Passport ni aina mojawapo ya utambulisho hasa unapotaka kufanya mambo ya kimataifa. Hata baadhi ya scholarships, kozi fupifupi, kazi za nje ya nchi nk unapo apply wanataka uweke passport yako. Kumbuka wakati unapo apply scholarship au kazi, bado unakua hujapata mwaliko wa kwenda kwenye nchi husika lakini wanataka passport. Sasa hua nawashangaa uhamiaji wanapodai utoe ushahidi wa safari wakati hiyo passport ndio unaihitaji ili upate hiyo safari!
Cha kufurahisha ni kuwa watu wote pale uhamiaji wanajua kwamba zile sababu tunazojaza wakati wa kuomba pasi hua ni za uongo na wala hawana shida na hilo😁. Hii ndio Tz bwana..