QasraNet
Member
- Jan 3, 2018
- 39
- 57
Picha tunayoitumia kwenye vitabu haionyeshi uhalisia wa hali ya waafrika miaka hiyo ya 1905. Yaani hii picha haikufaa kabisa kuendelea kutumika. Hiyo ni picha ya kuchorwa na mkono. Picha inamuonyesha Kinjeketile kama Mtu mwenye kitambi/kiribatumbo, yupo tumbo wazi, anamduara ule kichwani, anacheni hiyo shingoni, na yule jamaa pale chini ana liuvimbe usoni. Hii picha yaani haifai kabisa, wazungu waliitengeneza kuendelea kutudidimiza kwa miaka na miaka.
Sasa ukifanya Google search ndogo tuu, unaletewa picha halisi zilizopigwa wakati huo. Yaani hatukuwa wakaa uchi. Picha inayotumika inaturudisha nyuma kisaikolojia kujiona mpaka kufikia mwaka 1900 afrika ilikuwa bado kabisa hata kuvaa nguo walikuwa bado wanavaa kufunika tupu. Najua kuna wengine watasema haiathiri kitu lakini kusema hivyo ndiyo haswa lengo lao wazungu, muone haiathiri kitu ili muendelee kuwalisha matangopoli watoto juu ya wale mashujaa.
Kuna mambo mengi yamefutwa kwenye historia ya vita hii. Mfano: watu wa kanisa katoliki walikatazwa kupigana vita hii, why.