Kwanini maeneo mengine nchini hayajengi vituo vya afya (kipekee Moshi Vijijini/ Vunjo)

Kwanini maeneo mengine nchini hayajengi vituo vya afya (kipekee Moshi Vijijini/ Vunjo)

NorthJuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2017
Posts
396
Reaction score
257
Pongezi kwa Wilaya zote nchini ambazo zimekamilisha/zinaendelea kujenga vituo vipya vya afya kwa fedha za Serikali.
Katika Wilaya ya Moshi Vijijini (Vunjo) kwa miaka mingi maeneo ya Kitowo, Kirararacha, Kyala, Komalyango, Nduweni, na maeneo mengine mengi ya Moshi Vijijini/Vunjo hayana vituo vya afya, hata hizo zahanati za akina mama na watoto wanazisikia kwenye radio tu.

Mgonjwa/ Mjamzito analazimika kutembea umbali mrefu mpaka kwenda Hospitali ya Kilema kupata huduma.
Wale wakazi wa Moshi Vunjo/ ambao wamekuwa wakisumbuka na adha hii, hii ndiyo fursa yenu ya kumuuliza Mbunge Mh. James Mbatia na watangulizi wake, Mh. Augustino Lyatonga Mrema n.k. ni kwanini Vunjo hakuna miradi kama hiyo ya maendeleo kwa wananchi? Ni fedha hakuna? ama hazijatolewa? Na pesa za jimbo zinafanya kazi gani? hasa Mh. James Mbatia Mb. jibu swali hili maana 2020 siyo mbali.

Swali hili pia linahusu wabunge wote katika majimbo yote nchini ambao wamelala katika swala la ujenzi wa Zahanati katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi.
 
Pole huko unakosema kuna hospital kubwa achana na ya KCMC... Huruma Rombo, Kilema, na Marangu hospital Headquarter kuna hospital pia.... mwache mbunge wetu msomi ndugu mzalendo James Mbatia...............

Kimaro si alikuwa Mbunge alifanya nini zaidi ya kukaanga maandazi NAKARA
 
Acha masikhara ww, yaani mgonjwa utembee kutoka Posta mpaka Mbezi kwa miguu kufata huduma katka hospitali kubwa unaona iko sawa? Kwa nn zisijengwe hizo zahanati maeneo hayo?
 
Back
Top Bottom