Kwanini M23 wanajiamini kiasi hiki?

Kwanini M23 wanajiamini kiasi hiki?

icon_2000

Senior Member
Joined
Jul 14, 2024
Posts
177
Reaction score
256
Yani wanataka jeshi liweke silaha chini😔
Screenshot_20250125-230627.jpg
 
Congo nchi kubwa lakini inashindwa kulinda mipaka yake vema. Waasi na wavamizi wanajichukulia vipande watakavyo. Congo ilitakiwa iwafagie M23 mpaka kwa anayewafadhili, wanamjua. Kinshasa tu ndio kuna usalama lakini maeneo mengine hali ya usalama ni tete
 
Exactly, ni kama Nyerere alivyomfuata Idd Amin hadi Chumbani kwake. Shida hao M23 ni Wafaransa wanaomtumia Kagame kupora utajiri wa DRC
 
Kama wafaransa wanamtumia kagame kuteteresha amani na usalama wa congo anyukwe tu mpaka kigali. Ufaransa iambiwe wazi inachofanya congo si kizuri
 
Si Ufaransa tu.. hapo DRC wapo warusi, wachina, Wamarekani nk.
Wote wanataka madini ya Bei chee au barter trade ya silaha Kwa madini
 
Wamefocus kuwauwa vijana wao tu badala wawapeleke jeshini wakafie kuipigania nchi yao wanawauwa ovyo, wawalete bongo wapate mafunzo
 
Congo wajinga sana.wamekazana kuua vibaka waitwao koluna lakini waasi wa m23 wamewashindwa.Jinga kabisa hii nchi
 
Exactly, ni kama Nyerere alivyomfuata Idd Amin hadi Chumbani kwake. Shida hao M23 ni Wafaransa wanaomtumia Kagame kupora utajiri wa DRC
Unaweza kuthibitisha uwepo wa ufaransa ndani ya m23 au ndiyo store za kwenye kahawa
 
Unaweza kuthibitisha uwepo wa ufaransa ndani ya m23 au ndiyo store za kwenye kahawa
Sila za kivita zinazotumika na M23 ni brand ya Ufaransa, zinatengenezwa Ufaransa.., mfano rocket launcher wanazo za kisasa kabisa, na baadhi zilikamatwa na Tshekedi.., unataka wadhibitishe vipi tena.., pia panapotokea machafuko ya M23, mauzo ya Madini nje ya nchi ya Rwanda huwa yanapaa kwa 200% , madini ambayo Rwanda hayapatikani, mfano Cobalt na Tantulum.., hiyo maana yake nini? Na refinery destination ya hizo exports ni Ufaransa, hiyo maana yake nini?
 
Back
Top Bottom