Kwanini Madaktari wengi wahuni?

Kwanini Madaktari wengi wahuni?

BICHWA KOMWE -

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2022
Posts
6,373
Reaction score
16,073
Hawa madaktari wa siku hizi ni kama wamevamia fani?

Haswa haswa hawa vijana walioajiriwa karibuni, hawajui maadili ya kazi wala hawajui kuhudumia wagonjwa.

Ukizungumza nae hakusikilizi, yuko bize anachati WhatsApp halafu kaweka earphones. Kavaa mlegezo na KIDUKU. Ati daktari!

Sijui walifunzwa wapi hawa, anakujazia madozi chungu mzima bila hata kujua unaumwa nini kwa hakika! Yuko bize na simu anafuatilia udaku wa INSTAGRAM.

Ni tofauti kabisa na madaktari wa zamani, ukifika unasikilizwa kwa makini, unahojiwa, unachunguzwa, unaambiwa achama mdomo aaaahhh, unaachama mdomo, unakaguliwa macho, yaani hadi raha!

Lakini hawa vibushuti wa mwendokasi wa siku hizi wanaovaa milegezo, bure kabisaa!

Nitaanza kwenda hospitali na bakora, ni mwendo wa kuwatandika kweli kweli.

Kama waajiri wao wameshindwa kuwadhibiti, nitafanya mwenyewe. Ni bakora tu mpaka wanyooke.
 
Hawa madaktari wa siku hizi ni kama wamevamia fani?

Haswa haswa hawa vijana walioajiriwa karibuni, hawajui maadili ya kazi wala hawajui kuhudumia wagonjwa...
Si kwamba natetea ila hio ipo kila mahali, hata maofisi yenu ukifika utakuta vidada visecretary vinajivuta, vinajishaua, vimekunja mdomo kama vile vinalipwa millioni 10 kumbe laki3 tuu
 
Back
Top Bottom