuwa best scholar in country HAKUNA kitu hicho duniani.
 
Ni throw. aya tigana nao . yaani kumaanisha CBC iko sawa
 
Huu ambao hamuwezi kuingia vyuo nchi za magharibi bila kufanya a levels equivalent!
 
Hili ndio tatizo lenu wakenya, kujisifia hovyo bila kuwa na vigezo vyovyote;
1)Kenya imeendelea kuwa na tatizo la unemployment rate kubwa kuliko nchi zote za ukanda huu
2)Kenya imeendelea kuwa na very poor civil engineers katika ukanda huu na Africa kwa ujumla, majumba yanayoporomoka Kenya kwa mwaka ni sawa au kuzidi Nyumba zote zinazoporomoka Africa Nzima
3)Kenya imeshindwa kupambana na tatizo la ukame miaka yote tangu 1963
4)Elimu ya Kenya imeshindwa kabisa kupambana na ukabila
5)Tatizo la maji ni sugu Kenya
6)Rushwa imekita mizizi Kenya

Elimu nzuri ni Ile inayoiwezesha jamii husika kutatua matatizo yake, sio kukimbilia nchi za nje kufanya kazi ili kutuma pesa nyumbani, huo ubora wa Elimu ya Kenya unaonekana wapi?
 
Acha kupoteza muda wako ukijaza pumba zako kwenye servers. CBC haijaanza jana na kwa muda wote huo wa uwepo wake hakuna uzi wowote umeanzishwa humu na wakenya. Nyinyi wenyewe ndio mmeibuka na taarifa zenyewe humu na nyinyi wenyewe tu ndio mnaisifia. Huku mkiponda vyenu, yaani mnajitekenya na kucheka wenyewe kama machizi.
 
Mkuu hoja iko chini sana.

Unasema mtoto kwa kuaplai kwenye maisha???

Are you serious??

Mwalimu atamkuta wapi huyo mtoto ili ampime kama anaweza kuaplai noleji aliyoipata shuleni??
 
Kuna kitu kinaitwa Triangle [emoji832]hii ilitokana na uchache wa Shule kipindi hicho kwa hiyo ili kuchuja wanafunzi na kupata wachache besties ilibidi utumike mfumo huo ila kwasasa kutokana na Elimu kutanuka hauna haja tena pongezi kwa Wakenya kwa kuliona hilo
 
Mkuu nafurahi kuona kwamba kuna watu km nyie tunawaza pamoja
 
🤣🤣🤣

Ebu soma huu uzi wa Mtanzania mwenzako Bwana Joto. Labda utaelewa wenzako wanachomaanisha wakisema elimu ya Kenya ina hadhi kuliko ya Bongo.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…