Kwanini magolikipa siku hizii hawavai track wakiwa mchezoni kama zamani?

Magoli kipa wa kisasa ni wachezaji kama wa ndani, zamani kazi ya goli kipa ilikuwa kudaka ila Kwa Sasa anavaa pensi ili apige mashuti mbali
 
Zamani viwanja vilikuwa Kipara,yaani golini kulikuwa hakuna majani,ukijaribu kujirusha upande lazima utoke na Mashilingi(Ile michubuko kipindi hicho ndiyo tuliita)Kwa hiyo vibukta vilikuwA havisaidii kitu.
 
Viwanja vya sasa vingi ni vya kisasa na vina nyasi za bandia, hivyo magolikipa wa sasa hawahitaji kujilinda kuchubuka kwenye viwanja vya viwango vya chini kama vya kale.


Pia magolikipa wa sasa wapo tofauti na wazamni kiuchezaji , sasa hivi walimu wengi hupenda kuanzisha mashambulizi kutokea kwa magolikipa na sio kubutua tu mbele , hivyo magolikipa wanahitaji mavazi kama ya wachezaji wengine kurahisisha mfumo huo wa uchezaji🤔🤔🤔🤔
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…