Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Hivi mfano umekatia BIMA Passo yako au Vits then hiyo gari haikupata ajali wakati huo,so bima ikiepire hua tunakwenda kudai hiyo hela uliyokatia bima?,mfano huu hauna tofauti na hii ya bank
mkuu ni vitu viwili tofauti kabisa kati ya bima ya mkopo na bima ya gari
 
Wewe hujaingia mkataba wa bima ila benki ndio imeingia mkataba na bima. Wewe umeingia mkataba na benki ambapo ndani yake kuna clause ya malipo ya bima (premium) na yana maelekezo kuwa endapo mteja atafariki au kupata ulemavu ambao hataweza kulipa deni basi bima italipia deni lake.

Kwa kuingia mkataba na benkini kwamba benki watabanwa na hiyo clause ya bima hivyo likitokea la kutokea hawatakukata deni bali bima itakulipia

Hayo mambo yapo kwenye mkataba. Tatizo ni kwamba wakopaji uwa hatusomi maelezo ya mkataba.
 
mkuu ni vitu viwili tofauti kabisa kati ya bima ya mkopo na bima ya gari
Hakuna bima inayorudishwa duaniani kanuni kuu ya bima ni wengi kuchangia kidogo kidogo ili mmojawapo anapopata janga basi Fidia inatoka kwenye pool ambayo wote mmechangia. Unaweza wewe binafsi usipate janga ila ulichokatwa kimemchangia mwenzako. Kwa logic hiyo hata chako kidogo kimetumika na wengine na huwezi kurudishiwa. Hiyo ndio logic kuu ya bima. Hizo nyingine ni categories tu za bima lakini msingi mkuu wa bima ni kuchangia kidogo kidogo ili mmoja akipata janga anafidiwa kutoka kwenye michango ya wenzake

Nimetumia lugha rahisi ili nipate kueleweka hata na layman
 
Pia benki hawawezi kuuza shamba au mali yako yoyote kama hujakubaliana nao iwe sehemu ya dhamana ya mkopo, hata mafao yako kama ni mafanyakazi hayawezi kuguswa unless umekubaliana nao. Kwanza kama hujaiandikisha hiyo mali kama shamba au nyumba kwenye dhamana ya mkopo wao wataijuaje kama unayo? Benki walipata shida sana kwenye haya ndio maana wakaona waje ni suala la bima ili kupunguza risks za kupoteza fedha kutokana na vifo au ulemavu
 
ngoja niende NMB fasta wanirudishie hii pesa yangu, maana tayari nshalipa deni pamoja na riba so nawafuata kesho asubuhi
Ukipata jibu utupe mrejesho mkuu maana nami ni mhanga mtarajiwa.
 
Umeongea kitu cha maana wengi wengi huwa hawatilii maanani ili lakini unapoint ya msingi sana kama mkopo umenda smooth kuna kila sababu ya kurefund hii pesa, labda endelea fatilia zaidi tujue sheria zetu zinasemaje
Ukilipia bima ya gari ya mwaka lisipopata ajari pesa unarudishiwa? Bima ya afya usipougua unarudishiwa? Sheria ya bima inasemaje.
 
Mkuu tafadhari tofautisha bima ya mkopo na hizi bima zingine.... Inawezekana na wewe ukawa mwehu mkuu
alaaah kumbeeee......Bima ya mkopo maana yake nini hebu leta reference, ili tuongee kwa facts zaidiii. Na onyesha mkataba ambao ulisaini unasema kwamba wanapaswa kukurudishia hiyo hela ..
 
Mimi nadani hiyo hela ni haki kurudishiwa kwasababu mkopo ulikua na marejesho yenye riba ambayo riba ndio faida yao hiyo bima inakuwepo tu incase anything hapen.kwaiyo kama umemaliza mkopo na hakuna lililotokea kwanini wasirudishe hiyo hela. na katika hali ya kawaida hiyo bima inafanana tu jina la bima lakini ni kitu tofauti sana na bima zingine kama za majengo, magari na afya.Nadhani hapa watu wa mabank watueleze vizuri hiyo ela inakuaje.
 
Unajua ukifikiria kwa kina unaona kuna kitu kimejificha hapa kwenye hiyo bima ila sema ndo hivyo namna yakuliweka vizuri ndo inaleta shida kwasababu limeangukia kwenye bima ila nadhan kuna kitu hakiko sawa hapa.
Mi sikuingia mkataba na bima na kipindi nakopa hela wamekata bank sijui kama walipeleke bima, na sijui kama bima wananitambua mimi kama mteja wao na mimi siwafahamu wao
 
Mi sikuingia mkataba na bima na kipindi nakopa hela wamekata bank sijui kama walipeleke bima, na sijui kama bima wananitambua mimi kama mteja wao na mimi siwafahamu wao
Wewe uliingia mkataba na bank nao bank 1wapo ya masharti ni mkopo kuwa na bima. Hivyo uliyakubali masharti hayo na kasaini nayo bank kama wakara wa bima alimlipa bima asilimia uliyoisaini kwa usalama wa pesa uliyokopeshwa.
 
Ukikaa kimya hawakuambii na wanazila,hakuna benki isiyoibia watu nchi hii...
 
...Hoja Njema Sana. Kweli, kwa mini hawarudishi....?
 
hivi mkuu nikiweka bond simu kwako ukanipa 120K kwa makubaliano nikilipa deni lako na riba uliyonipa unirudishie simu yangu, nikimaliza deni utakatalia simu yangu?
Hivi hela unazokopa Huwa zinalingana thamani Na bima uliyoweka?
 
Maana hio ni kama bond endapo umetimiza matakwa yao yote una haki zote za kurudishiwa bond yako hio maana hata mahakamani ukipeleka hati kama bond kesi ikiisha unarudishiwa hati zako iweje hizo hela umerudisha na riba juu wao wasirudishe?
Sidhani kama bond inalingana Na hiyo Bima.Bond unaweka kitu ambacho thamani yake inalingana Na ile hela unayokopa.Unaweka bond kama nyumba,ukishindwa kulipa wanauza tu nyumba.Sasa hii Bima ya mkopo wa Benki Ina thamani sawa Na hela unazokopa?
 
Swali: Kama usingemaliza mkopo, je unafikiri kile kiasi ulichokatwa kama bima kingetosha kulipia mkopo uliobakiza?? Je? Kama hakitoshi fedha nyingine inatoka wapi kulipia deni lako?
Swali zuri
 
Unatufungua macho mkuu,hiyo cover note inakuaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…