Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Mkuu Kuna nyumba imetangazwa karibu mara ya sita sasa na mkopaji no marehemu imekaaje hii. Jamaa ni mtoto kwenye hiyo familia wazazi wake wamefariki wote, ndugu zake kaka na dada wamefariki kabaki yeye na wajukuu wa hiyo familia. Yeye ndio mtoto pekee wa marehemu akaenda kukopa 70M . Baada ya Kama mwaka amefariki mbona nyumba inapigwa mnada Kama marehemu hadaiwi.
 
Well said. Umemaliza mkuu
CASE CLOSED kama kuna mbishi aende darasani kusoma kuhusu bima.
Ila watanzania wengi sana wana uelewa mdogo mtu anashindwa hata kujua bima inafanyaje kazi anakuja kusema alikopa Kenya alivyomaliza akarudishiwa bima, hamna kitu kama hicho ELIMU ELIMU ELIMU. Tujifunze kuhusu vitu kama security, bond, insurance, collateral n.k ni mambo ya finance, uchumi na hata sharia za mikataba. Tutumie mitandao vizuri haya mambo yamejaa humu tena bureee. Tunashinda insta tu kupigana vijembe wakati internet ina kila kitu cha kukukomboa kiakili na kukutoa kwenye ujinga
 
Kwenye mikopo kuna option tofauti tofauti kutokana na makubaliano. Mikopo mingine unaweka bima kama ukifa au kupata ulemavu ambao hautaweza kufanya kazi tena basi bima inafidia na kuna mingine ambayo mtu anaweka dhamana kitu/mali kama nyumba shamba n.k kwa hiyo option ya pili ukifa wanachukua dhamana kufidia mkopo.

Mara nyingi mikopo ya kukata kwenye mishahara ndio uwa inawekewa bima au mingine mafao yako na mikopo mingi ya biashara dhamana uwa ni mali/vitu

Huyo ambaye amefariki na nyumba yake inauzwa atakuwa aliweka hiyo nyumba kama dhamana ya kukopea na kwenye mkataba inaandikwa kabisa ukishindwa kulipa kwa sababu zozote ikiwemo kifo dhamana itatumika kufidia deni
 
Nimefurahi mada ni nzuri ila Cha kusikitisha ni kwamba watu wanambishia mtoa mada bila kuwa na sababu za kubisha. Mimi nimewahi kukopa lakini sikusaini sehemu yoyote inayoonesha kuingia kwangu mkataba na bima, kwa maoni yangu tusome zile fomu kwa umakini na tuje na majibu hapa kwa wadau au piga picha hiyo page inayoelezea bima ya mkopo.mimi naamini bima hii haiwezi kufanana na bima ya magari au nyumbani, hebu tukubali kupokea mawazo mapya na tuyachunguze kama yana ukweli au la tusiwe na mawazo mgando. Nimefurahi jamaa kaleta challenge kubwa japo inaonekana simple kwa wale simple mind.
 
Kuna vitu viwili hapa naanza kuwa na mashaka :-
(A)loan insurance
(B)loan security
Vipi wadau hivyo vitu vinafanana nafikiri kule bank wanatumia neno mojawapo Kati ya hayo
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Yani Unaongea Vitu viwili tofauti mzee baba... Kaa ukijua Riba pale sip Bank kwamba umeweka hela wakutunzie Riba wanachukua hela yako kwamba Likitokea tatizo wao wahusike kulisolve mfano wewe unaweka Riba laki 2 lakini kwa Riba hio hio wai likitokea tatizo la Mil 2 watalisolve. BIMA means pesa zinachangwa kusaidia kutatua matatizo ya watu kwa urahisi yatakapotokea so kama wewe halijakupata tatizo kuna wenzako wamepatwa na majanga na pesa yako Obvious itatumika kusolve lile tatizo kama vile ambavyo pesa yao itatumika kusolve tatizo lako likutokea. HUWEZI DAI PESA YA BIMA KAMA NHIF ETI KISA HUJAUMWA NOOO[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] BIMA SIO BANK PALE UKITAKA HIVYO PELEKA HELA YAKO BANK IKAE.
 
Reactions: Ctr
Ingekuwa unachosema ni sahihi basi makampuni ya Bima yasingestawi. Hela unayochajiwa Kw ajili ya bima ndio faida ya makampuni ya Bima pindi inapotokea umemaliza salama mkopo wako,

Ukipata hasara pesa hiyo ndio inachanganywa na nyingine za wenzako ku compesate majanga, ni kama kwenye magari tu
 
Tatizo la kifedha ni tatizo kama matatizo mengine tuu maana hata Kwenye bima zingine kinachotoka ni fedha...!!
 
