Kwanini kitabu cha Enoch kinapingwa vikali na Wanathiolojia?

Yetu niyale ambayo ametufunulia ambayo hatujafunuliwa sio yetu wala tusihamgaike nayo maana hakuna awezae kuongeza limo cha urefu ulio nao. WEWE MKUBALI YESU KUWA MWOKOZI WA MAISHA YAKO TU.
Muwe mnajaribu kufikiri nje ya boksi,, hivi haujui kuna watu walikaa kuipanga Biblia, kwani unafikiri walikuwa watakatifu sana??
 
Huna haja ya kuogopa....Vitabuvya Apocripha vipo vingi sana,,,,,Hata kule kwenye Agano la Kale vipo kibao...Ila havina maana yoyote kwa maisha ya Mkristo zaidi ya kujaa uzushi na ushabiki...
Kwanini sasa useme vimejaa uzushi??, Ni nani hao waliokuwa wanavichambua wanaona hichi ni uzushi na hichi sio??, Na vipi kama walikuwa wanafanya kwa maslahi yao???
 
Biblia gani hiyo inaongelea mambo ya sisimizi??
 
Uwezo wako wa kufikiri hauko kama unavyoufikiria kuwa,,
 
Mungu tutamwonaje na hataki kujitambulisha tumuone live.
Huwezi kumuona Mungu ana kwa ana kupitia macho yako ya damu na nyama. Mungu ni Roho, ukitaka kumuona ni kupitia ibada katika roho sio mwili, na wala sio kupitia jicho la tatu kama meditators wanavyowadanganya wafuasi wao.

Kuona kupitia jicho la tatu, utaweza kuwaona, kuzungumza na hao malaika walioelezewa katika kitabu cha Enoch.(fallen Angels).
 
Kama mungu ni mwenye kusamehe uko mnapopaita jehanam kwa kazi gani si autoe hata uo moto maana hatamuhukumu mtu wote tutasamehewa.

Na swala la mbinguni wewe unaamini vipi kuwa mbinguni ni kwa wanadamu wakati hiyo bibilia inasema kuwa mbingu ni mahala na makazi ya malaika,je itawezekana kweli malaika wakachangamana na wanadamu na kuishi pamoja?.

Kuna mambo ukiyasoma inaonesha wazi tunalishwa matongo pori si ndo hiyohiyo bibilia inasema dhambi zote ni sawa sasa hapa unamfunza mwanadamu nini ndipo unakuta mtu anabaka na kujiamanisha kuwa endapo alipitiwa na uovu ata samehewa lakini pia licha ya msamaha kiutendaji dhambi yuko sawa hata na yule mtu muongofu(mdanganyaji)


embu tuwe tunajitoa tongotongo kwa ishu nyingine sio ushabiki tu usio na mbele wala nyuma,bibilia inazingua sana na nadiliki kusema imeharibu watu na imewapaka dhambi zaidi na dhambi kuu iliowapaka watu ni hii MUNGU NI MWENYE KUSAMEHE NA SISI NI WANA WAMGU.


wana wa mungu haitakuja iwe na haitatokea akawa mwanadamu,mungu alimuumba mwanadamu kwa mfano wake/wao....(kwenye bibble uko kumejikanya two place ya kwanza wao ikaja wake)sasa kama mimi niliumbwa kuwa kama mfano ni vipi aniite mwana wake?,katka kushushwa kwa yesu ambaye pia ni malaika,hapa niwe mtulivu kuna sehemu uko juu umempinga enock alipomtaja yesu kama malaika umebisha kuwa sio malaika,sasa wewe kama unabisha yesu si malaika mbona shetani alikuwa malaika miongoni mwa malaika wenzie,na bibilia inasema yesu alikuwako na aliitwa NENO,basi katka hili neno kuna kitu humu,maana mungu aliumba dunia kwa kutumia neno kumbe kama alitumia neno alisaidiyana na huyu yesu ambaye aliitwa neno,kwa hiyo yesu na ni malaika na ana uungu ndani yake.
 
Acha kutudanganya mungu yupi umemwona wewe au matokeo ya mambo yako kwenda vizuri ndo mungu.

Sisi tuna tatizo moja mzungu alishatuwahi kutulisha hii sumu ya kitu inaitwa imani ya bibilia hatuwezi kuitema...


We toka lini watu wamevipanga vitabu huko wakatuletea huku sisi tunaamini bibilia ni kitabu kitakatifu si ufala huu..


Yesu mwenyewe alitumia maandiko halisi ya manabii wa nyuma katika masinagogi hakudiliki kuyasema kuwa yalikuwa maandiko matakatifu..


Tuache utoto tukuwe tusijifanye wajuaji wakati watu wamekaa tu uko wanatuchora tunavyominyana uku...niko naendelea kusoma hoja zenu endeleeni.
 
Wewe umenijibu vzr sana.
 
Hahahhaaa mkuu kuna situation ambazo unaamini Mungu yuko... Kuna siku nilikuwa nanyongwa ili nife ila nilipoita jina la Mungu aliyehai yaani aliyekuwa ananinyonga akaachia tu ghafla na kutoweka hapo hapo sasa unafkiri Mimi zitto junior hapo siwezi kuamini kuwa Mungu yupo??

