Kashishi yetu
JF-Expert Member
- Mar 22, 2014
- 3,509
- 3,741
UMUOFIA KWENU WAUNGWANA!
Kwanza niwapongeze waliopata ajira nasema Hongereni! Na mliokosa ajira poleni sana lakini tambueni kuwa Mungu yupo pamoja na nyinyi!! MSIKATE TAMAA.
WITO WANGU KWA SERIKALI ,Nafasi nyingi zimehamishiwa Halmashauri ambapo watu wanaomba moja kwa moja. Kumejitokeza changamoto zifuatazo ambazo Serikali inabidi izitatue ili kuleta ahueni kwa waombaji wa ajira:
Mosi, KUCERTIFY VYETI, Sioni umuhimu wake zaidi ya kuwaongezea gharama waombaji wa ajira.Kumbuka mtu akituma maombi ya ajira katika Sehemu tofauti tofauti labda sehemu kumi na tano atawezaje kumudu gharama hizo za kwenda kucertify vyeti katika hatua ya awali tu tena bado hajafanikiwa?
Unamwambia mtu Acertify vyeti anaenda kulipa. Kwa wakili labda elfu 20000 bado hajatoa kopi ya vyeti vyake na mtu huyu hana Ajira wengine hawana hata wazazi wanajihangaikia wao wenyewe sasa wanapataje hizo pesa ili hali hawana ajira?
Haya amecertify vyeti vyake na bado kakosa ajira Serikali haioni kuwa inazidi kuwadidimiza Kiuchumi na kuwaongezea machungu hawa waombaji wa ajira?
Halafu hata akipata ajira bado tena vyeti vyake mtavihakiki kwa kuvipeleka baraza la mitihani kuhakikiwa tena!!!Sasa kunahaja gani ya kucertify kabla hajaajiliwa?
Maoni yangu suala la kucertify vyeti Serikali iachane nalo katika hatua za Awali za waombaji bali litakapokuwa limefikia hatua ya watu kuajiriwa basi ñdo wacertify vyeti vyao na Serikali ifanye yenyewe kwa kumtumia mwanasheria wao wa halmashauri ambapo waombaji wa ajira wanaweza kulipia 5000 na pesa hiyo ikaingia serikalini na asilimia kidogo akapewa mwanasheria wa halmashauri kama posho yake kuliko kuwaachia wanasheria wa mitaani ambapo wanawakamua pesa. Nyingi.
Kwa hiyo kama kuna ulazima wa kucertfy vyeti kabla ya kuajiliwa, basi Hatua ya awali waombaji waombe bila kucertify vyeti, Hatua ya mtihani wa pili ambao ni wa oral Ndipo waombaji waliobahatika kuingia hatua hiyo wanaenda na hela kidogo ya kucertify vyeti vyao kwa mwanasheria wa halmashauri labda elfu mbili au elfu tano kiwango kisiwe kikubwa sana kumbuka waombaji wengi wao wanatoka katika mazingira magumu ya kipesa hivyo ukiweka kiasi kikubwa watashindwa na kiasi hicho kiwe flate late kwa nchi nzima.
Vinginevyo Serikali isubiri watu waajiliwe kabla ya muombaji kusaini mkataba wa ajira serikali ifanye uhakiki yenyewe kwa gharama zake.
TATU, MAOMBI YAAMBATANE NA PICHA MBILI, TATU, MOJA N.K. Hii nayo ni kumuongezea maumivu maombaji!
Muombaji anatuma sehemu tofauti tofauti labda sehemu kumi na tano,Sasa piga hesabu kila sehemu wakahitaji paspoti size mbili, Hapo lazima uwe na paspoti size 30 !!! Paspoti size kupiga ni sh. 4000-5000 na huwa zinatoka 6. Ili upate picha 30 maana yake urudiwe kupiga mara tano. Zidisha 5000* 5 =. 25,000/= Na bado mtu huyu hana uhakika wa ajira yenyewe. Na bado mtu huyu amecertify vyeti vyake. Na bado nauri za kwenda kwenye interview, bado hajapata guest ya kulala na bado hajala na zaidi ya yote wengine hawana baba wala mama!!!! Serikali iliangalie hili linawaumiza sana waombaji wa ajira.
MAONI YANGU,PICHA WAPELEKE PALE WANAPOFIKIA HATUA YA KUSAINI MKATABA NA ZAIDI YA YOTE VYETI SIKU HIZI VINAPICHA.
TATU, TAREHE NA VITUO VYA KUFANYIA USAILI VIANZISHWE. Muombaji ajira kaomba ajira Newala labda na masasi na kote kote alitumia gharama kutuma maombi yake.
