Huyu B-boy ukimskiliza vizuri utagundua ako na kitu kwenye namna anavyotengeneza midundo yake.
Sijajua ni labda kwakua wako na muunganiko mzuri na huyu kijana Harmonize au ni kweli anauwezo mkubwa kwenye midundo ya aina hii.
Kwenye huu wimbo wa "me too" alitulia sana kwa maana wimbo umenyooka kiasi cha kumfanya msikilizaji asione shida kuurudia kwa kadri anavyoona inafaa(ofcoz waimbaji wamefanya kazi kubwa nao na ndio maana sauti na mdundo viko kwenye muunganiko ulio sawa).
Sasa, kama kawaida kwenye playlist yangu ya Leo huu wimbo nao ulikua miongoni mwao (namaanisha huo wimbo wa "me too") and ofcoz niliurudia mara kadhaa.
Ila hapa kwenye kuurudia sasa ndio hisia zilikua zinahama na kuanza kuingia kwenye wimbo wa Maua Sama na Ibrah Nation wa "sukari guru" ambao huu wimbo mdundo wake ulitengenezwa na Emma the boy(huyu nae sijui alipoteleaga wapi but alikua na sanaa nzuri sana ya kutengeneza midundo)
Sijajua kuna muunganiko gani kati ya hizi nyimbo mbili ila nahisi kuna kitu kipo kati yake, ni labda namna duets ilivyofanyika kwa nyimbo zote au huyu B-boy na Emma the boy kuna mahala wamekutana kwenye midundo ya hizi ngoma au ni Mimi nimeanza kuzeeka vibayaπ€£π€£.
Kutokana na hili nimeona niweke maneno jamvini ili wataalam mniambie kwanza, ni uzee wangu unanikujia vibaya au ni kweli kuna muunganiko usio wa moja kwa moja upo kwenye hizo nyimbo?π π
But huo wimbo sikuwa nao kwenye playlist yangu na sikuwa nimeuskiliza kwa muda mrefu sana ila baada ya hapo ndio ikabidi niutafute nione kama kuna connection yoyote.