Kwanini Madereva wa Mabasi huwa wana haraka hata kama sehemu haiwaruhusu kupita wanalazimisha?

Prince05

Member
Joined
Feb 27, 2024
Posts
18
Reaction score
29
Tabia ya madereva wengi wa mabasi Tanzania kuvunja sheria au kuwa na haraka kuliko watumiaji wengine wa barabara ni chanzo cha ajali nyingi. Ifikie wakati wamiliki wasifumbie macho tabia hii. Serikali pia iwawajibishe wasiangalie makosa ya vibao vya 50 tu au kuzidisha abiria kuna tabia nyingi sana hatarishiri kuliko ambazo wanazozitilia mkazo.

Your browser is not able to display this video.
 
Dawa ya huu UJINGA ni kuweka miundombinu mizuri ya treni pia usafiri wa ndege ukiwa nafuu hakuna MTU atapanda mabus.
Kwa mfano treni kutoka DAR Hadi mwanza itakuwa Tsh 70-80 ni abiria gani mjinga atapanda bus?
Mwisho wa siku biashara ya mabus itajifia tu
 
Ushasema wana haraka sasa unataka tukujibuje mkuu mtoa uzi
 
Madereva wakorofi na wanaoendesha ovyo dawa yao ni Latra kuweka sheria ya lazima(mandatory) kila basi ya abiria iwe na dashboard camera na iwe Connected na Polisi,Latra,mmiliki.

Hii itakuwa dawa ya Madereva wanaofanya uzembe,kuovateki ovyo,uchovu,kuendesha masaa mengi bila kupumzika na itasaidia kujua chanzo cha ajali kwa haraka. Na kampuni isiruhusiwe kufuta kumbukumbu pasipo kutoa taarifa
 
Wanakula na wakubwa, na jamaa hawajari muendesha kwa miguu au boda, i hate those guys.
 
Nikiwa naendesha piki piki huwa naona niko safe haijalishi niko speed kali namna gani

Lakini kama anaendesha mwingine amani sina

Kile uonacho wewe ni hatari, Dereva haoni uhatari huo kama wewe uonavyo
 
Haraka zile sio zao ni jumla ya haraka zoote za abiria wake.....ndio anazibeba yeye...upoo ?
 
Sio dereva sema abiria kwasababu abiria ndivyo wanavyo taka na wanatimiza kulinda brand .
Weka mabasi 2 muja litoke saa 1 lifike saa 6 na lingine nitoke muda huohuo ila lifike saa 10 af uone lipo litajaa kabla
 

Hii nchi ngumu mkuu wala hilo sio suluhisho. We hushangai Kila bus limefungwa king’amuzi cha kucontrol speed ambapo mfumo huo upo connected na traffic/polisi. Ila ni marangapi unatembea na bus king’amuzi kinapiga kelele kwamba dereva kazidi speed? Ulishawahi kuona bus limesimamishwa kwa kuzidisha speed? Watu wanakula kwa urefu wa kamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…