Najiuliza sana ni kwa nini madactari walio wengi huwa hawaamini kuwepo malaria sugu ?
Yaani mgonjwa anatumia dose kamili tena baada ya kuthibitisha kuwa anao parasites wa malaria, lakini baada ya wiki tatu ni mgonjwa tena na kuthibitisha kwa kupima vile vile ,
Anaamua kubadili dawa na kukamilisha dose bado yana jirudia yale yale kila baada ya wiki tatu hadi mwezi miaka nenda rudi ?
wakati mwingine unaweza kudhani doctor hajatilia maanani tatizo lako, ila kumbe sio, amekusikia na anatamani kufanya kutu kikubwa kwa ajili yako ila tatizo ni muda tu wa kukufuatilia na kanuni za kazi