Chachasteven
JF-Expert Member
- Jul 4, 2014
- 1,941
- 2,044
Haya, salaam wandugu,
Nilikimbia Commerce na Book keeping lakini kidogo nina nadharia kuhusu biashara ingawa ninaweza nisiwe accurate sana kwa hivyo mtanisahihisha ambapo nitakosea.
Nimeandika huu uzi kutokana na ishu ya CMG na Tigo kushusha bei za tiketi za tamasha lao la fiesta. Tunajifunza nini kama wafanyabiashara kwenye hili? Ni mbinu nzuri?
Biashara, iwe kubwa au ndogo, zina mambo mengi. Na kuna wakati unahitaji mbinu sahihi ili kukabiliana na hayo mambo mengi. Moja ya mbinu muhimu ya kibiashara ni upangaji wa bei - Na hapa mara nyingi inategemeana na ushindani na mazingira
Hapa wafanyabiashara wengi wanadhani njia nzuri ya kuwahifadhi/kuwabakiza wateja wao na kuongeza mauzo ya bidhaa zao ni kupunguza bei za bidhaa zao, pia wengi wanafanya hivyo wakiamini wataondoa upinzani na kuongeza mauzo. Hata hivyo ukweli ni kinyume chake
Licha ya uwepo wa faida katika hili bado mzani wa uzito ni mkubwa kwenye hasara katika kupunguza bei ya bidhaa zako kama mfanyabiashara.
Tuanze na hasara chache ambazo zipo wazi wazi, mfano wa kwanza:
Kwenye hilo jedwali, utaona bei ya kuuza ilikuwa 100 lakini ikakatwa kwa 10% ikawa 90. Utaona faida zako zitapungua kwa asilimia 50% ukilinganisha na kama ungeuza kwa bei ya 100 na hapo ukumbuke tumepunguza asilimia 10% tu.
Ni hasara tayari ila inayoonekana kama faida ila kwa kuwa tunakuwa na hisia kuwa tutauza zaidi endapo tutashusha bei, acha tuone mfano wa pili ukiwa na mauzo mengi zaidi kwa bidhaa iliyoshushwa bei.
Kama unavyoona, tumeuza bidhaa 60 - yaani 10 zaidi kulinganisha na jedwali la kwanza. Utaona faida yetu imeongezeka na kufikia 600 lakini bado haijafikia ile faida iliyopo kwenye kuuza bila kushusha bei. Kwa hivyo ili upate faida ambayo italingana na ile ya bidhaa ambazo hazijashushwa bei itahitaji uuze bidhaa 100 ambapo kimsingi ni hasara iliyojifunika kwa sura ya faida. Binafsi, siamini kama itakuwa rahisi kuziba pengo la hasara hio kwa urahisi kwa kutumia njia ya kushusha bei za bidhaa.
Mbali na hapo pia, utakapopunguza bei ya bidhaa zako ujue utapunguza na heshima ya bidhaa zako waliyokuwa nayo wateja wako. Hii inamaanisha wateja watadhani umeshusha bei ya bidhaa zako kwa kuwa zina ubora kidogo sana.
Kwa sababu hizo chache nilizotaja kati ya nyingine nyingi utaona ni kwa kiasi gani ambavyo kushusha bei ya bidhaa zako itakuwa na hasara kubwa sana kwenye biashara yako has kipindi cha anguko la uchumi au ushindani!
Zipo njia nyingi nzuri za kubakisha wateja wako na kushinda ushindani bila kupunguza bei ya bidhaa zako. Hadi hapo nitakapopata kalamu na karatasi nitarudi tena.
Levoz beibee.
Nilikimbia Commerce na Book keeping lakini kidogo nina nadharia kuhusu biashara ingawa ninaweza nisiwe accurate sana kwa hivyo mtanisahihisha ambapo nitakosea.
Nimeandika huu uzi kutokana na ishu ya CMG na Tigo kushusha bei za tiketi za tamasha lao la fiesta. Tunajifunza nini kama wafanyabiashara kwenye hili? Ni mbinu nzuri?
Biashara, iwe kubwa au ndogo, zina mambo mengi. Na kuna wakati unahitaji mbinu sahihi ili kukabiliana na hayo mambo mengi. Moja ya mbinu muhimu ya kibiashara ni upangaji wa bei - Na hapa mara nyingi inategemeana na ushindani na mazingira
Hapa wafanyabiashara wengi wanadhani njia nzuri ya kuwahifadhi/kuwabakiza wateja wao na kuongeza mauzo ya bidhaa zao ni kupunguza bei za bidhaa zao, pia wengi wanafanya hivyo wakiamini wataondoa upinzani na kuongeza mauzo. Hata hivyo ukweli ni kinyume chake
Licha ya uwepo wa faida katika hili bado mzani wa uzito ni mkubwa kwenye hasara katika kupunguza bei ya bidhaa zako kama mfanyabiashara.
Tuanze na hasara chache ambazo zipo wazi wazi, mfano wa kwanza:
Bei | 100 | 90 |
Gharama za kununua | 80 | 80 |
Idadi ya bidhaa zilizouzwa | 50 | 50 |
Mapato | 5,000 | 4,500 |
Faida | 1,000 | 500 |
Ni hasara tayari ila inayoonekana kama faida ila kwa kuwa tunakuwa na hisia kuwa tutauza zaidi endapo tutashusha bei, acha tuone mfano wa pili ukiwa na mauzo mengi zaidi kwa bidhaa iliyoshushwa bei.
Bei | 100 | 90 |
Gharama za kununua | 80 | 80 |
Idadi ya bidhaa zilizouzwa | 50 | 60 |
Mapato | 5,000 | 5,400 |
Faida | 1,000 | 600 |