fungi06
JF-Expert Member
- Jul 1, 2020
- 738
- 1,017
Binafsi mimi ni mpenzi mno wa chakula yani napenda sana kula chakula kizuri, kisafi, kitamu, ambavyo vinajenga mwili na akili kama sote tujuavyo dhamira kuu ya chakula mwili..
Nimekua nikijiuliza sana kwa nini visu vyangu kila nikikatia vitunguu geto vinaanza kuisha makali mdogo mdogo
Nilishtuka nikaweka katafiti changu nikatenga kisu maalumu kwa ajili yakukatia vitunguu maji nililobaini nikua kisu cha vitunguu kiliwai kuisha makali haraka sana kiasi kwamba hata stake ya nyama haikati kabisa
Nikasema yanini kuumiza ubongo wangu akati kuna jukwaa lakuweza kunipatia majibu yangu
Je, ni mechanism gani kitunguu inafanya mpaka kisu kiishe makali haraka ivyo?
Je, kitunguu maji pia kina chemical gani izo mpaka tulie?
Je, kuna dawa yakuzuia kutoka machozi ukiwa unakata vitunguu maji?
Msaada wenu wakuu majibu ya hovyo kwa watu wa hovyo yanaruhusiwa pia