BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Hivi wakuu mmegundua wizi unaofanywa na Mabenki kwenye makato ya miamala? Licha ya Serikali kufuta Tozo za Miamala ya uhamishaji fedha ndani ya Benki, kwenda kwenye Simu pande zote, kutoka Benki moja kwenda nyingine tangu Okt. 1, 2022 lakini bado kuna Benki zimeendelea kukata tozo hizo bila maelezo yoyote.
Suala lingine ni kimya wa Serikali unanitia mashaka kwenye hili jambo kwamba je haitambui au inashiriki kwenye huu wizi wazi wazi? Na kama Benki zimeongeza gharama mbona hazijatoa taarifa kwa mteja kuhusu mabadiliko hayo?.
Serikali ichukue hatua za haraka kudhibiti wizi wa wazi unaofanywa na Mabenki katika suala la Tozo za Miamala pia Benki zitoe taarifa fedha zinazokatwa nani anafaidika nazo. Vinginevyo tutaamini kuwa ilituhadaa kuwa imefuta lakini hakuna kilichofanyika.