Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Alafu nnachoshangaa mi kitabu cha tobiti akiubiliwi kabisa na wachungaji maaskofu mapadre kwanini???
Wewe tu huubiwa sana labda makanisani (Catholic)/endelea kuhhdhuria Ibada za kila siku asubuh saa 12:30 na jumatano saa 10:30 jioni pamoja jumapili utavisikia...
 
Kama wewe ulivisoma na havikukutenga,kwa nini unakuwa sehemu ya watu wanaokandamiza haki za wengine kuvisoma vitabu hivyo?Huoni hii ni tabia ya kiburi na majigambo dhidi ya watu wengine unaowaona hawawezi kufikiri vizuri?Nachukia sana ujinga huu ambao umerudisha nyuma sana maendeleo ya mwafrika.

Waafrika tubadilike,kama unaamini nguvu ya roho mtakatifu,na kwamba kila mtu ana haki ya kumpokea,kwa nini uwe na mashaka kwa watu wengine kusoma vitabu hivyo?
 
Kwani biblia imeandikwa na nani mkuu
Kimeandikwa na watu watano tofauti na HENOKO hakukiandika cha kushangaza anasema I ENOCH kila anapokuwa quoted as if yye ndio alioandika......

Nachotaka muelewe ni kwamba kimeandikwa miaka 300 kabla ya Yesu sasa Henoko alishakuwa amekufa hivyo msihusishe hicho kitabu na Henoko mnashangaza sana

Tafiti zote zineonyesha zile script hazikuwepo kabla ya huo mwaka 300 BC ssa mnakazania ni Henoko alieandika ili iweje??

Kina ukweli kiasi ila 70% iliyobaki ilichezewa na waandishi wa mashariki ya kati hivyo hakina credibility kabisa ya kuwekwa kwenye biblia

Kwa ufupi Henoko hamtambui Yesu kma Mungu wala hatambui kma kuna kukombolewa kutoka dhambini sasa mnaoking'ang'ania sijui mna ajenda gani
 
Kinajichanganya na biblia sasa ukisoma huoni unaweza kuwa kwenye njiapanda kwamba uamini mwandishi wa mwanzo au umuamini mwandishi wa Henoko ???

Sasa biblia haijasema kma malaika walizaa na binadam ila henoko anasema hivo

Henoko anasema Safina ya nuhu ilijengwa na malaika watupu ila biblia inasema alijenga Nuhu sasa huoni itachanganya wakristo
 
Ukisoma kitabu cha Henoko 8:1 - 8 utaona Henoko anavyoelezea jinsi ambavyo wale malaika walioshuka pale kilele cha Ardis mlima Armon ambao waliwaingilia wana wa binadam (Henoko 7:1-8), utaona anasema jinsi walivyowafundisha binadamu maarifa ya kutengeneza silaha, uganga (sorcery), elimu ya nyota, n.k.

Nauliza, ikiwa haya mambo ni kweli yalitokea na ni kweli ukiona hata leo kwa kiasi kikubwa waganga na watabiri wa nyota ni kama wana ushirika na majini au pepo wabaya ambao kwa uelewa wangu ndio hao malaika walioanguka, je, kuandika habari hizi kunakifanya kitabu kikose sifa ya “utakatifu” kama vitabu vingine tunavyosoma leo katika Biblia?
 
We jamaa unaboa sana!Kama ni ubishi ni ubishi wa kishamba sana!Unaulizwa swali kwa hoja,unajibu kwa hisia zako!Hakuna swali ulilojibu kwa hoja,isipokuwa kwa jinsi ya kujibu tamaa zako na kukwepa hofu unayoiona mbele yako.

