Kwanini kila kitu kizuri lazima kiitwe jina la Mwanasiasa?

tubalayya

Senior Member
Joined
Apr 16, 2010
Posts
117
Reaction score
203
Nisingeandika haya lau si kuchukizwa na kitendo hiki cha kishamba: kila kitu chetu kiitwe jina la mwanasiasa, awe hai au amefariki.

Nchi hii ina watu wengi waliochangia kwa kiwango kikubwa na hata kufahamika duniani kutokana na mchango wao. Lakini ni wanasiasa tu, wengi wao wakiwa wameharibu zaidi kuliko walivyojenga, ndiyo wanaokumbukwa. Naapa, kama nitakuwa Rais, na hiyo ni haki yangu, nitafuta majina mengi ya hawa na kuweka majina ya wale waliojitolea kwa dhati bila kupata manufaa makubwa ya kifedha.

  1. Elimu na Uandishi
  • Shaaban Robert
  • Abdulrazak Gurnah
  • Mohammed Said Abdulla
  • Euphrase Kezilahabi
  • Mohamed Said

  1. Uhifadhi wa Mazingira
  • Jane Goodall
  • Mary Leakey
  • Fidelis Masao

  1. Michezo
  • Filbert Bayi
  • Juma Ikangaa
  • Suleiman Nyambui
  • John Stephen Akhwari (wengi hawamjui Bongo, lakini nje ya nchi jina lake hutolewa kama mfano katika vikao vya mafunzo Ulaya, Marekani na hata Asia. Katika Olimpiki ya 1968 nchini Mexico, pamoja na kuumia vibaya mwanzoni mwa mbio, Akhwari aling’ang’ania kuzimaliza.

Alifika saa 12 baada ya washindi, wakati giza likianza kuingia. Alipoulizwa kwa nini hakukata tamaa, alisema: “Nchi yangu haikunituma kilomita 5,000 kuja kuanza mbio; ilinituma kuja kuzimaliza.”

Katika kozi moja Chuo Kikuu cha Wales, mwalimu mmoja alimtaja kama mfano wa azma na ukakamavu wa kufikia lengo. Hawa magabacholi wana uzalendo huo?)



Sayansi na Tiba
  • Mwele Malecela
  • Mohammed Yakub Janabi
  • Yohana Wavenza Lusambo
  • Dr. Askwar Hilonga (aliyegundua chujio cha maji kinachotumia nanoteknolojia, kilichopata sifa duniani)

  1. Uvumbuzi na Ugunduzi
  • Jumanne Mhero Ngoma (mvumbuzi wa Tanzanite)

Ongezeni majina mengine. Naamini wako wengi walioipa nchi yetu heshima kubwa lakini hawatambuliwi. Siku zote tunawatukuza wanasiasa pekee waliotufikisha hapa.

Hata miongoni mwa wanasiasa hao, wapo waliofanya mengi lakini hawakumbukwi.
 
Samahani mtoa mada! Kwani kumetokea nini tena huko mjini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…