Kwanini Kingunge asihstakiwe

Kwanini Kingunge asihstakiwe

Mbogela

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2008
Posts
1,384
Reaction score
258
Miaka kama mitatu hivi kumekuwa na kesi za makampuni makubwa duniana kuficha taarifa za mapato yao na kuwafanya maboss wa makampuni na wamiliki wake kufikishwa mahakamani. Sasa je kwanini sisi tusimfikishe mahakamani Kingunge Ngombale Mwilu kwa kuficha ukweli kwa makusudi kabisa huku akijua anatenda kosa kinyume na sheria za JMT juu ya mapato ambayo kampuni yake ilikuwa ikikusanya Ubungo bus terminal?

Jiji lanusa mchezo mchafu stendi ya Ubungo
Imeandikwa na Irada Mahadhi; Tarehe: 25th November 2009 @ 06:09

MAPATO katika Kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani cha Ubungo (UBT), yameongezeka kutoka sh milioni moja kwa siku hadi sh milioni nne.

Wakati Kampuni ya Smart Holdings ilipokuwa ikikusanya mapato kituoni hapo ilidaiwa kuwa ilikuwa inakusanya sh milioni moja kwa siku, lakini baada ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuchukua jukumu hilo sasa zinapatikana sh milioni nne kwa siku.

Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji, Ahmed Mwilima, alitoa taarifa hiyo jana katika Baraza la Madiwani la Jiji na kusema kutokana na ongezeko hilo, inaonesha kulikuwa na mizengwe katika taarifa zilizokuwa zikitolewa awali kuhusu mradi huo.

Mwilima ambaye alikuwa akizungumzia juu ya mapato yatokanayo na mradi huo wa ukusanyaji mapato UBT, alisema halmashauri imegundua kuwa mapato yaliyokuwa yakidaiwa kukusanywa awali yalikuwa ni kidogo.

Alisema halmashauri haijaamua imkabidhi nani mradi huo kwa kuwa wanaendelea kufanya uchunguzi wa utendaji wake na vielelezo vyote muhimu kwa ujumla ili kuepuka utata kama uliotokea awali.

"Suala hili ni nyeti, linahitaji umakini wa hali ya juu katika kulitekeleza na kabla ya kukabidhi mradi huu kwa yeyote. Ni vizuri halmashauri iendelee kuuendesha kwa sasa ili kujua uhalisia wa makusanyo yake na utendaji wake ili kabla ya kukabidhi au kutafuta mkusanyaji mwingine, halmashauri iwe tayari na maelezo yote muhimu yanayotakiwa kuhusu mradi huo ili kuepuka mtafaruku mwingine kama wa awali," alisema Mwilima.

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilianza kazi ya kukusanya mapato katika kituo hicho Novemba mosi mwaka huu kutokana na kumalizika kwa mkataba wa Kampuni ya Smart Holdings inayomilikwa na familia ya mwanasiasa mkongwe na Mbunge wa Kuteuliwa, Kingunge Ngombale-Mwiru.

Wakati wa usimamizi wa kampuni hiyo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwahi kutembelea kituoni hapo na kubaini kuwepo kasoro katika ukusanyaji wa mapato.

Alimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua mapato na matumizi ya makusanyo katika kituo hicho pamoja na Soko Kuu la Kariakoo.

Tayari CAG ametoa ripoti zake na kumkabidhi Waziri Mkuu ambaye wataalamu wake wanaendelea kuzifanyia kazi. http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=4542&cat=kitaifa

Hizi kesi za ufisadi zitaisha lini nchi hii? kila siku zinazaliwa mpya?
 
Mie nawashangaa sana Jiji kwa kuzubaa hadi wakati huu kuweza kuchukua shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na familia ya Mzee Fisadi Kingunge. Hii wanaokusanya fedha za parking kwenye mitaa ya jijini hapa si ndio hao hao familia ya Kingunge? Kwa nini Jiji wasiifanya na kazi hiyo ili kuongeza mapato hatimaye waweze kujenga parking systems za underground na hata kujenga barabara za juu kupunguza msongamano unaokera?

Si Kingunge huyu huyu aliyekuwa kwenye Serikali ya Ujamaa na Kujitegemea? Leo kageuka jiwe kawa Bepari mkubwa anayenyonya mapato ya Taifa!
 
Mie nawashangaa sana Jiji ...... Kwa nini Jiji wasiifanya na kazi hiyo ili kuongeza mapato hatimaye waweze kujenga parking systems za underground na hata kujenga barabara za juu kupunguza msongamano unaokera?

!

Asante sana mkuu lakini nadhani kumpokonya na kuongeza mapato ni jambo moja lakini kwanini tusiwe kama wenzetu, huyu ni wa mahakamani, huu ni wizi wa makusudi. Nchi zilizoendelea huwezi kuficha mapato ya kampuni yako, sembuse huyu alipewa tenda, UBT yetu, yeye kaficha kile anachochuma kwenye kitega uchumi wetu. Kama serikali yetu ipo serious tunategemea kusikia Kingunge amevuliwa ubunge na kesho yupo mahakamani na hii kesi tunashinda. Mbona tukizungumzia Downs wanasema wanaogopa atatupeleka mahakamani, kwanini nasisi tusiogopwe na vifisadi kama akina Kingunge kuwa wakidokoa tu tunao, tunwavutia mahakamani na kesho wapo keko kutumika miaka?
 
Back
Top Bottom