Ila kumbuka, Mungu ana nguvu kuliko ujanja ujanja wa kibinadamu na katika vizazi vyote watakuwepo tu wanaomcha yeye.
 
tatizo la watu wengi ni mareligious na sio spritual so kuna vitu hawataweza kuvijua maishani ! kuna biblia 6000 huku duniani .achana na hii moja ya mzungu aliyoiframe kwa manufaa yake hapa africa
Acha uongo wewe hebu taja hizo biblia zako
 
baby wangu kumbe unamjua Mungu eeh ngoja nitafute kitabu cha tomaso halafu kitakuwa cha kweli maana huyu tomaso alikuwa mwanafunzi wa yesu so ina maana aliyoandika ni ya kweli maana aliyaona unlike kina mathayo .luka marko wale walisimuliwa tu
There was a time a lot of people were writing books and naming them after the disciples of jesus
So sio kila ukiona jina kwamba it was genuinely written by that character sio kweli
 
The problem is we Africans and probably Arabs
Siku zote tubakuwa tunatafuta sababu za kujipa moyo about our sacred nature and so on ......all those are conspiracy theories watu wore ni sawa hakuna mashetani wala nini we are all genuine humans
 
King james bible ndio version sahihi ya bible
I hate tabia ya Ku draw conclusions without research ....how do you know that the bible we use is corrupt?

Who are u by the way ?
Au u participated in that corruption!!!!

You guys should understand those are just translations !!!! Kama unataka original learn Hebrew ,Aramaic and Latin ukasome the natural language
 
Tanzanians kuna reason kubwa behind theological rejection ya hicho kitabu !!!
That book ukisoma utagundua hakiko consistent with other biblical books kimalize chote utaona matango pori yaliomo humo


By the way wanakitumia Ethiopian Orthodox church tyu
 
Simply scrolls za hicho kitabu ziligunduliwa Ethiopia.
Na zinamuelezea binadamu wa kwanza kua ni mtu mweusi.
Ila kuna mtoto alizaliwa mwenye rangi kama ya Malaika (Albino).
Kitabu cha Enoch kina mpa superiority Mtu mweusi ndio maana kilitolewa.
Deceit
 
Injili ya barnaba pia ilifutwa..
Sijui kama maelezo ya yesu kuoa ni ya kweli
Injili ya Barnabas kiliandikwa baadae sana na mhispania mmoja ambaye alikuwa no roman catholic alipobadili dini na kuwa muislam ndo akaandika kitabu hicho

Hakihusiani na Barnabas mwanafunzi was Paulo hata kidogo
Intact ukifanya simple examination ya hicho kitabu utagundua it was written 10A.D sasa miaka kama 1000 baada ya yesu na mitume wote kufariki in kitabu cha kipuuzi tyuu
 
There u talked brother
 
Mimi lmani yangu Iko stable, najua uongo ni UPI na ukweli UPI , hivyo hata nisome kitabu kipi hakiwezi niteteresha kiimani maana ukweli naujua. Mkristo mwenye imani changa akisoma katabu cha Enoch ataweza kuterereka katika imani..kitabu cha Enoch hakijulikani mwandishi ni nani. Ukitazama kwa undani zaidi, utakuta mafundisho ya Gnostic yanabeba sehemu Fulani katika kitabu cha Enoch.

Vile vile kitabu cha Enoch kina alama au symbols zinazotumiwa na waabudu mashetani. Kwa mfano nyota ya pentagram, (nyota ya pembe tano iliyosimamia ncha moja). Nyota ya Mfalme Daudi,(pembe tatu mbili zinazoingiliana).Vile vile kitabu cha Enoch kina maelezo zaidi kuhusu malaika kuliko kumhusu Mungu.

Kwa hivyo kitabu cha Enoch hakimsaidii Mtu mchanga kiimani, isipokuwa kumuelekeza katika kuabudu malaika ambao ndio walioelezewa zaidi ndani ya kitabu hicho.
 
Salute.
Unafaham malaika waliopo kwenye kundi la Matatron Arch angels..?
 
Mkuu ni kweli, kitabu cha ench Hakina msaada wowote kwa wokovu wa mwanadamu..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…