Halmashauri hizi zinafanya kwa makusudi Mazima kuweka tarehe ya usaili siku moja!!! Muombaji huyu anajikuta sehemu moja hatofanya mtihani kwa sababu ya kutakiwa kote awepo licha ya yeye kugharamikia kutuma maombi lakini tarehe zimepangwa siku moja za usaili. Hili nalo ni kuwaongezea mzigo usio wa lazima.
MAONI YANGU. Matangazo yanayotolewa ya ajira basi yataje na tarehe ya usaili ili huyu muombaji kabla hajatuma maombi yake ajue kuwa tarehe fulani atahitajika kwenye usaili halmashauri fulani. Hili litasaidia yeye kutumia pesa yake kihalali kuliko kutuma maombi halafu unakuta tarehe zimegongana.
.
PIA, Serikali ifikirie kuanzisha matawi ya usaili kwa nafasi zote kwa kila wilaya. Mfano: Nafasi za kazi labda za Ruangwa.Wale walioomba nafasi za Ruangwa interview zao zifanyike kila mkoa badala ya watu kusafiri kwenda Ruangwa wakitokea Dodoma ili kuwapunguzia gharama za malazi, nauli ukizingatia zimepanda bei na chakula.
Serikali iweke mawakala katika kila mkoa au wilaya wakuendesha hizo Saili zao.
NNNE, KIPENGELE CHA KUFANYA KAZI KWA KUJITOLEA KAMA KIPAUMBELE CHA KUAJILIWA KIONDOLEWE, Hiki hakina maana yoyote ile zaidi ya kuwabinya ambao wapo mbali na maeneo hayo ya kujitolea,Nafasi zenyewe chache labda zipo sita sasa wote watapata hizo nafasi za kujitolea? Je, wale watakaokosa ndo mnawatrete kuwa siyo wazalendo? Ndomaana kwenye kuajiriwa wanapewa kipaumbele wale waliokuwa wanajitolea kuliko wale ambao hawakuwa wanajitolea kwasababu mbali mbali wengine makazi yao yapo mbali na mji wanashindwa kumudu gharama za nauli mnawatupa nje ya kapu la ushindani kwa kigezo siyo wazalendo!!!
MAONI YANGU, hiki kipengele kifutwe na iwe mwiko mtu kujifanya anajitolea, kwani huko ni kujitengenezea himaya ya Rushwa na kujuana. Ajira zikitoka hakutakuwa na ushindani wa haki. Hivyo naomba Serikali iliangalie upya hili suala.
TANO, WAKATI WA USAILI MUDA UZINGATIWE,CASE STUDY NEWALA. Kuna Mhanga wa aLiniambia kuwa waombaji waliingizwa ukumbini saa moja asubuhi wakaambiwa hakuna mtu kutoka Wamekaa humo bila hata kuruhusiwa kwenda kunywa chai si kwamba walikuwa wanafanya mtihani hapana wamekalishwa tu!!! Ilipofika saa nane na dakika zake wakapewa karatasi za kujibia mtihani wakakaa tena zaidi ya lisaa lizima Jingine bila kupewa Mtihani!!! Ilipofika saa tisa wakapewa mtihani kwahiyo WalikalIshwa ukumbini tangu saa moja hadi saa tisa bila kula halafu wakaingia kwenye mtihani bila kula.
Huku nako ni kuwaongezea maumivu na gharama za kulala gesti bila sababu za msingi! Kulikuwa na sababu gani za kuwaingiza saa moja halafu mtihani unakuja kugawa saa tisa mchana? Haya majibu yamekuja kutolewa usiku wa saa tano kasorobo!.Kumbe wangeanzisha mtihani saa mbili kamili asubuhi majibu yangeweza kutoka saa nane mchana na hivyo waombaji wangekwepa kulipia gharama za kulala gesti kwa siku hiyo!.
WITO WANGU, Serikali iwaagize Wakurugenzi wote kuzingatia muda wa kunzisha mitihani na majibu watoe mapema ili waombaji wajijue kama wamepita au hawajapita ili wale ambao hawakufanikiwa waanze kuondoka mapema wakabidhi vyumba vya gesti kwa wahusika ili wasichajiwe tena gharama ya kulala.Tuwaonee huruma hawa waombaji wengine hawana wazazi na wengine ndio wanaotegemewa na wazazi wao au wadogo zao.
SITA, MADAI YA KUWEPO KWA RUSHWA, UPENDELEO. Hili ni tetesi japo sina hakika nalo lakini lisemwalo huenda lipo kama halipo basi laja.
MAONI YANGU, vyombo vya ulinzi na usalama vihusike kwenye mchakato wote wa ajira.
Kwa nilowakwaza wanisamehe sana,Halikuwa lengo langu kuwakwaza.
Naomba Kuwasilisha.