Kwanini Mahouse girl wanaongea sana na simu kama call centre/phone operator

Kwanini Mahouse girl wanaongea sana na simu kama call centre/phone operator

ubarinolutu

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2012
Posts
2,424
Reaction score
4,954
Toka hii dunia naifahamu nimeweza kujionea watu wanaoongea na simu mara nyingi sana, kwanza ni Hawa watu wa call centre /phone operators wa makampuni makubwa kama TANESCO na mitandao ya Simu, Hawa masaa ishirini na nne ni simu tu , hakuna kingine shift Kwa shift ni simu tu.
Ukiachilia watu hao, wengine wanaopenda kuongea na simu au Wana ugonjwa wa kuongea na simu muda mrefu ni Hawa dada wa kazi, au kwa kizungu wanaitwa house girls, house maids
Hawa wadada wa kazi kwanza sielewagi wanaongea na nani muda wote, mazungumzo Gani yasiyo na mwisho, wengine wanaenda mbali zaidi na kuongea Kwa kilugha example Kisukuma.

Nimejaribu kubadili wadada wa kazi wengi lakini it seems wote Wana hiyo inherent character ya addiction ya kuongea na simu, anaosha vyombo simu, usiku wa manane simu, anapika simu, Sasa ni kina nani hao Kila siku Kila anakuwa tu anaongea nao Kwa simu, hii kitu inaniwazisha.

Sasa Kuna mmoja mama watoto alimpa sharti aongee au ashike simu pale ambapo anakuwa kamaliza kaI zake yaani mda wa kupumzuka, aliweza siku mbili tatu, akaona ni mateso akatoroka bila kuaga.
Sasa wanajamvini hizi simu za wadada hatuwakatazi lakini zinapunguza ufanisi, hivyo naombeni ushauri wenu namna ya kudhibiti hii tabia Ili mambo mengine yafanyike Kwa ufanisi
 
Aisee hawa wakuu ndio wanatajirisha makampunj ya simu, kila saa simu sikioni, yaan unakuta anauliza habari za kila mtu kijijini kwao...
Kuna mmoja nilipiga akawa ananipigia simu usiku na nyimbo za rayvan ananiimbia, nishida kwelikweli
 
Wakwangu nilijikoroga nikampa smartphone 😂😂😂😂.
Mshahara wote unaushia kwenye vocha aingie tiktok. Kulala ni saa 9 usiku, simu kila mahali. Hadi nimejuta kumpa simu nikawaza niichukue ila nikaona sio poa.
 
Wakwangu nilijikoroga nikampa smartphone 😂😂😂😂.
Mshahara wote unaushia kwenye vocha aingie tiktok. Kulala ni saa 9 usiku, simu kila mahali. Hadi nimejuta kumpa simu nikawaza niichukue ila nikaona sio poa.
Pole sana 🤣🤣
 
Back
Top Bottom