Kwanini Madaktari wengi wahuni?

Wahuni wako kila mahali, Polepole nae alilalamika huko CCM kuna wahuni pia.
 
Well said.
 
Usikute umekutana na Intern anayejifunza kazi.

Anyway somehow uko sahihi sana.
 
Watu waache ushamba,jaji mkuu wa Kenya alikuwa anavaa hereni.
 
Hii nchi ni ya kipumbavu kuliko unavyoweza kudhani. Madaktari wazuri wapo mtaani; hospitali nyingi za umma zimejaa madaktari wa ovyo wanaojiriwa kwa vimemo na kujuana.
hakuna cha dakitari mzuri yuko mtaani wala nini, ni vile mazingira yake ya kazi yanambana, mfano wengi wako Private hospitals codes of conduct haziruhusu(ama zinasimamiwa ipasavyo), nae akiingia kwenye mfumo huu wa vijana wa serikali(wengi wao) atakua hivyo hivyo

mtoa mada yuko sahihi, hivyo viduku na milegezo sidhani kama vinaashiria ujanja wowote hasa kwa madakitari, sana sana ni wagonjwa kupunguza imani kwao

lakin kwa watu wa kada nyingine mfano IT mm naona ni sawa tu, kozi zao zimekaa kijanja zaidi, zinahitaji mtu mjanja mjanja wa kucheza na mifumo, na uvumbuzi kibao, so hata akiamua kua hivyo mm sioni shida, anadeal zaidi na vitu

Lakini medicine is Life,
 
Mimi daktari alienyoa kiduku kavaa bana suruali sijui busy na simu nitamfokeaa hatoamini na cha kunifanya atakosaa. Kwanza kidaktari kidogo dogo No plz Aniachee nife Asinihudumie
I
Aki ku overdose si utakufa. Usibishane na daktari. Fuata kilichokupeleka.
Tunamlaumu nani wakati hao madaktari ni watoto wetu wenyewe, kwani wamelelewa kenya ? Wayoyo wana misbahave tunawaangslia tu sasa ni muda wa kuturudi.
Kazi kusema dio mtoyo wangu atajuana na wazazi wake, kumbe kuns mda au mahsla mtakutana na huyo mtoto, we gine mtawakuta mahajamani, TAMISEMI, polisi, migration, shileni.
Tuwe wapole tu wameharibika tukiwaona na pengine tumechangia kuwaharibu.
 
Kosa ni kurahisisha taaluma, Zamani kupata PCB division 1 ilikuwa ngumu,hata masomo ya udaktari siku hizi ni shallow shallow tu mradi wamalize, MD wa sasa ukimuweka na RMA wa zamani MD anaweza akapigwa nje.

Zamani kupata material, past papers na lecture nzuri za walimu wanaojua kufundisha ilikuwa kazi ngumu sana.

Now days zama za internet kila kitu kinapatikana kwa wepesi.

Youtube kuna walimu wa kila kitu.

Quora kuna wataalamu wa kujibu maswali ya kila tatizo.

Hapo lazima watoto wapige division one kwa wepesi kuliko zamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…