Kwanini mahusiano/ndoa nyingi hazidumu?

Familia imekuwa kama familia ya kambale wote wana ndevu hamna anaye kubali kushuka chini,kila mtu mbabe (hasa kwa baadhi ya dada zetu wasomi/wanaharakati/matajiri) Siku hizi hamna,upendo wala kuvumiliana mkizinguana kila mtu na lake.

Yaani tuna tengeneza kizazi cha ajabu kijacho ambacho kinalelewa na mzazi mmoja ,kwa sasa huwezi ona ila huko mbele NDOA,FAMILIA zitakuwa hazina maana kwa baadhi ya watu.Watajiona wajanja ila wakikaribia 35+ ndipo watakapojua nini maana ya family na nini umuhimu wa ndoa na malezi ya wazazi wote wawili.

Ila siku zote mkiachana mnayemuumiza ni mtoto,kuna utofauti mkubwa sana kati ya mtoto aliyelelewa baba na mama na aliyelelewa na mzazi mmoja,siku zote hela hazilei mtoto ila upendo wa baba na mama ndio unao mlea mtoto.
 
Huuu...mfumo wakuwafanya Watu ma Padre na masista una mazaifu mengi Sana.

Kama unauthibitisho wa tuhuma zako..peleka mahala husika.
 
Speaking from my experience as a married woman ili ndoa idumu inahitaji uvumilivu mwingi, uwazi katika kuwasiliana , kukubali tofauti za mwenzako, kujishusha pale inapobidi na kuomba sana Mungu awape hekima ya namna ya kuishi pamoja. Sio rahisi, ila ukiamua inawezekana.
 
Kwiayo ili ndoa zidumu..wanawake wavumilie Kila Aina ya vituko KUTOKA kwa wanaume..

Ndo wale wanawake mwanaume anamuacha na watoto wanne...Mwanamke anaangaika

Alafu baada ya Miaka 25..anarudi akiwa mzee Hana nguzu Tena Wala Mali na Ni MGONJWA..

Eti nisamehe mke wangu...naumwa niuguze
Mke baada ya Miaka 25 yakuomba mume arudi...anaenda kutoa sadaka ya shukurani kwa kujibiwa maombi.

Ndoa inaitaji Watu wawili waijenge...Tena kwa nguvu zao Zote.. huwezi MUACHIA jukumu mwanamke TU la kulinda ndoa na kutunza ndoa..kwanini
 
Kuna wanaume vimeo balaa lakini haisemwi wanawake ndio wanatakiwa kuvumilia kwa mtazamo wa wengi.

Ndoa ni ya wawili.
 
Napozungumza haya lengo si kubishana ila ni kukuonesha kiasi gani mnafeli. Hata vitabu ya dini vyasema, "pepo ya mwanamke ipo mikononi mwa mumewe"

Haimaanishi kwamba wanaume hawana mapungufu ila mwanamke ana mchango mkubwa katika kusawazisha hayo mapungufu ikiwa atakuwa na hekima na uvumilivu.
 
Kuna wanaume vimeo balaa lakini haisemwi wanawake ndio wanatakiwa kuvumilia kwa mtazamo wa wengi.

Ndoa ni ya wawili.
Sasa mwanaume wako kimeo, umechukua approach gani ili kuhakikisha unasawazisha tofauti zenu? Kum frastruate ndio suluhu au kudai divorce?
 
Uko sahihi kabisa sema tu kuna kitu kimoja umekisahau na ambacho ndo kinatesa ndoa nyingi leo
Siku hizi mwanamke unaweza kuwa mtii kwa mumeo,ukamfanyia kila kitu ila atakukosea heshima mno kwa kuwa na michepuko ya kila aina tena bila hofu!
Kwa hali ya kawaida hii huleta maumivu makubwa sana kwa mwanamke mwishoe nae anaona liwalo na liwe ndo hapo unasikia wanaanza kusema mwanamke mjeuri kumbe nyuma kuna chanzo!
Nnachojua wanawake wengi wamejeruhiwa hisia zao na waume zao ndo mana nao mwisho wanaishia kureact negatively,japo wapo wachache ambao their case is different
 
Daaah hatari sana nimecheka sanaaaaa
We jamaa ni shidaaa kwani ni kosa kuwa na mtoto mzee?
 
Hapo ni balaa, mwanamke anatakiwa aishi katika kutii mamlaka. Mambo ya haki za jinsia sijui mashindano ndio shida. Halafu wazazi nao pia wako biased kwa kutetea watoto wao zaidi. Ila mie ntasikiliza case ilivyo kama ni upuuzi natia binti makofi na kumuamuru arudi kwa mumewe haraka.
 
Upo sahihi kamanda. Muna baba namjua alikatwa mguu kisa kisukari na alikua na wake wawili. Mke wa kwanza kamkimbia kisa jamaa mlemavu na hapigi show(kwa maneno ya wanaomzunguka) ila mke wa pili ndiye anayemtunza na ni msataarabu yule mama na heshima anayo. Hana skendo ya kuwa na mwanaume mwingine zaidi ya yule bwana.

Kwakweli jamaa amepata mke aisee
 
Daaah hatari sana nimecheka sanaaaaa
We jamaa ni shidaaa kwani ni kosa kuwa na mtoto mzee?
Huyo jamaa madai yake anani blackmail πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyo ndio mwanamke alielelewa katika mazingira kuwa mume ni mamlaka na anapaswa kuishi nae kwa hekima, utiifu na uvumilivu. Huyo mwanamke aliekimbia ametokea familia ya hovyo bila shaka ndio hawa kizazi cha .com!
 

Eti mlevi mmbwa [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

We mzee bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…