Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

Kwanini Landrover Defender zinapendwa sana?

Huu uzi mtamu sana kuusoma wakuu tupieni madini.
Mimi nanatamani sana brand za Landrover, Nikaanza na Freelander ila changamoto zake zikanishinda nikapiga chini.
Nikipata hela nitarudi tena.
Nna uzoefu na Freelander 1 achana na hio gari kabisa,engine zake za K-Series zinazingua mbaya kabisa.

Wadau wengi kwny Freelander1 wametoa engine yake wakapachika 3S ya Rav 4.

Freelander 2 hio ndio sina uzoefu nayo so siwezi ku-comment chochote boss.
 
1PZ sijawahi kuzielewa kwa kweli ila 13B ni ya kibabe 😂😂😂!!!

1HZ ndio mashine ya ndima kwa miaka na miaka na still anaendelea kuitumia tu hata kwenye matoleo ya 2020! Siku akikatisha production ya 70 series watu wengi tutaumia sana.

Ila 1VD sijawahi itumia japo nikafeel pulling yake ila kwa body jepesi la 70 series itakuwa ina move sio kitoto.
Kaka 1PZ moto wake achana nao si wa kitoto.Mjapani hii injini alitengeneza kimajaribio kwenye Land Cruiser Series 75 na akaja kuweka kwenye Toyota Coaster baadhi.

1PZ ilikuwa ni ni inline 5 cylinder na gearbox yake ilikuwa ni gear 4.Mjapani hakuendelea kuzalisha tena injini hii. Kwa Tanzania Cruiser nyingi zilizokuwa na 1PZ ni za makanisa na taasisi binafsi ndio wengi zipiwasumbua kwenye cylinder head gasket na kasheshe ilikuwa ni ina 5 piston upatikanaji wake ilikuwa mgumu.

Coaster zenye 1PZ ziliogopwa sana, hii injini haitaki shurba za kazi ngumu ila ina spidi sana.

Kama Toyota angeendelea kuzalisha au kuifanyia maboresho kwa kupunguza ukubwa na kuipa turbo leo hii tungekuwa tunaishindanisha walau na Td5 ya Land Rover.
 
sema Landrover hakubase sana kutengeneza engine zenye cc kubwa kama cruiser.labda kwa discovery 3 and 4
Land Rover injini alizotengeneza cc kubwa ni upande wa petrol tangu zamani zina 4600cc. Kwenye diesel alitamba na teknolojia ya kuwa na cc ndogo+turbo kisha ingini inakuwa na nguvu.

Kuchamba kwingi kutoka na mavi. Land Rover injini za Diesel huko Ulaya uzao wa Td200/Td 300/Td 5 zimeshindwa kukidhi vigezo vya Euro Emission. Hizo hata wakiboresha vipi zilishindwa kukidhi vigezo zinachafua mazingira mpaka zikafanya soko kwa Ulaya kuwa Gumu.
 
Land Rover injini alizotengeneza cc kubwa ni upande wa petrol tangu zamani zina 4600cc.
Kwenye diesel alitamba na teknolojia ya kuwa na cc ndogo+turbo kisha ingini inakuwa na nguvu.

Kuchamba kwingi kutoka na mavi.
Land Rover injini za Diesel huko Ulaya uzao wa Td200/Td 300/Td 5 zimeshindwa kukidhi vigezo vya Euro Emission. Hizo hata wakiboresha vipi zilishindwa kukidhi vigezo zinachafua mazingira mpaka zikafanya soko kwa Ulaya kuwa Gumu.
engine gani ya Landrover ina cc 4600?
 
Hiyo gari kaweka bomba kubwa ili apate mzuka wa sauti ya injini.

Hiyo haijafanyiwa tunning yoyote, jamaa jioni nilikuwa namuona akirudi nayo kuelekea Kimara inatia hamasa kwa sauti ukiwa nyuma.
Huyu bwana fundi wa malori ni mbunifu.
hata kwenye altezza huwa wanafanya sio?
 
Nna uzoefu na Freelander 1 achana na hio gari kabisa,engine zake za K-Series zinazingua mbaya kabisa.

Wadau wengi kwny Freelander1 wametoa engine yake wakapachika 3S ya Rav 4.

Freelander 2 hio ndio sina uzoefu nayo so siwezi ku-comment chochote boss.
Mkuu yangu ni Freelander 1 ni gari nzuri ukiwa nayo road very powerful na ina balance sana,
Niliweka engine ya 3s Rav 4 kidogo angalau ila changamoto ni kuvunja ma bush na spear zingine asee hizi gari zinahitaji matunzo sana.
 
Aisee hizo gari ni changamoto mkuu lkn ziko poa sana,nilikua nayo miaka flani lkn changamoto zake zilinishinda nikamuuzia mtu akaja kuweka engine ya 3S akawa anapiga nayo misele.
 
engine gani ya Landrover ina cc 4600?
Land Rover ana injini za V8 petrol mpaka ya 5000cc. Hizo nyingi zipo kwenye Land Rover Defender na Range Old Model.
Land Rover Defender na Range old model zenye V8 ndio watu hutumia kuchezea rally.

Kama utahitaji kuzijua kiundani kuna jamaa wapo Arusha wanaizo Range Old model wanachezea rally, Tanga yupo Bahoza ana dude kama hilo.
 
lazima nitafute engine hiyo?
 
Back
Top Bottom