Kwanini kesi za kazi zinachukua muda mrefu kumalizwa?

Kwanini kesi za kazi zinachukua muda mrefu kumalizwa?

David lusinde

Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
7
Reaction score
0
Nina kesi tangu 2008, mpaka sasa bado inainaendelea.

Tumeshinda kesi hiyo ktk ngazi ya usuluhishi, uamuzi na tukafika mahakamani kwa ajili ya ukazaji wa hukumu, hukumu iliakazwa na ikaamuliwa yule mwajiri alipe.

Yyule mwajiri hakulitekeleza agizo la mahakama kama alivyoamuriwa, ikafuata kuanza kukamata mali zake ili ziuzwe ili tulipwe, zilikamtwa gari mbili, yule mwajiri akaenda mahakamani kuweka pingamizi kwamba pesa anayodaiwa ni kidogo lakini hizo anazoamuliwa na mahakama ni nyingi.

Mahakama ikamridhia ktk hilo na ndio hatua tuliyopo. Mbona naona tunapotezewa muda bure ikiwa hukumu za nyuma zinaonyesha mambo yale yale sasa iweje mahakama imridhie kutupotezea muda ikiwa kila kitu kiko wazi?

Kwanini basi kesi ya kazi ifanane na kesi ya mauaji au ndio mambo ya rushwa?
 
mkuu lusinde sijakuelewa,unaposema ulishinda kwenye mediation,ulishinda kvp? maana kwenye mediation hamna ruling, labda arbitration.

hiyo kesi yako iliamuli upande mmoja? halafu kama ilitolewa order kuwa mali zikamtwe na akakabithiwa hiyo kazi court broker, hiyo court juction iliwekwa mahakama gani? ni superior court au ni ni high court hiyo hiyo iliyotoa maamuzi ya awali?

maana mpaka kufijia kukamata mali ina maana decree debtor/ respondent alikataa kutekeleza maamuzi ya cma,maana arbitrator anagrant 14 day za utekelezaji na miezi 3 yakuomba revision incase pande zote mbili zilihudhuria shauri,lakini kama ni exp arbtrn rufani anatakiwa akate cma kutengua uamuzi wa upande mmoja, zaidi ya happ ni kukazia rulibg high court nao wanamtumia wito saipofika ndio hiyo order inatolewa ya kakamata mali, na utekelezaji wake lazima ufanyike,sasa yeye kwenye afidavity ameeleza nini mpaka mahakama imezuia kuuza mali?

maana lazima aanze kueleza ni kwa nini hajugushuria ktk shauri na ni kwa nini hakutekeleza maamuzi
 
David Lusinde kwa ushauri huu labda kutambua na kung'amua misingi mikuu inayosimamia KESI zinazohusu mambo ya KAZI.
Kwa utaratibu ulivyo ni hivi...

1. Kwenye Usuluhishi(mediation) kinachofanyika pale maongezi ya kawaida kati ya mwajiri na mfanyakazi mbele ya Afisa Msuluhishi(mediator) ambapo muhafaka wake ni pande mbili kuridhia kile mlichokubaliana kwa maana kwamba huwa hakuna kushindwa bali nyote mnakua mmeshinda kwa makubaliano(win-win situation) lakini msipo kubaliana hapo basi kwa makubaliano shauri linapelekwa hatua ya Uhamuzi(Arbitration)

2. Katika uhamuzi(Arbitration)- ndipo sasa taratibu za kisheria zinachukua mkondo wake haswa na ndipo mnatakiwa kuleta ushaidi wa kile kinachobishaniwa na hatimaye mwamuzi(arbitrator) anafikia hatua ya kutoa uhamuzi wenye nguvu ya kisheria. hapa sasa kuna concept ya KUSHINDA AU KUSHINDWA (win-lose situation) sasa baada ya hapo; kinachofuta ni kama Mh. Nduu/mamaya alivyofafanua.
 
Mkuu Lusinde naona ishu hii ni ya muda mrefu sana. Naomba feedback, umemalizana vipi na jamaa...., au bado mizengwe mizengwe!!
 
Kesi hii ilipoiilipoingia kwenye uamuzi iliamuliwa upande mmoja tukapewa ushindi. Akagoma kulipa,tukaenda kwenye kukaza hukumu mahakamani,paia akaamuliwa kulipa,hakufanya hivyo,mahakama ikatoa amri kwamba mali zake zikamatwe ili kulipa deni,akakata rufaa akidai pesa alizotakiwa kulipa ni nyingi tofauti na pesa alizokuwa ameamliwa na mwamuzi ,hivyo alilazimika kudiposit pesa pale mahakamani ili gari zake ziachiwe ili na rufaa yake isikilizwe. Baada ya rufaa kukatwa alikuja akaiondoa mahakamani ,sisi tukaendelea na ukazaji hukumu,tukashinda na akaamuliwa kulipa.hakufanya hivyo,bali alika rufaa akidai msajiri hana uwezo wa kufanya hesabu zetu upya ila mwamuzi. MpakaMpaka february 18 mwaka jana mahakama ikampa ushindi ila hukumu hiyo ilikuwa imetengua hukumu ya msajiri na ikawa imekaa kimya bila kuonyesha nini kinaendelea juu ya kesi yetu ikiwa na maana kuwa kesi imekwisha na sisi kuwa tumeshindwa.
 
Back
Top Bottom