Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Kwanini Mabenki hayarudishi pesa wanazokata kama " Bima ya mkopo pindi deni la mhusika linapoisha

Witmak255

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2019
Posts
3,264
Reaction score
5,419
Habari zenu wanajamvi
Miaka sita (6) iliyopita nilichukua mkopo bank ya CRDB kwa dhamana ya utumishi na marejesho yakiwa yanakatwa moja kwa moja kwenye mshahara, moja ya masharti ya ule mkopo ilikuwa ni lazma ukatiwe bima dhidi ya kifo au ulemavu wa kudumu, maafisa mikopo wa CRDB walinielimisha vizuri sana kuhusu hii bima amabayo wanaikata kwenye kile kiasi ulichoomba mkopo, nadhani ni kama 200k+ kama sikosei.wakanielieza kwamba

Kile kiasi cha pesa kilichokatwa kwenye mkopo nilioomba kama Bima kinasimamia upotevu wa fedha,mali iliyokatiwa Bima kutokana na kutokuwepo kwa uaminifu kutoka kwa waajiri wakati wafanyakazi wakiwa kazini. Bima hii pia inasimamia usalama wamali iliyochukuliwa kama dhamana. Wakaendelea kusema,

Bima hiyo inalipia hasara ya fedha anayoipata mkopeshaji ( ambao ni wao CRDB Bank) kutokana na matatizo aliyopata mdeni kufuatia majanga ya kifo au ulemavu wa kudumu kabla hajamaliza kulipa deni. Husaidia kupunguza hasara ikilinganishwa na dhamana iliyowekwa. Kwa wakopaji wasio na dhamana za kazi Bima hii ina hakikisha familia ya mhanga haiachwi bila makazi au mzigo wa kuendelea kulipia deni linalodaiwa pale mkopaji anapofariki au kupata ulemavu wa kudumu.

HOJA YANGU
Deni langu lilikuwa la miaka mitano (5) na mwaka jana nilimalizana na hili deni, yaani hawanidai tena tangu mwaka jana, nilitegemea baada ya deni kumalizika hawa CRDB bank wanirudishie ile pesa yangu Zaidi ya 200K kwa vile mkopo wao tayari nimeurudisha wote pamoja na riba na bila usumbufu, mwanzoni mwa mwaka huu niliwatumia barua kuwakumbusha kuhusu kunirejeshea hii pesa hawajanijibu hadi leo, jana nimewatumia email kupitia kwa DG wao bado pia naona kimya.

Hii kitu imeekaaje kwa hapa bongo, au ndo bank inadhulumu wateja wao…, nakumbuka nilikopaga pesa stanbic bank nikiwa Kenya kwa mda wa mwaka mmoja na baada ya mkopo kuisha nikarejesehewa hii pesa tena wakani email kabisa kunitaarifu.

Najua wakopaji kwenye hizi taasisi za kifedha wako wengi na najua na wao hawajui kama wanatakiwa kurudishiwa hii pesa baada ya mikopo kumalizika , naombeni kujulishwa kama hapa bongo hii pesa huwa hairudi hata kama deni lao umemaliza lote?
 
Umeongea kitu cha maana wengi wengi huwa hawatilii maanani ili lakini unapoint ya msingi sana kama mkopo umenda smooth kuna kila sababu ya kurefund hii pesa, labda endelea fatilia zaidi tujue sheria zetu zinasemaje
 
Fuatilia tu kwa umakini pengine utaeleweshwa na wahusika
 
Sidhani kama ni rahisi kurudishiwa bima ya mkopo kwa sababu hata wao benki hiyo hela wanayokukata kama bima wanaenda kuilipa kwenye kampuni ya bima na hawabaki nayo kama faida.

Mfano mzuri umekata bima ya gari lako hauwezi kwenda kudai kwa sababu eti gari lako halijapata ajali katika huo mwaka husika ambao umekata bima.
 
Umeongea kitu cha maana wengi wengi huwa hawatilii maanani ili lakini unapoint ya msingi sana kama mkopo umenda smooth kuna kila sababu ya kurefund hii pesa, labda endelea fatilia zaidi tujue sheria zetu zinasemaje
Ndio mkuu lazima warudishe, vinginevyo watakuwa wanawaibia wateja wao
 
Hatimae ufumbuzi wa vitu visivyoeleweka unaweza patikana..
 
Wakati unachukua mkopo ulisoma masharti na vigezo mkuu?lile karatasi lenye maelezo mareeefu ambayo usipoangalia kwa sababu unakuwa na kiherehere cha kuchukua mkopo unajikuta unasainishwa rundo la mafomu bila ya hata kusoma,nina uhakika hapo ndio pana haya maelezo yote...
 
Sizani kama ni rahisi kurudishiwa bima ya mkopo kwa sababu hata wao benki hiyo hela wanayokukata kama bima wanaenda kuilipa kwenye kampuni ya bima na hawabaki nayo kama faida.
is this true? nani ananiwekea sign huko kampuni za bima kwamba nimelipa mimi?
 
Wakati unachukua mkopo ulisoma masharti na vigezo mkuu?lile karatasi lenye maelezo mareeefu ambayo usipoangalia kwa sababu unakuwa na kiherehere cha kuchukua mkopo unajikuta unasanishwa rundo la mafomu bila ya hata kusoma,nina uhakika hapo ndio pana haya maelezo yote...
nijulishe kama unajua mkuu, ishu ni hii pesa ya bima natakiwa nirudishiwe au la?
 
ngoja niende NMB fasta wanirudishie hii pesa yangu, maana tayari nshalipa deni pamoja na riba so nawafuata kesho asubuhi
 
una point ya msingi, hata mimi inabidi nianze kuulizia
 
yes bank inatakiwa ituambie ukweli, la sivyo watakuwa wanatupiga pesa nyingi sana
Maana hio ni kama bond endapo umetimiza matakwa yao yote una haki zote za kurudishiwa bond yako hio maana hata mahakamani ukipeleka hati kama bond kesi ikiisha unarudishiwa hati zako iweje hizo hela umerudisha na riba juu wao wasirudishe?
 
kabisa mkuu, hapa mimi itabidi wanirudishie tu maana nitawasumbua sana
 
Bima hairudishwi mkuu, tafasiri nyepesi ni kuwa wakati wewe umerejesha mkopo smooth, kuna mwingine hakurejesha kabisa labda kafariki, kwa hiyo kiasi ulichotoa wewe na mwingine na mwingine kama bima kinaenda kufidia deni la yule ambaye hakurejesha kwa sababu hizo. Mfano bima ya afya, usipougua wewe katika kipindi hicho cha bima haina maana kuwa pesa yako utarudishiwa, kwani kuna mwingine kanufaika kupitia pesa yako ( kwa kupata matibabu zaidi ya kile alichochangia katika bima yake.
 
Mi nimemaliza mkopo iwaje nilipe fidia ya wengine bado jibu halijakaa sawa
 
Back
Top Bottom