Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,689
- 5,497
Kipindi cha nyuma, simu za Iphone zilikuwa ni za moto katika bei, kuipata lazima upate connections na wanaofanya kazi kwa wadosi ili uuziwe kwa bei nafuu, ilikuwa ni simu inayouzwa kwa bei kubwa, kulinganisha na Android. Ila kwasasa flagship za android ndizo zimekuwa zinauzwa bei kubwa mno kuliko Iphone. Flagship ya Samsung, Oppo, Huawei, Vivo, Xiaomi, n.k. flagships zao za mwaka 2022 mpaka 2024 japokuwa ni za zamani lakini sokoni pamoja na kuuzwa kama simu za second hand, lakini bei zake bado zipo juu. Wakati ukiwa na 700,000/= unapata Iphone flagships ambayo imenyooka kabisa. Je hii imetokana na nini?
N.B
Android flagship sijazungumzia Tecno, Infinix, itel, na wafananao
N.B
Android flagship sijazungumzia Tecno, Infinix, itel, na wafananao