Hahaha hawa jamaa watakuwa wanapiga pesa sana kwa kutumia.Ungeweka hati za nyumba labda ungeipata, maana ya bima unatoa sehemeu ndogo ya thamani harisi ya kitu, ili itakapo tokea janga wao bima wachange na za wengine kufidia hasara, kwa kifupi kama hakuna dharura hiyo pesa inakuwa imeliwa au imetumika kufidia wengine.
Nimekuelewa japo naona kama janja janja tu za kupiga pesa.Ngoja na mimi nijaribu kuchangia;
Jambo la kwanza; bima yoyote inakatwa kwa ajili ya event. Na kwa ajili ya bima tunalipa insurance premium ambayo ndiyo uliyokatwa. Hii premium inatengeneza sum insured ambayo ndo ule mkopo uliochukua.
Kwenye hii arrangement ya mtoa mada kama nimeelewa vizuri, alikata bima ya maisha na ulemavu wa kudumu (credit life).
Ni kweli hii italipa deni lako litakalokuwa limebaki kama utafariki au kupata ulemavu wa kudumu wakati mkopo haujamalizika.
Lakini ikitokea ukacancel mkopo wako kabla ya muda basi utapaswa kurudishiwa sehemu ya premium ambayo haija-expire bado.
Lakini deni linapoisha kulingana na muda mliokubaliana basi na bima inaisha. Yaani lapse of time or marurity of the subject. Premium haiwezi kurudishwa kama muda umepita.
Ni hayo tu kwa sasa
Benki pekee inayorudisha bima wakati ukimaliza mkopo ni Standard charterd.Habari zenu wanajamvi
Miaka sita (6) iliyopita nilichukua mkopo bank ya CRDB kwa dhamana ya utumishi na marejesho yakiwa yanakatwa moja kwa moja kwenye mshahara, moja ya masharti ya ule mkopo ilikuwa ni lazma ukatiwe bima dhidi ya kifo au ulemavu wa kudumu, maafisa mikopo wa CRDB walinielimisha vizuri sana kuhusu hii bima amabayo wanaikata kwenye kile kiasi ulichoomba mkopo, nadhani ni kama 200k+ kama sikosei.wakanielieza kwamba
Kile kiasi cha pesa kilichokatwa kwenye mkopo nilioomba kama Bima kinasimamia upotevu wa fedha,mali iliyokatiwa Bima kutokana na kutokuwepo kwa uaminifu kutoka kwa waajiri wakati wafanyakazi wakiwa kazini. Bima hii pia inasimamia usalama wamali iliyochukuliwa kama dhamana. Wakaendelea kusema,
Bima hiyo inalipia hasara ya fedha anayoipata mkopeshaji ( ambao ni wao CRDB Bank) kutokana na matatizo aliyopata mdeni kufuatia majanga ya kifo au ulemavu wa kudumu kabla hajamaliza kulipa deni. Husaidia kupunguza hasara ikilinganishwa na dhamana iliyowekwa. Kwa wakopaji wasio na dhamana za kazi Bima hii ina hakikisha familia ya mhanga haiachwi bila makazi au mzigo wa kuendelea kulipia deni linalodaiwa pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu wa kudumu.
HOJA YANGU
Deni langu lilikuwa la miaka mitano (5) na mwaka jana nilimalizana na hili deni, yaani hawanidai tena tangu mwaka jana, nilitegemea baada ya deni kumalizika hawa CRDB bank wanirudishie ile pesa yangu Zaidi ya 200K kwa vile mkopo wao tayari nimeurudisha wote pamoja na riba na bila usumbufu, mwanzoni mwa mwaka huu niliwatumia barua kuwakumbusha kuhusu kunirejeshea hii pesa hawajanijibu hadi leo, jana nimewatumia email kupitia kwa DG wao bado pia naona kimya.
Hii kitu imeekaaje kwa hapa bongo, au ndo bank inadhulumu wateja wao…, nakumbuka nilikopaga pesa stanbic bank nikiwa Kenya kwa mda wa mwaka mmoja na baada ya mkopo kuisha nikarejesehewa hii pesa tena wakani email kabisa kunitaarifu.
Najua wakopaji kwenye hizi taasisi za kifedha wako wengi na najua na wao hawajui kama wanatakiwa kurudishiwa hii pesa baada ya mikopo kumalizika , naombeni kujulishwa kama hapa bongo hii pesa huwa hairudi hata kama deni lao umemaliza lote?
Mkuu hata mimi stanbic bank Kenya walinirudishia japo hapa wadau wanakataa kwamba hairudishwiBenki pekee inayorudisha bima wakati ukimaliza mkopo ni Standard charterd.
Wiki iliyopita nilitoa maoni yangu kwa bank nyingine kwamba walifikirie jambo hilo.
Gharama za processing fee ni wizi wa waziwaziProcessing fee kwa upande mwingine ni gharama inayolipwa na mkopaji kwa ajili ya shughuli mbalimbali zinazohitajika kukamilisha mkopo
Kwa haraka haraka nafikiri gharama zake ni kama vile stationeries, travel here and there, kuja kufanya uhakiki ( kwa baadhi ya aina ya mikopo), na vinginevyo
Huu nao ni wizi hayajatokea, why nisirudishiwe?Hivi unajua maana ya BIMA???
Bima amana inayowekwa ili yanapotokea matukio fulani ya kuleta hasara kwa kwa mlipaji basi aweze kufidiwa, ikizingatiwa kwamba matukio hayo yasipotokea, basi mlipaji hatarudishiwa pesa yake hiyo..
Sasa ndo sijafukuzwa na wala sijafa wanirudishie, hizi taasisi kuna sehemu hawatoi elimu vizuri ili wapate mwanya wa kutupigaMh kwani hiyo bima ni dhamana?..na je dhamana unatoa wewe mkopaji au benki?..kama unatoa wewe mbona bima imejumlishwa kwenye mkopo means hutoi wewe direct mfukoni mwako kama ilivyo hati ya nyumba....so kiutaratibu hairudishwi ila iliwekwa kumlinda mkopaji incase umetangulia mbele ya haki au umeachishwa kazi kwa sababu ambazo hukusababisha wewe basi mali yako isichukuliwe..hivyo tu...watakuja wenyewe na majibu
Kwanini warudishe?ndio mkuu lazma warudishe, vinginevyo watakuwa wanawaibia wateja wao