Kwanini magonjwa ya figo, ini pamoja na mapafu yanaondoa vijana wengi sana?

Kwanini magonjwa ya figo, ini pamoja na mapafu yanaondoa vijana wengi sana?

Niamini mimi. Dawa ni moja tu kupunguza ama kuacha kabisa matumizi ya sigara pamoja na pombe kali. Zile spirits si kila mtu zinamfaa, Wengine kwao zinawadhuru. Ni vyema mtu ukaacha tu mambo ya kisasa yakupite ili uwe salama.
 
Zamani ilionekana UKIMWI ni tishio kwa Dunia nzima, kwa dhana kwamba ni lazima mtu atakufa tu.

Siku hizi magonjwa ya ini, mapafu kujaa maji, Figo kushindwa kazi yake yamekuwa tishio sana na yanaondoa uhai wa watu wengi sana hasa vijana.

Sijui sababu kubwa ni matumizi ya pombe au sigara bila kula vizuri, kunywa maji mengi n.k?

Lakini mbona wazee wetu wanakunywa pombe miaka nenda rudi lakini hawasumbuliwi na magonjwa haya kama vijana wa leo?

Madaktari wameshindwa kabisa kuthibiti vifo vya magonjwa haya kiasi kwamba mtu akishaumwa tu haya magonjwa anahesabu kifo wakati wowote.

Kwanini yameshindikana?

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Hayo ni magonjwa yanayokuja na ukimwi na side effects za dawa za ukimwi.
 
DOUBLE KICK.hii pombe imemuua dogo mmoja alikuwa anapiga debe bajaj za mapinga pale bunju b.alikunywa jumamosi akaamka nayo jumapili.akachukua nyingine akaweka kwenye chupa ya maji.watu wakajua anakunywa maji kumbe double kiki.ilipofika saa 6 mchana mtu akaanza kubadilika macho yamemtoka wakaanza kumsugua kwa malimao kwenye nyayo.akaingia kwenye coma.mtu kalala tu.mpaka saa 3 usiku .wanakuja kupata akili ya kumpeleka hospital saa 5 usiku kufika bunju a wakamshindwa wakaambiwa wampeleke muhimbil.kafia huko.
 
Acha uongo jamaa..uli wapima..?na pia takwimu nyingi zinaonyesha magonjwa yasiyo yakuambukiza ndio yanaongoza kwa vifo..magonjwa nyemelezi ambayo ni ya kuambukiza ndio yanayo wapereka wenye ngoma..rudi shule boya wewe.

#MaendeleoHayanaChama
Unafikiri mtu akifa kwa figo watasema kafa kwa ngoma? Ngoma ndio inaleta hayo magonjwa yasiyoambukizwa sasa. Ngoma ndio mfadhili mkuu wa magonjwa hayo, ni kama Master hivi.
 
Pombe na sigara kupitiliza ,,pia kuna hizi sumu tunakula kila siku kama sukari especially ya kwenye bidhaa za viwandani kama juice, soda,pipi nk. Mafuta ya kupikia yanayotokana na mbegu ni hatari sana lakini ukijumkisha na madawa yanayopigwa kwenye mazao,mboga basi ni kama tunakula sumu inayotuua taratibu [emoji27][emoji27] .
Mkuu umenishtua ina maana mafuta ya mbegu za alizeti hayafai kwa matumizi?
 
Inatokana na unywaji wa pombe kali kwa sanaa bila chakula kizuri au chenye afya, lakin wazee walikuwa wanakunywa lakin kula ni uwakika sio sasa hivi kijana anakunywa pumbe kali lakin uwakika wa chakula cha kushiba hawana, ndo wanaishia kula chipsi mayai wakati wazee wanaamka wanakula supu nzito asubui mchana ugali nyama na usiku anakula nyama choma so hapo anajenga mwili vizur tuu, sema sasa vijana akiamka cha kwanza anataka chipsi ambapo kula kula tena mpaka usiku na usiku anakula tena chipsi ,
kwa nini magonjwa kama hayo yasiwanyemelee
 
Ngoma ndio inaondoa watu, vile tu ngoma sio ugonjwa bali ni hali...

Ndio maana yanatajwa magonjwa nyemelezi ambayo hutoa uhai wa wahusika...

Ukiacha hilo, matumizi makubwa ya pombe na vilevi vingine ambavyo kwa kiasi kikubwa ni chanzo cha magonjwa yasiyoambukizwa
Madawa ya kufubaza yanachosha ini na hatimae kuua figo!
 
Aisee!!!
Unaweza kufa ghafla bila kuumwa chochote..hapo ndipo utajua haujui.
 
Check hizo link hapo juu ambazo nimepost,,,mafuta bora ya kula ni nazi,mawese,olive pamoja na animal fats . Hushangai mtu akiwa na pressure anatakiwa kuacha kutumia mafuta ya kupikia,sukari nk! Maana yake hiyo ni sumu inayoua taratibu.

Which animal fat mkuu? Hata yanayotokana na nguruwe!? Maana yule anatoaga sana mafuta
 
Check hizo link hapo juu ambazo nimepost,,,mafuta bora ya kula ni nazi,mawese,olive pamoja na animal fats . Hushangai mtu akiwa na pressure anatakiwa kuacha kutumia mafuta ya kupikia,sukari nk! Maana yake hiyo ni sumu inayoua taratibu.
Duh
 
Which animal fat mkuu? Hata yanayotokana na nguruwe!? Maana yule anatoaga sana mafuta
Mafuta ya wanyama kama ng'ombe [emoji230], [emoji207], [emoji200] nk, Blueband (margarine) kaa nayo mbali sio natural fat.
 
Check hizo link hapo juu ambazo nimepost,,,mafuta bora ya kula ni nazi,mawese,olive pamoja na animal fats . Hushangai mtu akiwa na pressure anatakiwa kuacha kutumia mafuta ya kupikia,sukari nk! Maana yake hiyo ni sumu inayoua taratibu.
Olive oil hayatokani na mbegu mkuu?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom