Kwanini kocha wa Morocco alienda kumuingilia Mbemba alipokuwa anasali?

Kwanini kocha wa Morocco alienda kumuingilia Mbemba alipokuwa anasali?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
7,895
Reaction score
12,975
Kwa wale wafuatiliaji wa AFCON watakuwa wanajua tukio lililotokea katika mechi ya Morocco vs DRC na gumzo ambalo limekuwa linaendelea kuhusu vurugu zilizofuata.

Mengi yanasemwa nini kilitokea ila mimi ambaye niliangalia mechi ile live kitu cha kwanza nilichoona ambacho hakikunipendeza ni kitendo cha Kocha wa Morocco kwenda kwa Captain wa DRC, Chancel Mbemba na kulazimisha mazungumzo wakati Mbemba anasali.

IMG-20240127-WA0001.jpg


Kile kitendo cha kumpa mkono Mbemba kilikuwa ni cha kinafki maana alijua camera zingenasa kinachoonekana na siyo kinachosikika na bahati mbaya zaidi clip zote zinazosambaa zimekata hiki ninachokisema.

Najua kuna matukio yalitokea kabla ya pale yaliyochochea zaidi ila kile kitu sikukipenda kabisa maana kutoheshimu moment ya mtu akiongea na muumba wake ni dharau kubwa sana.

 
Hawa morocco ni mujahedeen inawezekana madude Yao yalifeli na mahesabu yakaharibika ikamkasirisha kocha ndiyo maana akamfuata Bemba akisali.

Maana hakuna sababu nyingine yenye mashiko ya kuleta vurugu .
 
Kwa wale wafuatiliaji wa AFCON watakuwa wanajua tukio lililotokea katika mechi ya Morocco vs DRC na gumzo ambalo limekuwa linaendelea kuhusu vurugu zilizofuata...
Kwani huyo kocha Mbemba alifuatwa kanisani/msikitini? Kocha wa Morocco angejuaje kuwa Mbemba alikuwa anasali? Usipende kuexaggerate vitu usivyovijua undani wake.
 
👇🏿
 

Attachments

  • E24F77B6-6CDF-42B6-B87C-8CCC7B52C85F.jpeg
    E24F77B6-6CDF-42B6-B87C-8CCC7B52C85F.jpeg
    1.5 MB · Views: 4
Inawezekana anacholalamikia kinahusiana na nilichosema hapa ukijumlisha na maneno anayosema alitamkiwa.

Nisingependa kuleta mijadala wa mambo ya kidini ila siku hizi nimeona trend kwenye mipira hata ya Tanzania ya watu wa imani fulani kuona kama wao ndiyo wako peke yao au kwamba watu wa imani nyingine hawana maana. Hili ni jambo baya na la hatari sana huko mbele tunapokwenda. Msinishambulie, mimi ni mleta ujumbe tu.
 
Naona wamemuondolea adhabu kocha wa Morocco Regragui ili watakapopata kichapo kutoka kwa ndugu zake Patrice Motsepe wasijesema aliwafanyia hujma.

Ila wamshukuru sana Mbemba kwa kuwasitiri, hili jambo lingekuwa kubwa na wangehitaji kuja kutumia nguvu kubwa sana kujisafisha.

IMG-20240127-WA0001.jpg
 
Morocco wamekutwa hawana hatia, ila kuna wabongo bado wanaendelea kuteseka tu
 
Kwa wale wafuatiliaji wa AFCON watakuwa wanajua tukio lililotokea katika mechi ya Morocco vs DRC na gumzo ambalo limekuwa linaendelea kuhusu vurugu zilizofuata...

Acheni kulalamika na kuzisemea timu za watu bwana

Morocco the best team in Afrika, so acheni kulalamika.
 
Hao wa morocco wabaguzi hata comments tu zinaonesha wanawachukia wacongo sana sijui kwanini
 
Back
Top Bottom