Kwanini kwenye kubadili Passport hakuna foleni kama NIDA licha ya kesho kuwa siku ya mwisho?

Hivi nchi nyingine unachukua pass kama nyanya?? Hawaulizi vidhibitisho na ushahidi wa uendako?
Nchi nyingi hawaulizi huo ujinga yaani mtu ana miaka zaidi ya 35 wewe unamuuliza ati unataka kwenda wapi na hii passport tunayokupatia
 
Gharama ni ya kawaida sana ila tatizo masharti rundo
 
Mi naona nchi yetu inafanya baadhi ya maamuzi bila kufikiri kwa kina... Mwakyembe alikuja na la vyeti vya kuzaliwa na ndoa... ndani ya masaa 24 Rais akatengua..!!! Tena kwa maneno ya kwamba inawezekana hata Mwakyembe hana hicho cheti...
 
Unataka pasi ya kusafiria wakati huna mpango wa kusafiri?

Sent using Jamii Forums mobile app
mipango ipo ila unanilazimisha niseme naenda wapi leo wakati ni mkakati wangu wa Muda mrefu kwenda mahala mbalimbali.

Ni sawa na kuniambia nikutajie jina la mke wangu kabla hata ya kupata mchumba.
Kutokuwa na uwezo wa kutaja haimaanishi sitaoa.
 
mipango ipo ila unanilazimisha niseme naenda wapi leo wakati ni mkakati wangu wa Muda mrefu kwenda mahala mbalimbali.

Ni sawa na kuniambia nikutajie jina la mke wangu kabla hata ya kupata mchumba.
Kutokuwa na uwezo wa kutaja haimaanishi sitaoa.
Passport ni aina mojawapo ya utambulisho hasa unapotaka kufanya mambo ya kimataifa. Hata baadhi ya scholarships, kozi fupifupi, kazi za nje ya nchi nk unapo apply wanataka uweke passport yako. Kumbuka wakati unapo apply scholarship au kazi, bado unakua hujapata mwaliko wa kwenda kwenye nchi husika lakini wanataka passport. Sasa hua nawashangaa uhamiaji wanapodai utoe ushahidi wa safari wakati hiyo passport ndio unaihitaji ili upate hiyo safari!
Cha kufurahisha ni kuwa watu wote pale uhamiaji wanajua kwamba zile sababu tunazojaza wakati wa kuomba pasi hua ni za uongo na wala hawana shida na hilo😁. Hii ndio Tz bwana..
 
Wengi wameshazamia mkuu hawana Muda na passport yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani achemi uzushi. Passport ukiwa na NIN au NID card,cheti cha kuzaliwa chako, cheti cha kuzaliwa mzazi au affidavit unapata ndani ya wiki mbili. Huku mitandaoni tumezoea kukuza vitu sana.

Halafu kuulizwa unaenda wapi haijaanza leo, na mbona watu wanapata passport? Mimi niliwaambia humu kwenye thread kama hii ukiulizwa safari wapi na lengo nini waambie safari ni SA au Dubai lengi matembezi kwahio hamna mualiko wala nini nchi hizi hatuhitaji Visa.

NB: Mimi niliipata passport siku saba tu.
 
@PRONDO

UFAFANUZI HAPA MKUU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…