Kwanini kijana wa kiume ukisema kuna hela naisikilizia huaminiki?

Kwanini kijana wa kiume ukisema kuna hela naisikilizia huaminiki?

The Eric

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
6,446
Reaction score
10,976
Salaam!

Hivi kwanini wakuu watu siku hizi ukiwaambia kuna hela nasikilizia hapa au kuna mishe naisikilizia hapa wanaona kama kijana analeta janja janja 😅😅😅

Tena ukitaka uachane na demu akuombe pesa afu umjibu kuna mishe nasikilizia hapa itiki ✅ ✔ yaani ile ikitiki nitakusanua, huyo demu lazima muachane.

Sasa vijana nao wengi wana stori nyingi sasa hivi hawasemi tena kuna mishe nasikilizia hapa.

Lakini kuna wakati kweli unakuta kuna mishe au hela unasikilizia ila hutoaminika kabisa.
 
Inaonesha jinsi gani hauko makini. Inajulikana kodi lini inalipwa, badala ya kuwa na pesa ndio kwanza unaanza hadithi kama hii?
Pesa haijawahi kuwa rahisi mi nakuona kama wewe ndiyo mwenye nyumba ushauziwa.
 
Duniani hakuna kundi la watu waongo kama vijana, kijana kuaminika ni kipengele sana.
 
Kuna mishe naisikilizia " hii statement imekaa kihuni fulani hivi,, na muhuni kibongo bongo directly ni tapeli, na tapeli ni mtu asiyeaminika hata na mtoto mdogo.
 
Back
Top Bottom