GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,660
- 121,325
Rais wa Tanzania Samia
Laiti wewe na serikali yako mngetengeza urahisi wa upatikanaji wa nishati mbadala (hasa matumizi ya gesi) kwa kuifanya ipatikane kwa bei nafuu mno, sidhani kama 95% ya Watanzania wangeendelea kuharibu misitu ili wapate kuni/Mkaa wa kupikia.
Hali ambayo imesababisha sasa sehemu kubwa ya nchi kuwa Jangwa na mvua kushindwa kupatikana, mito mikubwa kukauka, maji kutopatikana na sasa taifa liko katika mgao wa maji. Na muda wowote toka sasa mgao nao utatoweka na Watanzania tutaanza kufa kwa kukosa maji na chakula pia.
Makamu wa Rais Dk. Mpango
Moja ya jukumu lako mama (kuu) ni kushughulikia mazingira baada ya lile la muungano. Na wewe wenye akili (japo hatuna Doctorate kama yako) tulikutegemea kuwa kutokana na kuwa 'that Intellectual' basi ndiyo ungekuwa mtetezi mkubwa wa kupambana suala zima la utunzaji wa mazingira.
Hivi Makamu wa Rais yaani hujui kuwa kama ungekuwa mkali na kusimamia kauli zako na sera ya lazima ya upandaji miti kwa kila Mtanzania, leo hii nchi isingekuwa na huu ukame unaoenda kutukumba na taifa kuwa katika mgao huu wa maji?
Makamu wa Rais yaani siku zote nikikuona huwa nakuona unatoa tu matamko yako katika hafla zako ila sikumbuki ni lini GENTAMYCINE mimi nimewahi kukuona ukitembelea maeneo mbalimbali ya nchi kuhimiza ppandaji wa miti ili kutunza mazingira na kuzuia katika ukataki wa miti (misitu), ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mvua, ambayo sasa tunaisubiria inyeshe ili tupone na tishio la ukame mkubwa Tanzania na Afrika Mashariki yote kwa mujibu wa DW ya Ujerumani.
Makamu wa Rais Dk. Mpango jifunze kufanya 'Walk the Talk' na achana na hii 'Talk the Walk' kwani ndiyo imekugharimu kama msimamizi wa sera ya mazingira nchini Tanzania ambayo kikatiba wewe ndiyo msimamizi wake mkuu.
Hivi Makamu wa Rais Dk. Mpango ungekuwa kweli mkali (that tough), mimi GENTAMYCINE kila siku ningekuwa napishana na pikipiki 30 hadi 45 zikiwa zimebeba magunia ya mkaa ambayo huwa wanaifaulisha usiku kutoka katika malori makubwa, ambayo huwa yanapaki maporini Vigwaza, Msata na hata Kibaha?
Makamu wa Rais Dk. Mpango hivi una taarifa kuwa hivi sasa 85% ya mikoa yote ya Kanda ya Ziwa (kwetu GENTAMYCINE mkoani Mara), mikoa ya Kusini na mikoa ya Nyanda za Juu ni jangwa tupu? Miti imekatwa kwa ajili ya kuni na mkaa hivyo kupelekea mikoa hiyo muhimu na ya kimkakati nchini Tanzania kuwa jangwa, na ukame wa mvua inayosababisha upatikanaji wa maji.
Tafadhali Makamu wa Rais Dk. Mpango punguza sana kutupigia picha zako ukiwa makanisani kuabudu ili utuaminishe akina GENTAMYCINE kuwa wewe ni mcha Mungu sana na ni mtu wa imani. Bali sali kidogo tu kama Wayahudi wenye dini na imani yao, kisha tumia muda wako mwingi kupambana na kuzitatua changamoto za Watanzania wengi.
Ili hata basi ukimaliza kuzitatua na ukienda huko makanisani kusali (kuabudu) Mwenyezi Mungu anakubariki zaidi, kwani inawezekana kwa sasa unafululiza kusali ila hupokei unachokiomba kwake kwakuwa naye anaona bado hujawa msaada kwa maendeleo ya Watanzania aliyokupa uwaongoze kama Makamu wao wa Rais.
Tafadhali Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu wako (wetu) wa Rais Dk. Philip Isidori Mpango hali ni mbaya sasa nchini Tanzania kutokana na huu ukame mkubwa na kukosekana kwa maji, ambayo ni moja kati ya nishati muhimu kwa maendeleo ya kila Mtanzania na Tanzania kama taifa.
Hivyo kuanzia sasa lichukueni hili kama ajenda yenu kuu katika kuikoa hii hali, kwani msipoiwahi kuitatua sasa haitotuathiri kijamii bali zaidi kiuchumi na uwekezaji ulioko na hata ajira kutetereka pia.
Lipokeeni jambo langu hili kiumakini.