Kwanini kocha wa SIMBA anakua mzito kumuingiza Medie Kagere

Kwanini kocha wa SIMBA anakua mzito kumuingiza Medie Kagere

Kwa mtazamo wangu mimi alimuacha Boko kwa sababu Kagere si mkabaji ili kulinda goli letu la ugenini. Halafu Boko ana mchango mwingine katika kutoa assits ambapo Kagera si mzuri sana kwenye assists.
Muzamiru hakutoka naye kwa sababu hiyo hiyo ya kuboresha ulinzi na Muzamiru ana uwezo wa kuwa active dakika zote tisini na husaidia katika mashambulizi laukama siku hiyo hakuwa katika ubora wake.
Sub ya Morrison ilichangamsha game kwa namna fulani laukama mizaha yake kidogo tu isababishe goli.
Kwa hiyo basi basi, kama hakuna pressure ya kimchezo kiufundi, Kagere ni chaguo letu sisi wana Simba kama tunataka kupata matokeo ya haraka na ma-winger wawe Morrison na Miqueson.
Kwa hiyo basi, mimi simlaumu kocha kwa sababu lengo la kwanza kabisa lilikuwa ni kulinda ushindi na kwa hilo alifanikiwa. Mechi ijayo anaweza kufanya hivyo wapenzi wa Simba wanavyotaka kwani pressure siyo kubwa kivile. Ila tu asiache kumtumia Nyoni kama kiungo mkabaji katika kipindi ambapo Utopolo wako mbele na katika michezo ya kimataifa.
 
Back
Top Bottom