Kuna madada wawili watatu nawajua ambao walikuwa na maringo balaa siku za nyuma lkn oversudden nawaona wanabadilika kwa kasi ya 4G.
1.Mfano kuna mmoja nilisoma nae siku za nyuma,alikuwa montress alikuwa hanipendi balaa yaani kwa siku alikuwa ananiandika mara tatu swahili speaker lkn cha ajabu jana ananitumia txt eti MSAGA SUMU hivi unajua nilkuwa nakukubali tokea siku ya kwanza.
2. Kuna dada mwingine alikuwa CRDB kijitonyama kaunta,niliwahi kumuomba chenji ya buku 10,aisee aliniangalia jicho baya halafu akaniambia niende kwenye ATM kuchukua chenji, basi leo nimeenda na mishe zangu zingine ile kuniona tu akaniwahi kaka unahitaji chenji? Nikisema tayari nimeisha chenji kwenye ATM.
Wadau hii hali inaweza kuwa inasababishwa na hasara zinazopata hizo benki au vipi? Au ndo wanajua kuwa kuna layoff za maana inafuata so wanaanda mazingira mazuri ya sisi madalali kuuza magari yao ya mkopo?
Au kuna kitu kingine mimi sikijui?