Yani Hakuna utofauti hata Nukta hapa...!! Bima ya Mkopo sijui bodaboda...nyumba zote ni sawaa
 
Wakirudisha hiyo hela huo mfuko utakuaje sasa ili kesho uweze kumsaidia atakaepata hayo majanga? Ww hujapata ila pengine mwenzako kapata hiyo shida, hela yako na ya wengine imetumika kumlipia aliyepata shida. Bima huwa hairudishwi mkuu.. kwan kwa mfano ww hapo umetoa laki 2, alaf umekopa mil 50, ukapata shida wakat bado unadaiwa mil 40, unadhan hizo hela za kulipia hilo deni lako zinatoka wapi?
 
Mi nimemaliza mkopo iwaje nilipe fidia ya wengine bado jibu halijakaa sawa
Ww usingemaliza hiyo laki 2 inatosha kulipa mill 20? Jiulize hilo, hizo pesa ambazo ningejaziwa mm kama ningepata shida zinatoka wapi? Heb jiulize hayo maswali
 
mkuu madhumuni ya bima ya afya ni tofauti na bima ya mkopo... hii mikopo pamoja na kwamba wanakata bima pia kuna dhamana... mbna stanbic kenya walinirudishia, why hizi bank zetu za ndani hazirudishi?
Hiyo bima ndio itakuja kuzuia nyumba yako kuja kuuzwa kama ndio uliweka dhamana. Hiyo stanbik kenye labda ni trik yao tu ya kutafuta wateja ila mfuko hauwez kikua hapo uweze kukusaidia kesho ukipata shida.
 
Kanuni ya bima ni moja ingawa kuna bima za aina tofauti. Alicholeta mtoa mada ni mortgage insurance au loan insurance. Unapoingia mkataba na benki wao ndio wanaingia mkataba na kampuni ya bima na sio wewe. Mteja wa mkopo anachofanya ni kulipia premium ambayo benki inaipeleka kwenye kampuni ya bima na kama ikitokea mteja amekufa basi benki italipwa na kampuni ya bima.

Hapa mteja wa mkopo anakuwa kama third party kwani haingii moja kwa moja mkataba na shirika la bima bali benki ndio inaingia mkataka na bima ili kama ikitokea tatizo iweze ku-recover loss. Na pia hapa mteja wa mkopo hawezi kupewa insurance policy document kwani huo ni mkataba wa benki na bima.

Kuweka bima mkopo kuna manufaa sana maana ikitokea maafa basi mteja aliyepoteza uhai familia yake haitopata shida kwani bima itafidia deni tofauti na kuweka dhamana ya mafao au nyumba
 
Huyu jamaa amekataa kuelewa
 
Bima ya mkopo, maana yake ni kuwa pesa hiyo imepelekwa bima, iweje tene urudishiwe? Kama mkopo umelipwa pasipo tatizo maana yake ni kuwa bima ndiyo wamenufaika na fedha hiyo na siyo bank. Sasa iweje bank wakurejeshee pesa ya bima?

Bima za tahadhari yaani za magari, majumba, biashara, wafanyakazi nk zinazokatwa kila mwaka, je ukiisha mwaka bila kupata tatizo unarejeshewa?
 
Mi sikuingia mkataba na bima na nimrkopa na hela wamekata wapeleke bima. Ikitokea nimekufa ni kipi kitakacholinda shamba langu lisiuzwe?. Yaani si kwamba bank watapata malipo mara mbili. Kwenye familia yangu na kwenye bima wote tutalipa. Maana hakutakuwa na vielelezo vyovyote vya familia yangu kujinasua. Aliyeingia mkataba na bima ni bank mwenyewe. Inamaana mi kwenye bima sitambuliki ila nimewalipa!!
 
yes hata mimi ni hivi mkuu thats why nataka wanirudishie pesa yangu
 
Mi sikuingia mkataba na bima na kipindi nakopa hela wamekata bank sijui kama walipeleke bima, na sijui kama bima wananitambua mimi kama mteja wao na mimi siwafahamu wao
 
Hivi mfano umekatia BIMA Passo yako au Vits then hiyo gari haikupata ajali wakati huo,so bima ikiexpire hua tunakwenda kudai hiyo hela uliyokatia bima?,mfano huu hauna tofauti na hii ya bank
 
Mimi sijui sana lakini nimepata swali kutokana na bandiko lako.

Je, walikuambia kwamba hiyo fedha ya bima utarudishiwa?

Ninavyofahamu mimi ni kwamba huduma za bima zinatumia mfumo wa kuchangiana nikiwa na maana kuwa kama ulikopa M5 ukalipia bima 200k halafu ikatokea hauwezi kulipa benki itakua imepata hasara.Hivyo kinachofanyika ni kutumia fedha nyingine za bima kutoka kwa wateja wengine ili kufidia hasara.

Hata magari tunakatia bima na pale inapoisha hata kama hujawahi kuitumia hela yako hairudi na utaikatia bima nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…