... in brief ni "usanii wa wanasiasa". Actually, kilichopelekea kufanya hivyo kwanza ni kwa sababu kulikuwa na walakini mkubwa uchaguzi wa 2015 so, ili kujaribu kutafuta support of the mass, machinga ilikuwa kimbilio la kwanza.
Pili, Lowasa kupanda dalala kwenye kampeni za mwaka ule kwa CCM ilionekana kama inapoteza ushawishi kwa watu wa chini, so the best option kwa CCM kujionesha bado kipo na watu wa chini na sio chama cha matajiri na viongozi kama ambavyo ilikuwa inaonekana machoni pa umma, ni lazima hadaa za kila namna ilikuwa zifanyike kujaribu kuboresha "image ya chama" na kimbilio again ilikuwa machinga, bodaboda, na makundi ya aina hiyo.
Nirudie tena, zote hizo zilikuwa hadaa tu ili kupata support ya kisiasa bila kujali athari za approach hizo! Matokeo yake umaskini umezidi kuongezeka nchini kwa kiwango cha kutisha, gharama za maisha usiombe, miji imekuwa shaghalabagala, diplomasia imevugwa kwa kwango ambacho hakikuwahi kufikiriwa, just to mention few.