Kwanini kwasasa flagship za android smartphones imekuwa bei ya juu kuliko flagship za Iphone?

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,689
Reaction score
5,497
Kipindi cha nyuma, simu za Iphone zilikuwa ni za moto katika bei, kuipata lazima upate connections na wanaofanya kazi kwa wadosi ili uuziwe kwa bei nafuu, ilikuwa ni simu inayouzwa kwa bei kubwa, kulinganisha na Android. Ila kwasasa flagship za android ndizo zimekuwa zinauzwa bei kubwa mno kuliko Iphone. Flagship ya Samsung, Oppo, Huawei, Vivo, Xiaomi, n.k. flagships zao za mwaka 2022 mpaka 2024 japokuwa ni za zamani lakini sokoni pamoja na kuuzwa kama simu za second hand, lakini bei zake bado zipo juu. Wakati ukiwa na 700,000/= unapata Iphone flagships ambayo imenyooka kabisa. Je hii imetokana na nini?

N.B
Android flagship sijazungumzia Tecno, Infinix, itel, na wafananao
 
Una masihara wewe, flagship za android bei hufa mapema sana kwenye Used market kuliko Iphone.
 
Sababu Apple ana mkataba mrefu wa ram na storage, anapata ram bei nafuu.

Sasa hivi ram ndio kifaa ghali zaidi kwenye computer, hadi asilimia 60 ya BOM ni ram na storage, mwenye ram za bei rahisi ndio anakamata soko.

Wote Samsung na Apple watakamata soko wakati huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…