Kwanini kuna Watanzania wamechukia timu ya Taifa Lao kufuzu AFCON 2023?

Naomba msaada wa ufafanuzi toka Kwa Watanzania wenzangu. Tangu Jana majira ya saa 6:10 usiku kuna Watanzania wameanzisha nyuzi humu JF na mitandao mingine kuonyesha jinsi walivyo na kinyongo Kwa timu ya Taifa kutoa Sare na Algeria na hivyo kufuzu Fainali za AFCON.
NINI kiko nyuma ya chuki na makasiriko haya maana si kawaida Mtoto wa Mtu kufaulu mtihani halafu mzazi wake akanuna. Huwa nasikia kuna wazazi wanachukia watoto wao kufaulu pale wanapokuwa wamepanga kuwaozesha au kama ni wa kiume kuwatumia kuchunga mifugo. Lakini pia wazazi wengine huwa wanachukia sababu ya kuwa na uwezo mdogo kiuchumi.
Sasa hii Hali ya baadhi ya mashabiki àmbao hawachangii hata 100/= kugharamia timu kuchukia mafanikio ya timu ya Taifa Lao inatokana na Nini?
Hao waliochukia ni WAJINGA. Kwenye mpira sio Kila shabiki anaujua mpira. Wengine wamo kwasababu wengine wamo.
 
Watanzania wenye chuki na mama Samia kila jema kwenye utawala wake kwao ni baya.

Waleeee.
 
Hatujafurahi sababu huko tuendako tunaenda kutia aibu taifa.
 
Wakamalia wa beting
Screenshot_20230908-182708_1.jpg
 
Wameninyima milioni nne kwa kutofungwa kwao
 
Naomba msaada wa ufafanuzi toka Kwa Watanzania wenzangu. Tangu Jana majira ya saa 6:10 usiku kuna Watanzania wameanzisha nyuzi humu JF na mitandao mingine kuonyesha jinsi walivyo na kinyongo Kwa timu ya Taifa kutoa Sare na Algeria na hivyo kufuzu Fainali za AFCON.
NINI kiko nyuma ya chuki na makasiriko haya maana si kawaida Mtoto wa Mtu kufaulu mtihani halafu mzazi wake akanuna. Huwa nasikia kuna wazazi wanachukia watoto wao kufaulu pale wanapokuwa wamepanga kuwaozesha au kama ni wa kiume kuwatumia kuchunga mifugo. Lakini pia wazazi wengine huwa wanachukia sababu ya kuwa na uwezo mdogo kiuchumi.
Sasa hii Hali ya baadhi ya mashabiki àmbao hawachangii hata 100/= kugharamia timu kuchukia mafanikio ya timu ya Taifa Lao inatokana na Nini?
U Simba na U Yanga ni sumu! ingawa bado kuna watu wanaona ni sahihi kuendelea kuukumbatia kwa sabab za kisiasa.

Hawa S & Y walitumika enzi hizo, mbinu zao zimeshapitwa na wakati, turuhusu wawekezaji wafanye maendeleo kwenye soka, ajira zitaongezeka na soka litachangamsha Nchi na kikua zaidi

Wachache wataelewa andiko langu.
 
Lazima wachukie wamekosa stori za kubishania,,,kukandia na kukosoa kwenye vijiwe Vyao maana ndio hulka za wabongo huwaga wanasubiri makosa au ukosee tuu waanze mashambulizi na ujuaji wa hovyohovyo tuu!!
 
Back
Top Bottom