Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

kwenye Maisha yangu nimemwomba Mungu nimiliki hizi gari tu. Nina uzoefu wa miaka mitatu natumia hizi gari aisee ni nzuri over watu wanavyosema unapita popote na zina stability nzuri sana barabarani. Ukitaka uzifaidi zaid tumia ambazo ni petrol hutakaa uache hizi landrover ni zaid na Zaidi.
 
[emoji3][emoji3] ni sawa na kampuni za Tours zilizonunua Landrovers nyingi kipindi cha Utalii ukiwa juu sana, hizo gari zilikuwa zinawachefua sana zikirudi kutoka porini ni matatizo sana....ila wenye Land cruiser mkonge wanapeta tuu... Chuma inafika inapita carwash asubuhi inarudi porini tena
Hapa Moshi kila mwenye kampuni anapambania LandCruiser tu! Kuna wanaojitutumua kununua Landrover ila wachache mno. Nina hakika watarudi kwa Mjapan msimu wa mvua ukiisha
 
kwenye Maisha yangu nimemwomba Mungu nimiliki hizi gari tu. Nina uzoefu wa miaka mitatu natumia hizi gari aisee ni nzuri over watu wanavyosema unapita popote na zina stability nzuri sana barabarani. Ukitaka uzifaidi zaid tumia ambazo ni petrol hutakaa uache hizi landrover ni zaid na Zaidi.
Diesel vipi?
 
Landrover defender engine ya toyota Ihz [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
IMG-20200727-WA0001.jpeg
IMG-20200727-WA0003.jpeg
IMG-20200727-WA0002.jpeg
IMG-20200727-WA0000.jpeg
 
Kuna mdudu TUNDRA pia naitamani sana hii garii sema bado nafanya utafiti nipate ya mkono wa kulia sio LHD
Ndio zao wazungu, wamegundua mbali na sifa ila Landrover ni gari sumbufu.
 
Kuna Land rover moja ya shirika nilikuwa nagongea gongea kipindi fulani, kwa kweli ni gari nzuri sana upande wa engine, power ya kutosha na mafuta zinakula vizuri tofauti na Toyota pia haziyumbi barabarani. Faida yake nyingine ni kwamba ukiwa Off-road huwezi kwama hata iweje, inapita popote pale ambapo pana upenyo wa njia...
Hapa sijaelewa, unaiitaje nzuri pamoja na hayo mapungufu yote?
 
Waasi hawataki ujinga na chuma ya mjapani! 1Hz kwa kwenda mbele 🤣🤣🤣 hadi ikazua mjadala kwanini waasi wananunua LC nyingi mno? Nani anawapa hizo gari?

Aliuliza bwana trump!
Waasi wanapenda L/Cruiser 1HZ ila saizi wengine wamehamia kwenye L/Cruiser zenye 1VD-FTE huko majangwani wanakimbiza magari kama rally.

Hawa jamaa sijui wanapata wali hizo gari, wanaenda sawa na UN na NATO.
 
Hapa sijaelewa, unaiitaje nzuri pamoja na hayo mapungufu yote?
Land Rover ni nzuri kwa uimara wa body zile za aluminium hata ukigongwa unarudi nyumbani unanyosha na nyundo kisha unapiga drill na kuweka pop livert.

Injini zao nzuri kwenye nguvu na ulaji wa mafuta. Tatizo ni kwenye kuua bush,bearing na kuna Defender nyuma zina coil spring hizo hazitaki shurba ya mzigo.

Kuhusu kutulia barabarani hawajatofautiana kati ya Land Cruiser series 70 na Defender. Hizo zote ukijiroga kulala kwenye kona Kali na 80km/h lazima uguse ardhi.
 
kwenye Maisha yangu nimemwomba Mungu nimiliki hizi gari tu. Nina uzoefu wa miaka mitatu natumia hizi gari aisee ni nzuri over watu wanavyosema unapita popote na zina stability nzuri sana barabarani. Ukitaka uzifaidi zaid tumia ambazo ni petrol hutakaa uache hizi landrover ni zaid na Zaidi.
Mkuu inaonekana unapenda mbio, hizo injini za Petrol za Land Rover ukigusa kidogo inafunguka sana.

V8 za petrol ni hatari kwa barabara zetu labda uwe kwenye Discovery 3 ikiwa kwenye L/Defender unaweza ukapinduka maana inachanganya haraka na ina mbio.
 
Land Rover ni nzuri kwa uimara wa body zile za aluminium hata ukigongwa unarudi nyumbani unanyosha na nyundo kisha unapiga drill na kuweka pop livert.

Injini zao nzuri kwenye nguvu na ulaji wa mafuta.
Tatizo ni kwenye kuua bush,bearing na kuna Defender nyuma zina coil spring hizo hazitaki shurba ya mzigo.

Kuhusu kutulia barabarani hawajatofautiana kati ya Land Cruiser series 70 na Defender. Hizo zote ukijiroga kulala kwenye kona Kali na 80km/h lazima uguse ardhi.
Mkuu, sasa Defender mpya 110 wametupia na air suspension, na umeme/computer kila kona. Likiroga huko porini sijui unalitoaje.
 
Back
Top Bottom