Kwanini klabu ya Simba iandae mechi ya kirafiki timu ya Taifa ikicheza?

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,703
Reaction score
1,724
Wakuu, nimetatizwa na uamuzi wa uongozi wa klabu ya Simba kuandaa mechi ya kirafiki na timu ya AFC Leopards tena ikichezwa hapa nchini wakati timu yetu ya Taifa ikicheza katika mashindano na timu ya taifa ya Uganda.
Najiuliza hivi wachezaji wao wangechaguliwa kuchezea timu yetu ya Taifa mechi hii ingekuwepo?
Huu ni mzaha mkubwa.
 
Mechi ya simba ni mechi ya kirafiki ni kama zoezi tu,mbona Manula yupo kwenye timu ya taifa,kwani yanga mlikatazwa?wachezaji wa simba waliocheza Leo ni wale hawakuitwa taifa stars au wale walioachwa,kama nye yanga ni wazembe hamwezi kuita mechi ya kirafiki msitusumbue ndo maana mmebaki maskini timu ombaomba maana hamjitumi
 
Timu ya Simba ni mambumbumbu... Hawajali utaifa kabisa
Ulitaka wajali vp utaifa? Taifa staz imecheza saa 10 na Simba saa 1 usiku. Shida ipo wapi hapo?! Punguza kulalamika na chuki za kike kwa Simba mkuu..! Unalalamika sana utasema nyumba ndogo
 
Ulitaka wajali vp utaifa? Taifa staz imecheza saa 10 na Simba saa 1 usiku. Shida ipo wapi hapo?! Punguza kulalamika na chuki za kike kwa Simba mkuu..! Unalalamika sana utasema nyumba ndogo
Jibu hoja au hujaielewa.....wachezaji wa Simba wangechaguliwa ktk Timu ya Taifa hii mechi ya saa moja ingekuwepo!? Ndipo mtoa hoja anapotatizwa....?
 
Ulitaka wajali vp utaifa? Taifa staz imecheza saa 10 na Simba saa 1 usiku. Shida ipo wapi hapo?! Punguza kulalamika na chuki za kike kwa Simba mkuu..! Unalalamika sana utasema nyumba ndogo
Huwa siwezagi kuongea na mtu kwa kauli chafu chafu kama zako....

Jifunzeni nidhamu ninyi mashabiki pamoja na wachezaji wenu... Na viongozi wenu wa timu
 
Jibu hoja au hujaielewa.....wachezaji wa Simba wangechaguliwa ktk Timu ya Taifa hii mechi ya saa moja ingekuwepo!? Ndipo mtoa hoja anapotatizwa....?
Kwani ni timu ina wachezaji wangapi? Taifa Staz waliita 6 tu ina maana kukosekana hao Simba isingecheza mechi ya kirafiki?
Wakosoeni wachezaji wa Simba kwa kukosa nidhamu,lakini msiipangie timu kitu cha kufanya wakati kulikuwa na utofauti wa masaa baina ya mechi ya Simba na Timu ya Taifa.
 
Huwa siwezagi kuongea na mtu kwa kauli chafu chafu kama zako....

Jifunzeni nidhamu ninyi mashabiki pamoja na wachezaji wenu... Na viongozi wenu wa timu
Unajibiwa kulingana na mtazamo wako. Unamtazamo hasi dhidi ya Simba na mechi yao ya leo.
AFC Leopards leo wamecheza na Simba na wakati huohuo Kenya imecheza,umesikia wapi Wakenya wakilalamika dhidi ya mchezo wa leo? Jibu ni moja tu,hawana mtazamo hasi na akili finyu kama za kwako.
 
Ulitaka wajali vp utaifa? Taifa staz imecheza saa 10 na Simba saa 1 usiku. Shida ipo wapi hapo?! Punguza kulalamika na chuki za kike kwa Simba mkuu..! Unalalamika sana utasema nyumba ndogo
Ushawahi kuona barca inacheza wakati team ya taifa inacheza?
 
Ushawahi kuona barca inacheza wakati team ya taifa inacheza?
Inashindikana nini? Kila kitu kinakwenda na ratiba na mahitaji ya mwalimu. Timu haijacheza mechi kwa zaidi ya wiki sasa na wiki ijayo ligi inaendelea. Ni muhimu kwa mwalimu kupata mchezo wa kirafiki ili awaweke sawa kisaikolojia wachezaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…