Kwanini kuna malalamiko TARURA?

Kwanini kuna malalamiko TARURA?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
948
Reaction score
1,627
Juzi kupitia taarifa ya habari ya usiku Meneja wa TARURA Wilaya ya Urambo alipoulizwa na Baraza la Madiwani kuhusu hali mbaya ya barabara katika Wilaya hiyo bila kuogopa alitamka wazi kuwa ni muda mrefu umepita Wilaya yake haijapokea fedha toka Serikalini.

Siyo tu kwa wilaya ya Urambo bali karibu nchi nzima wanapitia tatizo hili. Juzi kwenye kikao cha Bunge la Jamhuri kule Dodoma, Mbunge wa Singida Mashariki wakati akichangia kwenye mjadala alisema kuwa Wakandarasi wengi hawajalipwa madai yao licha ya kuwasilisha certificate kwa mamlaka husika kwa ajili ya malipo.

Tunajiuliza kunanini na kwanini wakandarasi hawalipwi madai yao ili waendelee na kazi?. Hii ni tofauti kabisa na awamu ya tano pale mkandarasi alipomaliza kazi yake na kuwasilisha cerificate na kukaguliwa alikuwa analipwa mara moja.
 
Pesa Hakuna. Madiwani kazi wanayo waombe serikali ipeleke pesa TARURA Otherwise wasitumie miradi ya Barabara kujinadi mwaka huu😀😀.
 
Sasa kama Idara na Taasisi za Serikali hazipelekewi fedha za miradi ya maendeleo, watawezaje kuitekeleza?

Sio TARURA tu, nenda Tanroads pia RUWASA hali zao ni hivyo hivyo

Huu ni Mwaka wa Uchaguzi, fedha za Serikali zinaelekezwa nyingi huko
 
Back
Top Bottom