Kwanini kipande cha barabara Kimara - Ubungo kimeachwa?

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,311
Reaction score
15,640
Tumejenga fylover ubungo na kweli saa hizi hatuna tena foleni za ajabu pale. Tukapanua barabara kuanzia Kimara Mwisho hadi Kibaha na kweli njia hii unatirirka tu.

Ila ajabu na cha kushangaza ni hiki kipande cha Ubungo hadi Kimara, kwanini kimeachwa? Yaani unatiririka vizuri ila ukifika tu hiki kipande unawaza foleni.

Hivi hawa Tanroads wanakaaga kabisa na kuwaza? Hii njia inamalori sana na daladala nyingi na zote zinaumana kwenye hiki kipande.

Daladala zinasimama barabarani kupakia na kushusha,malori nayo hayakawii kuzingua na kuziba barabara...kwanini wasipanue hata njia za muda zile za pembeni kuendana na flyover ya Ubungo na njia 8 ya Mbezi? Labda mnaojua mtanielewesha huenda uelewa wangu ndo tatizo.
 
Plan ya ubungo hadi kimara haiwezekani aisee ni gharama sana labda wanaona na pengine makazi ya watu ni mengi ishu za fidia zitakuwa changamoto
Fidia walisha lipwa siku nyingiii na notes walishapewa ...yaan pale ni swala la any time any day ikimpendeza mkuu wa wakuu wote ..akitamka + fedha ikiwepo mfukoni basi kina sanuliwa pale
 
Fidia walisha lipwa siku nyingiii na notes walishapewa ...yaan pale ni swala la any time any day ikimpendeza mkuu wa wakuu wote ..akitamka + fedha ikiwepo mfukoni basi kina sanuliwa pale
fidia walilipwa lini? leta usaidi wa hiyo fidia kulipwa
Kwa taarifa yako Waliobomolewa kimara hadi mbezi na magufuli bila kulipwa fidia wameshinda kesi mahakamni serikali inatakiwa kuwalipa fidia karibia tirion 2
 
Sasa ulitaka njia nane iende hadi wapi? It had to stop somewhere
 
Tatizo waliokwisha lipwa fidia walishauza maeneo yao zamani.
hakuna kitu kama hicho naweza kukupa mfano Thomas Lyimo analigodown lake ni gereji lipo tokea miaka ya 80 huko wakazi wengi wa kipande hicho ni wakazi wa miaka zaidi ya 40 walinunua wakati huko ni mapori na wapo hadi sasa.
Wengi wao ni wachaga nakwambia hakuna mchaga anayeuza ardhi yake kirahisirahisi
 
Kiko kwenye upanuzi na matayarisho yameshaanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…