Kuna situation nyingi tu nimepitia nakumbuka hta mtihani wa kidato cha 6 nlikuwa nna shida flani hivyo sikuweza kusoma miezi miwili ya mwisho ila nakumbuka niliandika marks nazotaka Mungu anipe na nliweka kwenye karatasi na nikapeleka madhabahuni tukaiombea..... Ingawa mitihani nilifanya kwa kuunga unga ila marks zilikuja vilevile kma nlivyoandika kwenye ile karatasi sasa unafikiri nikisema NIMEMUONA MUNGU nadanganya???

Anyway haya mambo ni ya kiroho ila cku akitokea mchawi au jini ambao lazima upambane nao kiroho ndio nahisi unaweza kuamini kuwa Mungu naye yupo... Hiyo ni kama unaamini shetani yupo pia!!
 
1. Mkuu kuhusu Yesu kuwa malaika kwanza elewa mimi reference yangu ni biblia na hakuna sehemu kwenye biblia ambapo Yesu anatambulishwa kama malaika tu mara zote anatambulishwa kama mwana wa Mungu yaani Mungu mwana katika ule utatu mtakatifu

2. Huyo anayejiita Henoko sijampinga tu kuhusu kumuita Yesu malaika ila pia nampinga maeneo mengi ikiwemo kusema wanefili walikuwa na urefu mpaka Futi 450!!! Yaani warefu kuliko safina ya Nuhu afu eti wakaomba Nuhu awafungulie waingie???? Yaani aingie kwenye kitu anachokizidi ukubwa???.... Pia nampinga alipotosha kuwa safina ya Nuhu ilijengwa na malaika na sio Nuhu mwenyewe???.... Na mengine mengi tu ikiwemo ya kumfananisha Yesu kma malaika wa kawaida tu ilihali manabii wengine wote walimuona kma Messiah na Mwana wa Mungu atakayekomboa ulimwengu ila Henoko anasema Yesu atakuja kuharibu ulimwengu na wenye dhambi kumalizwa ??!!!!

3. Jehanum hakuumbiwa mwanadamu ilikuwa hukumu kwa Lucifer.... Sema shetani ndio anawadanganya wanadamu toka siku ile amepenyeza dhambi kwenye bustani ya Eden hivyo ukiasi Mungu basi unakuwa mali ya shetani ambaye kwake ni jehanum ila kabla ya anguko la Adam hatukupaswa kwenda jehanum wala hakukuwa na kifo ila shetani ndio anataka kwenda na wenzake huko hivyo sio kweli Mungu aliweka jehanum kwa ajili ya wanadam

4. Kuhusu msamaha..... Kumbuka Mungu alishajua fate yetu kwamba utakuwa moto wa milele maana watu walimuasi na kufanya dhambi ila kwa kuwa ana huruma na upendo akatupa neema ya kuepuka kwenda Jehanum kwa kumtuma mwanaye Yesu kristo aje atuokoe na kweli alikuja akafundisha na kuturudisha kwenye mstari na hata sasa tuna neema ya kwenda mbinguni ambayo zamani haikuwepo sababu dunia nzima hata wayahudi walikuwa wameasi na wanaabudu miungu wa ajabu ajabu..... Sasa bila msamaha angemtuma Yesu??? Kwanini ametupa second chance???

NB: msamaha upo kwa atakayeutaka sio ndio kwamba unasemehewa ilihali hujaungama dhambi
.... Ila ukikiri na kuomba msamaha Mungu anasamehe hapo hapo nafkiri unakumbuka yule jambazi pale msalabani pamoja na madhambi yake yote aliomba msamaha palepale akaambiwa ataenda mbinguni!!!

Ahsante
 
Biblia gani hiyo inaongelea mambo ya sisimizi??
Book of jasher sura za kwanza kwanza utakuta habari za henoko.... Sio ya sisimizi tu ila alikuwa kwa wiki anafunga siku 6 na siku moja tu ndio anatoka hadharani.

Alikuwa anaogopa dhambi hadi akajitenga na watu akaishi kwenye mapango ili asije shawishika kufanya dhambi. Kwa maelezo zaidi soma hicho kitabu ingawa biblia haikitambui so soma tu kama historia basi
 
Kwanini sasa useme vimejaa uzushi??, Ni nani hao waliokuwa wanavichambua wanaona hichi ni uzushi na hichi sio??, Na vipi kama walikuwa wanafanya kwa maslahi yao???
Uzushi sababu vinaongelea mambo tofauti na manabii wengine wa kwenye biblia.

Mfano Biblia tunajua Henoko alichukuliwa na Mungu YEYE KAMA YEYE ila Book of jasher inatuaminisha waliomfuata walikuwa takriban laki 6 wakati safari inaanza walipaa naye maana hawakukuta mwili wowote wala mabaki ya wale watu laki sita eneo ambalo Henoko alipaa sasa kma sio uzushi ni nini?
 
Nilichojifunza katika kitabu cha Enoch ni juu ya origin ya mtu mweupe (kina eleza Mungu aliumba mtu mweusi ila mtu mweupe alitokana na malaika wenye tamaa i.e fallen angels waliokuwa wakiwaingilia kimwili binadamu)

Aliumba mtu mweusi sasa kwanini manabii aliokua akiwatuma walikua ni weupe au baada ya kutokea akawa hana jinsi ikabidi awahalalishe tu?
 
kuna majadiliano yaliwahi kufanywa na CNN kuhusiana na kuharibiwa old bible ambayo inasemekana ilikuwa inamzungumzia zaidi mtu mweusi na pia wazungu ni uzao uliolaaniwa uliotokana na wale malaika waliowaingilia watoto wa binadamu
 
Wachina, Wahindi, Korean nao asili yao ni fallen angel?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…