Kwanini kocha wa Simba SC (Benchikha) anasikilizwa sana kuliko makocha wengine waliopita Msimbazi?

Mnachokozaga mkitukanwa mnaanza kulia lia

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna sehemu nimekutaja hapo? Au wewe ndiye Mangungu? Maana huyo pekee ndiye niliyemtaja.

Halafu siyo kwamba siwezi kujibu mashambulizi ya hayo matusi yenu. Ni vile tu ninajitahidi kuilinda heshima yangu, kutokana na ukweli kwamba wengi wenu humu mnaopenda kutukana watu hovyo; ni watoto wa miaka ya 1990's na 2000's.
 
Profile ya Benchika ni kubwa kuliko za makocha wengine WOTE waliopita. Benchika atawaambia kua alipotoka alifanikiwa sababu ya mambo kadhaa ikiwemo kutoingiliwa uwanjani na kusikilizwa.

So Simba wakitaka kua nae na wafanikiwe nae basi moja ya masharti yake ni hayo.
 
Alitoa tahadhari kua yeye hapangiwi na wakimtaka afanye vzr baasi wampe uhuru kiufupi anaogopeka, angekua Roberto mda tu mngeshatukanwa sana.
 
Sijaona kosa uongozi kumsikiliza kocha wao.
 
Mwaka ambao niliingia kidato cha kwanza Kuna kitabu cha English kilikuwa kinaitwa "We Learn Through Mistakes" Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba 'Tunajifunza kutokana na Makosa' na Wahenga wanasema "Kufanya kosa si kosa Bali Kurudia Kosa ni Kosa" Kwa maana iyo Viongozi wa Simba wameshajifunza kwamba kumuingilia kocha kwenye
majukumu yake ni Makosa. Kwa iyo Kwa makocha waliopita hawakujua kama ni makosa Bali Sasa wamejifunza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…