Kwanini kiharusi mara nyingi hutokea bafuni au chooni?

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Nawashauri watu msioshe kichwa na nywele mwanzo mnapo anza kuoga! Ni makosa makubwa haya.

Hii inasababisha kubadilisha hali ya ujoto katika mwili wako haraka sana (na miili yetu ina Damu ya moto) na hivi kufanya mishipa ya Damu inayopeleka kwenye ubongo kuchanika na kupasuka na inahatarisha kwa binaadamu kupata kiharusi kwa haraka sana.

Njia nzuri ya mtu kuoga ni kuanza kutia maji katika mwili au miguu kwanza kabla ya kichwa ili kuweza kuupa mwili uzoefu na kufanya usawa katika ujoto wa Damu.
FB_IMG_1516946562007.jpg

Kuna ukweli ktk hilo jambo?
 
Ukweli upo, kwasababu kuna mifano halisi,, ila inategemea na maji unayooga,, ni ya baridi sana, ya baridi au ya uvugu vugu,, ukianza na ya baridi sana, ni kweli mishipa itasinyaa, lakini kumbuka kuwa kiharusi huambatana sana na shinikizo la damu,, kwahiyo, shinikizo ni kubwa, mishipa imesinyaa ghafla, na ni mishipa midogo milaini, kwahiyo kuna uwezekano wa kupasuka,,
 
Hakuna hewa ya oxygen ya kutosha na madirisha yake madogo
 
Mimi nakumbuka niliwahi kuanguka bafuni kabla sijaanza kuoga ila wakati huo nilikuwa naumwa kikohozi cha ajabu kbs.

Ubaya wa kuishi peke yako ndio huo nlikaanilipoteza fahamu kama nusu saa kilichonizindua ni maji nilikuwa nimefungulia kwny ndoo yalijaa yakamwagika na lile tundu la kutolea maji nilikuwa nmelilalia yakawa hayana pa kwenda ndio yalikuja kunizindua.
 
Mbona hukufa?
 
Daaah!
Mpaka Leo ingekuwa Kaburi lako tunafukua kupitisha Bomba la Mafuta toka Uganda
Poleni na Hongera kuepuka kufa kwa Muda
 
Hili ndio tukio langu la mwisho kubwa kunusurika kifo,mengine mawili yalikuwa ya ajali.

Mungu ni mwema jamani
 
Watu watumie vyoo vya kukaa zaidi hii ni kwa mujibu wa prof, janabi.
Vyoo vya kukaa navyo tunaambiwa vinachangia kwenye Kansa ya Njia ya haja kubwa kwa kuwa uchafu wote hauwezi kutoka wakati wa kuutoa!

Mkunjo unaojikunja kwenye choo cha kuchuchumaa hauachi uchafu tumboni
 
Nimejaribu kutafakari wengi ninaowafahamu waliofariki bafuni kwa tatizo hilo wengi ni wanaume.. Pengine kuna ukweli kwa maana wanawake hawapendelei kutia maji nywele zao. Ngoja niendelee kukusanya data zaidi. Ahsante kwa somo mkuu.
 
Hakuna uhusiano ILA ninachojua lazima kabla hujaingia chooni au bafuni usome Dua maana kule kuna Majini ya kiume na kike au masheitwani hivyo huweza kukukumba mda wowote. Mengine hutumwa mengine ndo home. Unatakiwa useme Allahuma inni audhubika minal khubuth walkhabaith. Tafsiri ni kuwa Ee mola nakuomba unikinge kutokana na masheitwani wanaume na wanawake. Na ukitoka pia uombe Dua ya kushkuru na kuomba msamaha. Ghufuranaka. Ee mola nisamehe.
 
Vyoo vya kukaa navyo tunaambiwa vinachangia kwenye Kansa ya Njia ya haja kubwa kwa kuwa uchafu wote hauwezi kutoka wakati wa kuutoa!

Mkunjo unaojikunja kwenye choo cha kuchuchumaa hachi uchafu tumboni
Yeah, kukaa sio njia asili ya kutoa haja kubwa. Ile angle kati ya mlango na utumbo mkubwa hairuhusu mzigo wote kutoka.

Hata hivyo kama una choo cha kukaa unaweza kutatua hili tatizo kwa kuweka kitu kinachonyanyua miguu juu kama kigoda hivi.
 
Kuna video moja niliona inaonyesha jinsi ya kutumia choo cha kukaa ili ufungue njia vzr
 
Ukweli upo, kwasababu kuna mifano halisi,, ila inategemea na maji unayooga,, ni ya baridi sana, ya baridi au ya uvugu vugu,, ukianza na ya baridi sana, ni kweli mishipa itasinyaa, lakini kumbuka kuwa kiharusi huambatana sana na shinikizo la damu,, kwahiyo, shinikizo ni kubwa, mishipa imesinyaa ghafla, na ni mishipa midogo milaini, kwahiyo kuna uwezekano wa kupasuka,,
Sababu ni kupiga nyeto bafuni zaidi uwapata wanaume
 
Back
Top Bottom