Kwanini madereva wetu wa Kiafrika hawawezi kufuata sheria za barabarani hadi wasimamiwe?

Kwanini madereva wetu wa Kiafrika hawawezi kufuata sheria za barabarani hadi wasimamiwe?

HOPEfull

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
1,882
Reaction score
2,313
Niko barabarani kwa mguu natoka mahali kwenda mjini kuna basi ya abiria imepita kwa speed sio nzuri sana eneo ambalo halitakiwi.

Sijajua hivi vibao vinavyoonyesha speed ya gari ya kutembea eneo husika vina maana gani kwa sisi madereva wa kiafrika.Sijajua alama za pundamilia za kuvuka watembea kwa miguu zina maana gani kwa sisi madereva wa Kiafrika.

Kibao kina kinaonyesha mwendo wa kutembea eneo husika lakini unashangaa gari inakuja speed kubwa na dereva anapiga honi mfululizo za ovyo kama yuko kwenye msafara wa harusi wakati eneo husika linaonyesha mwendo wa kawaida usiohitaji hata kupiga mluzi.

Kupiga honi nyingi za ovyo inaonyesha mwendo wa rough na usio makini.Derava mzuri haitaji honi nyingi na za fujo.

Wakati mwingine madereva tunajitakia wenyewe matatizo au ugomvi na watuwa usalama. Tunaweza tukawa tunawalaumu bure tu watu wa usalama.
 
Mkuu, wewe umeona barabarani tu?

Vipi vyoo vya umma, masokoni, ndani ya hilo basi ulilopanda, barabarani(mtu anakula ndizi au muwa maganda barabarani), makopo ya plastic (sijui kwa mini Serikali haijapiga marufuku machupa ya plastic?), nk
 
Umasikini tu, we ukishaona jitu linaambiwa na demu kuwa ana ngoma lakini bado linataka tena kula peku, kuna shida mahala ndiomaana wazungu wanatushangaa sana, MIAFRIKA NDIO TULIVYO
 
Unapogundua kwamba kila unapovunja sheria, hakuna adhabu yoyote unayoipata, hayo ndio matokeo yake. Sheria bila enforcement ni bure kabisa.

Ingawa kazi ya udereva inaajiri watu wengi sana, lakini bido haijawa a professional career. Ni kazi ambayo bado inafanywa na watu wapuuzi sana.

Nchi haina shule mahsusi za kufundisha watu jinsi ya kuendesha gari na kufuata sheria barabarani (Driving Schools)

Utingo wa Lori au dalala anakuwa dereva baada ya miezi 6 ya kukaa pembeni mwa dereva bila hata ya kusoma sheria za barabarani. Hapa unategemea nini? Na akivunja sheria, anapenyeza rupia kwa askari, maisha yanaendelea. Kesho yake...Lorry limeua watu 20! Hakuna anaejali.

1984, Tanzania [emoji1241]ilipoteza Waziri Mkuu wa nchi kutokana ajali za barabarani. 37 years later, hakuna anaejua la kufanya.
 
1984, Tanzania
emoji1241.png
ilipoteza Waziri Mkuu wa nchi kutokana ajali za barabarani. 37 years later, hakuna anaejua la kufanya.

Mkuu hicho kipande hapo juu ni conspiracy.....kuna wanao sema ni Framed
 
Ndio hivo tena... conspiracy theory kuhusu ule msiba zilisemwa sana lakini zimebaki hivyo hivyo. Si marehemu baba wa Taifa (Mzee Nyerere) au hata Mzee Mkapa waliegusia kuhusu suala hilo.

Muhimu ni kwamba nchi ilipoteza kiongozi mahiri na mzalendo kwa sababu ya ajali za barabarani. Morogoro bado ni machinjio ya binadamu. Labda (M/Mungu apishie mbali) yakimkuta kiongozi mwingine wa Serikali ndipo hatua imara za usalama barabarani zitakapochukuliwa.

Ni dhahiri kwamba vifo vya wananchi wa kawaida havivishtui vyombo husika.
 
Back
Top Bottom