Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Leo tarehe 10/10 ni siku ya Afya ya akili duniani. Moja ya sababu kubwa ya watu kujiua ni matatizo ya Afya ya akili. Na mgonjwa wa akili hatendi kosa zaidi ni anahitaji msaada wa matibabu.
Sasa nini kilipelekea Tanzania kuunda sheria kuwa kujiua(Kujaribu kujiua) ni kosa kisheria?
Hii sheria ina shida mbili.
Kwanza inamfanya anayejiua ahakikishe anakufa kabisa. Maana akipona atashtakiwa.
Pili inamfanya anayesakamwa na mawazo ya kujiua ashindwe kuomba msaada. Maana tayari anachowaza kimeshanyanyapaliwa kuwa ni kosa kisheria.
Nafikiri kuna haja ya kubadili hiyo sheria na pia kuna haja ya mamlaka husika kutoa msaada kwa wenye mawazo ya kujiua, kama kuanzisha namba ya msaada.